< Mwanzo 8 >
1 Mungu akamtazama Nuhu, wanyama wote wa mwitu, na wanyama wote wa kufugwa ambao walikuwa pamoja naye kwenye safina. Mungu akafanya upepo uvume juu ya nchi, na maji yakaanza kuzama chini.
神记念挪亚和挪亚方舟里的一切走兽牲畜。 神叫风吹地,水势渐落。
2 Chemichemi za vilindi pamoja na madirisha ya mbingu vikafungwa, na mvua ikakoma kunyesha.
渊源和天上的窗户都闭塞了,天上的大雨也止住了。
3 Maji ya gharika yakaanza kuzama kidogo kidogo katika nchi. na mwisho wa siku miamoja na hamsini maji yakawa yamezama chini.
水从地上渐退。过了一百五十天,水就渐消。
4 safina ikatulia katika mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, juu ya milima ya Ararati.
七月十七日,方舟停在亚拉腊山上。
5 Maji yakaendelea kuzama chini hadi mwezi wa kumi. Siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana.
水又渐消,到十月初一日,山顶都现出来了。
6 Ikatokea kwamba baada ya siku arobaini Nuhu alifungua dirisha la safina ambayo aliitengeneza.
过了四十天,挪亚开了方舟的窗户,
7 Akatuma kunguru na akaruka hadi maji yalipo kauka katika nchi.
放出一只乌鸦去;那乌鸦飞来飞去,直到地上的水都干了。
8 Kisha akatuma njiwa kuona kama maji yamezama chini kutoka kwenye uso wa nchi,
他又放出一只鸽子去,要看看水从地上退了没有。
9 lakini njiwa hakuona sehemu ya kutua unyayo wake, na akarudi kwake ndani ya safina, kwa kuwa maji yalikuwa bado yamefunika nchi yote. Akanyoosha mkono wake, akamchukua na kumuweka ndani ya safina pamoja naye.
但遍地上都是水,鸽子找不着落脚之地,就回到方舟挪亚那里,挪亚伸手把鸽子接进方舟来。
10 Akasubiri siku saba zingine akatuma tena njiwa kutoka kwenye safina.
他又等了七天,再把鸽子从方舟放出去。
11 Njiwa akarudi kwake jioni. Tazama! katika mdomo wake kulikuwa na jani bichi la mzeituni lililochumwa. Kwa hiyo Nuhu akatambua kuwa maji yamekwisha zama chini ya nchi.
到了晚上,鸽子回到他那里,嘴里叼着一个新拧下来的橄榄叶子,挪亚就知道地上的水退了。
12 Akasubiri siku saba zingine na akamtuma njiwa tena. Njiwa hakurudi kwake tena.
他又等了七天,放出鸽子去,鸽子就不再回来了。
13 Ikawa kwamba katika mwaka wa mia sita na moja, katika mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikuwa yamekauka katika nchi. Nuhu akaondoa kifuniko cha safina, akatazama nje, na akaona kwamba, Tazama, uso wa nchi ulikuwa umekauka.
到挪亚六百零一岁,正月初一日,地上的水都干了。挪亚撤去方舟的盖观看,便见地面上干了。
14 Katika mwezi wa pili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, nchi ilikuwa imekauka.
到了二月二十七日,地就都干了。
15 Mungu akamwambia Nuhu,
神对挪亚说:
16 “Toka nje ya safina, wewe, mke wako, wanao wa kiume, na wake wa wanao pamoja nawe.
“你和你的妻子、儿子、儿妇都可以出方舟。
17 Wachukuwe utoke nje pamoja nao kila kiumbe hai chenye mwili ambacho kiko nawe - ndege, wanyama wa kufugwa, na kila kitambaacho ambacho hutambaa juu ya nchi - ili kwamba viweze kukua na kuwa na idadi kubwa zaidi ya viumbe hai katika nchi yote, kwa kuzaliana na kuongezeka juu ya nchi.”
在你那里凡有血肉的活物,就是飞鸟、牲畜,和一切爬在地上的昆虫,都要带出来,叫它在地上多多滋生,大大兴旺。”
18 Kwa hiyo Nuhu akatoka nje pamoja na watoto wake wa kiume, mke wake, na wake wa wa wanawe pamoja naye.
于是挪亚和他的妻子、儿子、儿妇都出来了。
19 Kila kiumbe hai, kila kitambaacho, na kila ndege, na kila kiendacho juu ya nchi, kwa kabila zao, wakaiacha safina.
一切走兽、昆虫、飞鸟,和地上所有的动物,各从其类,也都出了方舟。
20 Nuhu akajenga madhabahu kwa Yahwe. Akachukua baadhi ya wanyama walio safi na baadhi ya ndege walio safi, na kutoa sadaka ya kuteketezwa juu ya madhabahu.
挪亚为耶和华筑了一座坛,拿各类洁净的牲畜、飞鸟献在坛上为燔祭。
21 Yahwe akanusa harufu nzuri ya kuridhisha na akasema moyoni mwake, “Sita laani tena ardhi kwa sababu ya mwanadamu, ingawa nia za mioyo yao ni mbaya tokea utoto. Wala sita haribu kilakitu chenye uhai, kama nilivyo fanya.
耶和华闻那馨香之气,就心里说:“我不再因人的缘故咒诅地(人从小时心里怀着恶念),也不再按着我才行的灭各种的活物了。
22 Wakati nchi isaliapo, majira ya kupanda mbegu na mavuno, baridi na joto, kiangazi na majira ya baridi, mchana na usiku havitakoma.”
地还存留的时候,稼穑、寒暑、冬夏、昼夜就永不停息了。”
A Dove is Sent Forth from the Ark