< Mwanzo 17 >

1 Wakati Abram alipokuwa na umri wa miaka tisini na tisa, Yahwe alimtokea Abram na akamwambia, “Mimi ni Mungu wa uwezo. Uende mbele yangu, na uwe mkamilifu.
亚伯兰年九十九岁的时候,耶和华向他显现,对他说:“我是全能的 神。你当在我面前作完全人,
2 Kisha nitalithibitisha agano langu kati yangu mimi na wewe, na nitakuzidisha sana.
我就与你立约,使你的后裔极其繁多。”
3 Abram akainama uso wake hadi chini ardhini na Mungu akazungumza naye, akisema,
亚伯兰俯伏在地; 神又对他说:
4 “Mimi, tazama, agano langu liko nawe. Utakuwa baba wa mataifa mengi.
“我与你立约:你要作多国的父。
5 Wala jina lako halitakuwa tena Abram, bali jina lako litakuwa Abraham - kwa kuwa ninakuchagua kuwa baba wa mataifa mengi.
从此以后,你的名不再叫亚伯兰,要叫亚伯拉罕,因为我已立你作多国的父。
6 Nitakufanya uwe na uzao mwingi zaidi, na nitakufanya mataifa, na wafalme watatoka kwako.
我必使你的后裔极其繁多;国度从你而立,君王从你而出。
7 Nitaimarisha agao langu kati yangu mimi na wewe na uzao wako baada yako, katika vizazi vyao vyote kwa agano la milele, nitakuwa Mungu kwako na kwa wazao wako baada yako.
我要与你并你世世代代的后裔坚立我的约,作永远的约,是要作你和你后裔的 神。
8 Nitakupa wewe, na wazao wako baada yako, nchi ambayo ulikuwa unaishi, nchi yote ya Kanaani, kuwa miliki ya milele, na nitakuwa Mungu wao.”
我要将你现在寄居的地,就是迦南全地,赐给你和你的后裔永远为业,我也必作他们的 神。”
9 Kisha Mungu akamwambia Abraham, “nawe lazima ulishike agano langu, wewe pamoja na uzao wako baada yako kwa vizazi vyao.
神又对亚伯拉罕说:“你和你的后裔必世世代代遵守我的约。
10 Hili ndilo agano langu, ambalo utalishika, kati yangu na wewe na wazao wako baada yako: Kila mwanaume wa kwenu lazima atahiriwe.
你们所有的男子都要受割礼;这就是我与你并你的后裔所立的约,是你们所当遵守的。
11 Lazima mtatahiriwa katika nyama ya govi la ngozi ya mbele, na hii itakuwa ishara ya agano kati yangu mimi na ninyi.
你们都要受割礼;这是我与你们立约的证据。
12 Kila mwanaume wa kwenu aliye na umri wa siku nane lazima atahiriwe, katika vizazi ya watu wenu. Hii ni pamoja na yule azaliwaye katika nyumba yako na yeye ambaye amenunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni yeyote ambaye si mmoja wa wazao wako.
你们世世代代的男子,无论是家里生的,是在你后裔之外用银子从外人买的,生下来第八日,都要受割礼。
13 Mtu ambaye amezaliwa katika nyumba yako na yule aliye nunuliwa kwa fedha yako lazima atahiriwe. Hivyo agano langu litakuwa katika mwili wenu kuwa agano la milele.
你家里生的和你用银子买的,都必须受割礼。这样,我的约就立在你们肉体上作永远的约。
14 Mwanaume yeyote asiye tahiriwa katika mwili govi la ngozi yake ya mbele atatengwa na watu wake. Amevunja agano langu.”
但不受割礼的男子必从民中剪除,因他背了我的约。”
15 Mungu akamwambia Abraham, “kwa habari ya Sarai mkeo, usimuite tena Sarai. Badala yake jina lake litakuwa Sara.
神又对亚伯拉罕说:“你的妻子撒莱不可再叫撒莱,她的名要叫撒拉。
16 Nitambariki, na nitakupatia mtoto wa kiume kwake. Nitambariki, na atakuwa mama wa mataifa. Wafalme wa watu wa mataifa watapatikana kutokana na yeye.
我必赐福给她,也要使你从她得一个儿子。我要赐福给她,她也要作多国之母;必有百姓的君王从她而出。”
17 Kisha Abraham akainama uso wake hadi ardhini, na akacheka, akasema moyoni mwake, Je yawezekana mtoto azaliwe kwa mwanaume ambaye ana umri wa miaka miamoja? na Je Sara, ambaye ana umri wa miaka tisini anaweza kuzaa mwana?”
亚伯拉罕就俯伏在地喜笑,心里说:“一百岁的人还能得孩子吗?撒拉已经九十岁了,还能生养吗?”
18 Abraham akamwambia Mungu, “Lau Ishmaeli angeweza kuishi kabla yako!”
亚伯拉罕对 神说:“但愿以实玛利活在你面前。”
19 Mungu akasema, Hapana, Sarai mkeo atakuzalia mtoto wa kiume na utamwita jina lake Isaka. Nita imarisha agano langu na yeye kama agano la milele pamoja na uzao wake baada yake.
神说:“不然,你妻子撒拉要给你生一个儿子,你要给他起名叫以撒。我要与他坚定所立的约,作他后裔永远的约。
20 Na kwa habari ya Ishmaeli nimekusikia. Tazama, ninambariki, na nitamfanya kuwa na uzao na kumzidisha maradufu. Atakuwa baba wa viongozi kumi na mbili wa makabila, na nitamfanya kuwa taifa kuu.
至于以实玛利,我也应允你:我必赐福给他,使他昌盛,极其繁多。他必生十二个族长;我也要使他成为大国。
21 Lakini agano langu nitalifanya imara na Isaka, ambaye Sarai atazaa kwako majira haya mwakani.”
到明年这时节,撒拉必给你生以撒,我要与他坚定所立的约。”
22 Alipo kuwa amemaliza kuzungumza naye, Mungu akaondoka kwa Abraham.
神和亚伯拉罕说完了话,就离开他上升去了。
23 Kisha Abraham akamtwaa Ishmaeli mwanawe, na wote ambao walizaliwa katika nyumba yake, na wote ambao walinunuliwa kwa fedha yake, kila mwanaume miongoni mwa watu wa nyumba ya Abraham, walitahiriwa mwili wa magovi ya ngozi ya mbele katika siku iyo hiyo, kama Mungu alivyo kuwa amesema.
正当那日,亚伯拉罕遵着 神的命,给他的儿子以实玛利和家里的一切男子,无论是在家里生的,是用银子买的,都行了割礼。
24 Abraham alikuwa na umri wa miaka tisini na tisa alipotahiriwa katika mwili wa govi la ngozi yake ya mbele.
亚伯拉罕受割礼的时候年九十九岁。
25 Na Ishmaeli mwanawe alikuwa na umri wa miaka kumi na tatu alipotahiriwa katika mwili wa govi la ngozi yake ya mbele.
他儿子以实玛利受割礼的时候年十三岁。
26 Siku ile ile ambayo wote wawili Abraham na Ishmael mwanawe walipotahiriwa, ndipo
正当那日,亚伯拉罕和他儿子以实玛利一同受了割礼。
27 wanaume wote wa nyumba yake walitahiriwa pia, hawa ni pamoja na wale waliozaliwa katika nyumba ile na wale walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni.
家里所有的人,无论是在家里生的,是用银子从外人买的,也都一同受了割礼。

< Mwanzo 17 >