< Mwanzo 10 >

1 Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya wana wa Nuhu, ambao ni, Shemu, Hamu, na Yafethi. Wana wa kiume walizaliwa kwao baada ya gharika.
ואלה תולדת בני נח שם חם ויפת ויולדו להם בנים אחר המבול
2 Wana wa Yafethi walikuwa Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Masheki, na Tirasi.
בני יפת--גמר ומגוג ומדי ויון ותבל ומשך ותירס
3 Na wana wa Gomeri walikuwa Ashikenazi, Rifathi na Togama.
ובני גמר--אשכנז וריפת ותגרמה
4 Wana wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Dodanimu.
ובני יון אלישה ותרשיש כתים ודדנים
5 Kutoka kwa hawa watu wa pwani waligawanyika na kwenda kwenye ardhi zao, kila mtu na lugha yake, kufuatana na koo zao, kwa mataifa yao.
מאלה נפרדו איי הגוים בארצתם איש ללשנו--למשפחתם בגויהם
6 Wana wa Hamu walikuwa Kushi, Misraimu, Putu, na Kanaani.
ובני חם--כוש ומצרים ופוט וכנען
7 Wana wa Kushi walikuwa Seba, Havila, Sabta, Raama, na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa Sheba na Dedani.
ובני כוש--סבא וחוילה וסבתה ורעמה וסבתכא ובני רעמה שבא ודדן
8 Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikuwa hodari wa kwanza juu ya nchi.
וכוש ילד את נמרד הוא החל להיות גבר בארץ
9 Alikuwa mwindaji mkuu mbele ya Yahwe. Hii ndiyo sababu hunenwa, “Kama Nimrod mwindaji mkuu mbele za Yahwe.”
הוא היה גבר ציד לפני יהוה על כן יאמר כנמרד גבור ציד לפני יהוה
10 Miji ya kwanza ya ufalme wake ilikuwa Babeli, Ereku, Akadi na Kalne, katika ichi ya Shinari.
ותהי ראשית ממלכתו בבל וארך ואכד וכלנה בארץ שנער
11 Kutoka katika nchi ile alikwenda Ashuru na akajenga Ninawi, Rehoboth- iri na Kala,
מן הארץ ההוא יצא אשור ויבן את נינוה ואת רחבת עיר ואת כלח
12 na Raseni ambao ulikuwa kati ya Ninawi na Kala. Ulikuwa mji mkubwa.
ואת רסן בין נינוה ובין כלח--הוא העיר הגדלה
13 Misraimu akazaa Waludi, Waanami, Walehabi, na Wanaftuhi,
ומצרים ילד את לודים ואת ענמים ואת להבים--ואת נפתחים
14 Wapathrusi na Wakasluhi ( ambao kwao Wafilisti walitokea), na Wakaftori.
ואת פתרסים ואת כסלחים אשר יצאו משם פלשתים--ואת כפתרים
15 Kanaani akamzaa Sidono, mwanawe wa kwanza, na Hethi,
וכנען ילד את צידן בכרו--ואת חת
16 pia na Myebusi, na Mwamori, Mgirgashi,
ואת היבוסי ואת האמרי ואת הגרגשי
17 Mhivi, Mwarki, Msini,
ואת החוי ואת הערקי ואת הסיני
18 Mwarvadi, Msemari, na Mhamathi. Baadaye koo za wakanaani zikasambaa.
ואת הארודי ואת הצמרי ואת החמתי ואחר נפצו משפחות הכנעני
19 Mpaka wa Wakanaani ulianzia Sidoni, katika mwelekeo wa Gerari, hata Gaza, na kama kuelekea Sodoma, Gomora, Adma, na Seboimu hata Lasha.
ויהי גבול הכנעני מצידן--באכה גררה עד עזה באכה סדמה ועמרה ואדמה וצבים--עד לשע
20 Hawa walikuwa wana wa Ham, kwa koo zao, kwa lugha zao, katika ardhi zao na katika mataifa yao.
אלה בני חם למשפחתם ללשנתם בארצתם בגויהם
21 Pia walizaliwa wana kwa Shemu, ndugu yake mkubwa wa Yafethi. Shemu pia alikuwa baba yao na watu wote wa Eberi.
ולשם ילד גם הוא אבי כל בני עבר--אחי יפת הגדול
22 Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Alfaksadi, Ludi, na Aramu.
בני שם עילם ואשור וארפכשד ולוד וארם
23 Wana wa Aramu walikuwa ni Usi, Huli, Getheri, na Mashi.
ובני ארם--עוץ וחול וגתר ומש
24 Arfaksadi akamzaa Sela, na Sela akamzaa Eber.
וארפכשד ילד את שלח ושלח ילד את עבר
25 Eberi akazaa wana wawili wa kiume. Jina la mmoja aliitwa Pelegi maana katika siku zake nchi iligawanyika. Jina la ndugu yake aliitwa Yoktani.
ולעבר ילד שני בנים שם האחד פלג כי בימיו נפלגה הארץ ושם אחיו יקטן
26 Yoktani akamzaa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
ויקטן ילד את אלמודד ואת שלף ואת חצרמות ואת ירח
27 Hadoram, Uzali, Dikla,
ואת הדורם ואת אוזל ואת דקלה
28 Obali, Abimaeli, Sheba,
ואת עובל ואת אבימאל ואת שבא
29 Ofiri, Havila, na Yobabi. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.
ואת אופר ואת חוילה ואת יובב כל אלה בני יקטן
30 Mpaka wao ulikuwa unaanzia Mesha, hadi Sefari, mlima wa mashariki.
ויהי מושבם ממשא באכה ספרה הר הקדם
31 Hawa walikuwa wana wa Shemu, kulingana na koo zao na lugha zao, katika ardhi zao kulingana na mataifa yao.
אלה בני שם למשפחתם ללשנתם בארצתם לגויהם
32 Hizi zilikuwa koo za wana wa Nuhu, kulingana na vizazi vyao, kwa mataifa yao. Kutokea kwa hawa mataifa yaligawanyika na kwenda juu ya nchi baada ya gharika.
אלה משפחת בני נח לתולדתם בגויהם ומאלה נפרדו הגוים בארץ--אחר המבול

< Mwanzo 10 >