< Mwanzo 5 >
1 Hii ni orodha ya vizazi vya Adamu. Katika siku ambayo Mungu alimuumba mtu, aliwaumba katika mfano wake mwenyewe.
亞當的後代記在下面。(當上帝造人的日子,是照着自己的樣式造的,
2 Mwanaume na mwanamke aliwaumba. Akawabariki na akawaita Adam wakati walipoumbwa.
並且造男造女。在他們被造的日子,上帝賜福給他們,稱他們為「人」。)
3 Wakati Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, akamzaa mwana katika sura yake mwenyewe, kwa mfano wake, na akamuita jina lake Sethi.
亞當活到一百三十歲,生了一個兒子,形像樣式和自己相似,就給他起名叫塞特。
4 Baada ya Adamu kumzaa Sethi, aliishi miaka mia nane. Akawazaa wana wengi waume na wake.
亞當生塞特之後,又在世八百年,並且生兒養女。
5 Adamu akaishi miaka 930 kisha akafariki.
亞當共活了九百三十歲就死了。
6 Wakati Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi.
塞特活到一百零五歲,生了以挪士。
7 Baada ya kumzaa Enoshi, akaishi miaka 807 na akawazaa wana wengi waume na wake.
塞特生以挪士之後,又活了八百零七年,並且生兒養女。
8 Sethi akaishi miaka 912 kisha akafariki.
塞特共活了九百一十二歲就死了。
9 Wakati Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani.
以挪士活到九十歲,生了該南。
10 Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815. Akazaa wana wengi wa ume na wake.
以挪士生該南之後,又活了八百一十五年,並且生兒養女。
11 Enoshi aliishi miaka 905 na kisha akafariki.
以挪士共活了九百零五歲就死了。
12 Wakati Kanani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.
該南活到七十歲,生了瑪勒列。
13 Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840. Akawazaa wana wengi wa ume na wake.
該南生瑪勒列之後,又活了八百四十年,並且生兒養女。
14 Kenani aliishi miaka 910, na kisha akafariki.
該南共活了九百一十歲就死了。
15 Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, alimzaa Yaredi.
瑪勒列活到六十五歲,生了雅列。
16 Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830. Akazaa wana wengi wa ume na wake.
瑪勒列生雅列之後,又活了八百三十年,並且生兒養女。
17 Mahalaleli aliishi miaka 895 na kisha akafariki.
瑪勒列共活了八百九十五歲就死了。
18 Yaredi alipokuwa ameishi miaka 162, alimzaa Henoko.
雅列活到一百六十二歲,生了以諾。
19 Baada ya kumzaa Henoko, Yaredi aliishi miaka mianane. Akazaa wana wengi waume na wake.
雅列生以諾之後,又活了八百年,並且生兒養女。
20 Yaredi aliishi miaka 962 na kisha akafariki.
雅列共活了九百六十二歲就死了。
21 Henoko alipokuwa ameishi miaka sitini na tano, akamzaa Methusela.
以諾活到六十五歲,生了瑪土撒拉。
22 Henoko akaenenda na Mungu miaka miatatu baada ya kumzaa Methusela. Aliwazaa wana wengi wa ume na wake.
以諾生瑪土撒拉之後,與上帝同行三百年,並且生兒養女。
23 Henoko aliishi miaka 365.
以諾共活了三百六十五歲。
24 Henoko alienenda na Mungu, na kisha alitoweka, kwa kuwa Mungu alimtwaa.
以諾與上帝同行,上帝將他取去,他就不在世了。
25 Wakati Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, alimzaa Lameki.
瑪土撒拉活到一百八十七歲,生了拉麥。
26 Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782. Akawazaa wana wengi wa ume na wake.
瑪土撒拉生拉麥之後,又活了七百八十二年,並且生兒養女。
27 Methusela aliishi miaka 969. Kisha akafariki.
瑪土撒拉共活了九百六十九歲就死了。
28 Wakati Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana.
拉麥活到一百八十二歲,生了一個兒子,
29 Akamuita jina lake Nuhu, akisema, “Huyu ndiye atatupatia pumziko kutoka katika kazi yetu na kutoka katika kazi ya taabu ya mikono yetu, ambayo lazima tuifanye kwa sababu ya ardhi ambayo Yahwe ameilaani.”
給他起名叫挪亞,說:「這個兒子必為我們的操作和手中的勞苦安慰我們;這操作勞苦是因為耶和華咒詛地。」
30 Lameki aliishi miaka 595 baada ya kumzaa baba wa Nuhu. Akazaa wanawengi wa ume na wake.
拉麥生挪亞之後,又活了五百九十五年,並且生兒養女。
31 Lameki aliishi miaka 777. Kisha akafariki.
拉麥共活了七百七十七歲就死了。
32 Baada ya Nuhu kuishi miaka miatano, akamzaa Shemu, Hamu, na Yafethi.
挪亞五百歲生了閃、含、雅弗。