< Waefeso 3 >
1 Kutokana na hayo, mimi Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu kwa ajili yenu, namwomba Mungu.
For this cause I Paul am the prisoner of Jesus Christ for the sake of you Gentiles:
2 Bila shaka mmekwisha sikia kwamba Mungu, kwa neema yake, alinikabidhi kazi hii niifanye kwa faida yenu.
as ye have heard the dispensation of the grace of God, which was given me to preach unto you:
3 Mimi nilijulishwa kwa njia ya ufunuo mpango wake uliofichika. (Nimeandika kwa ufupi juu ya jambo hili,
that by immediate revelation He made known to me the mystery, (as I wrote before in brief, by which,
4 nanyi mkiyasoma maneno yangu mtaweza kujua jinsi ninavyoielewa siri hiyo ya Kristo.)
when ye read it, ye may perceive my knowledge in the mystery of Christ, )
5 Zamani watu hawakujulishwa siri hiyo; lakini sasa Mungu amewajulisha mitume na manabii wake watakatifu kwa njia ya Roho.
which in other generations was not made known to men, as it is now revealed to his holy apostles and prophets by the Spirit; that the Gentiles should be co-heirs,
6 Siri yenyewe ni hii: kwa njia ya Habari Njema watu wa mataifa mengine wanapata sehemu yao pamoja na Wayahudi katika zile baraka za Mungu; wao ni viungo vya mwili uleule, na wanashiriki ahadi ileile aliyofanya Mungu kwa njia ya Kristo Yesu.
and of the same body, and joint-partakers of his promise in Christ, by the gospel:
7 Mimi nimefanywa kuwa mtumishi wa Habari Njema kwa neema ya pekee aliyonijalia Mungu kwa uwezo wake mkuu.
of which I was made a minister, according to the gift of the grace of God conferred on me by the effectual operation of his power.
8 Mimi ni mdogo kuliko watu wote wa Mungu; lakini amenijalia neema yake, ili niwahubirie watu wa mataifa utajiri wake Kristo usiopimika,
On me, who am less than the least of all saints, was this grace bestowed, that I should preach among the Gentiles the unsearchable riches of Christ,
9 tena niwaangazie watu wote waone jinsi mpango wa Mungu uliofichika unavyotekelezwa. Mungu aliye Muumba wa vitu vyote alificha siri hiyo yake tangu milele, (aiōn )
and make all men to see the communication of the mystery, which from the ages past hath been hid in God, who created all things by Jesus Christ; (aiōn )
10 kusudi, sasa kwa njia ya kanisa, wakuu na wenye enzi wa mbinguni wapate kuitambua hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi.
that the manifold wisdom of God might now be made known by the church to the principalities and powers in the heavenly regions;
11 Mungu alifanya jambo hilo kufuatana na azimio lake la milele ambalo amelifanya kwa njia ya Kristo Bwana wetu. (aiōn )
according to the ancient purpose, which He executed in Christ Jesus our Lord: (aiōn )
12 Basi, katika kuungana na Kristo, na kwa njia ya imani katika Kristo, sisi tunathubutu kumkaribia Mungu kwa uhodari.
by whom we have freedom and access with confidence through faith in Him.
13 Kwa hiyo, nawaombeni msife moyo kwa sababu ya mateso ninayopata kwa ajili yenu, maana hayo ni kwa ajili ya utukufu wenu.
Wherefore I desire that ye would not be discouraged at my afflictions on your account, which is your glory.
14 Kwa sababu hiyo, nampigia magoti Baba,
For this cause I bow my knees to the Father of our Lord Jesus Christ,
15 aliye asili ya jamaa zote duniani na mbinguni.
from whom the whole family in heaven and on earth is named,
16 Namwomba Mungu, kadiri ya utajiri wa utukufu wake, awajalieni kwa uwezo wa Roho wake, nguvu ya kuwa imara ndani yenu,
that He would grant you, according to his glorious riches, to be strengthened with might by his Spirit, as to the inner man;
17 naye Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani. Namwomba mpate kuwa na mzizi na msingi katika mapendo
that Christ may dwell in your hearts by faith: and be ye rooted and grounded in love,
18 kusudi muweze kufahamu pamoja na watu wote wa Mungu jinsi upendo wa Kristo ueneavyo kwa mapana na marefu, kwa kimo na kina.
that ye may be able, with all the saints, to comprehend what is the breadth, and length, and depth,
19 Naam, mpate kujua upendo wa Kristo upitao elimu yote, mjazwe kabisa utimilifu wote wa Mungu.
and height, and to know the love of Christ, which surpasseth knowledge; that ye may be filled according to the abundant fulness of God.
20 Kwake yeye ambaye kwa nguvu yake ifanyayo kazi ndani yetu, aweza kufanya mambo makuu zaidi ya yale tuwezayo kuomba au kufikiria;
Now to Him that is able to do exceeding abundantly above all that we can ask or think, according to the power operating in us,
21 kwake Mungu uwe utukufu katika kanisa na katika Kristo Yesu, nyakati zote, milele na milele! Amina. (aiōn )
to Him be glory in the church by Christ Jesus, throughout all the generations of eternal ages. Amen. (aiōn )