< Kutoka 34 >
1 Yahweh akamwabia Musa, “Kata mbao mbili za mawe kama zile za awali. Nitaandika kwenye hizi mbao za mawe maneno yaliyo kuwa kwenye mbao za mawe za mwanzo, mbao za mawe ulizo zivunja.
Bwana akamwambia Mose, “Chonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza, nami nitaandika juu yake maneno yale yaliyokuwa kwenye vile vibao vya kwanza, ulivyovivunja.
2 Kuwa tayari asubui na uje Mlima Sinai, na uje mbele zangu juu ya mlima.
Uwe tayari asubuhi, kisha upande juu ya Mlima Sinai. Uje mbele zangu kukutana nami huko juu ya mlima.
3 Hakuna atakaye kuja nawe. Usiruhusu mtu yeyote aonekana popote kwenye mlima. Hakuna kundi la mifugo wanao ruhusiwa ata kula mbele ya mlima.”
Mtu yeyote asije pamoja nawe, wala asionekane mtu popote juu ya mlima, wala kondoo na mbuzi au ngʼombe wasilishe karibu mbele ya huo mlima.”
4 Hivyo Musa akakata mbao mbili za mawe kama za mwanzo, na akaamka asubui mapema na kwenda juu ya Mlima Sinai, kama Yahweh alivyo muelekeza. Musa alibeba mbao za mawe mikononi mwake.
Kwa hiyo Mose akachonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza, naye akapanda juu ya Mlima Sinai asubuhi na mapema, kama Bwana alivyokuwa amemwagiza, akachukua vile vibao viwili vya mawe mikononi mwake.
5 Yahweh akaja chini katika wingu na akasima mbele za Musa, na akatamka jina “Yahweh.”
Kisha Bwana akashuka katika wingu akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina lake, Bwana.
6 Yahweh akapita kwake na kukiri, “Yahweh, Yahweh, Mungu ni wa rehema na wa neema, sio mwepesi wa hasira, na anadumu katika uwaminifu wa agano na uadilifu,
Bwana akapita mbele ya Mose, akitangaza, “Bwana, Bwana, Mungu mwenye huruma na neema, asiye mwepesi wa hasira, mwingi wa upendo na uaminifu,
7 ukishika uaminifu wa agano kwa vizazi maelfu, ukisamehe maasi, makosa, na dhambi. Lakini hamsafishi mwenye hatia. Ataleta adhabu ya dhambi za baba kwa watoto wao na watoto wa watoto wao, kwa kizazi cha tatu na hadi cha nne.”
akidumisha upendo kwa maelfu, pia akisamehe uovu, uasi na dhambi. Lakini haachi kuadhibu mwenye hatia; huwaadhibu watoto na watoto wao kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata katika kizazi cha tatu na cha nne.”
8 Musa haraka akainamisha kichwa chake kwenye ardhi na kuabudu.
Mara Mose akasujudu na kuabudu.
9 Kisha akasema, “Kama sasa nimepata upendeleo machoni pako, Bwana wangu, tafadhali nenda pamoja nasi, kwa kuwa hawa watu ni wa korofi. Samehe maasi yetu na dhambi zetu, na utuchukuwe kama urithi wako.”
Mose akasema, “Ee Bwana, kama nimepata kibali mbele zako, basi Bwana uende pamoja nasi. Ingawa watu hawa ni wenye shingo ngumu, samehe uovu wetu na dhambi yetu, tuchukue kuwa urithi wako.”
10 Yahweh akasema, “Ona, ninakaribu kufanya agano. Mbele za watu wako, nitafanya maajabu ambayo hayajawai kufanywa duniani kote wala kwenye taifa lote. Watu wote miongoni mwako wataona matendo yangu, kwa kuwa ni kitu cha hofu ninacho fanya kwako.
Kisha Bwana akasema: “Tazama ninafanya Agano mbele ya watu wako wote. Mbele ya watu wako wote nitafanya maajabu ambayo hayajafanyika katika taifa lolote katika ulimwengu wote. Watu wale mnaoishi miongoni mwao wataona jinsi ilivyo ya kushangaza ile kazi nitakayowafanyia mimi Bwana wenu.
11 Tii amri zangu leo. Ninawaondoa mbele yako Waamori, Wakanani, Wahivi, Wahiti, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi.
Tii yale ninayokuamuru leo. Tazama nawafukuza mbele yako Waamori, Wakanaani, Wahiti, Waperizi, Wahivi na Wayebusi.
12 Kuwa mwanglifu usifanye agano na wakazi wa nchi unayo kwenda, au wata kuwa mtego kwako.
Uwe mwangalifu, usifanye agano na wale wanaokaa katika nchi ile unayoiendea, la sivyo watakuwa mtego katikati yako.
13 Badala yake, lazima uvunje madhabahu zao, ponda nguzo zao za mawe, na kukata nguzo zao za Ashera.
Bomoa madhabahu yao, vunja mawe yao ya kuabudia na ukatekate nguzo zao za Ashera.
14 Kwa kuwa wewe haupaswi kumuabudu mungu mwingine, maana Yahweh, ambaye jina lake ni Uwivu, ni Mungu wa uwivu.
Usiabudu mungu mwingine, kwa kuwa Bwana, ambaye jina lake ni Wivu, ni Mungu mwenye wivu.
15 Hivyo kuwa mwangalifu usifanye agano na wakazi wa nchi, kwa kuwa wanajifanyia ukahaba kwa miungu yao, na wanatoa dhabihu kwa miungu yao. Kisha mmoja wao ata kukaribisha na wewe utakula baadhi ya dhabihu zake,
“Uwe mwangalifu usifanye agano na wale watu wanaoishi katika nchi, kwa maana wakati wanapojifanyia ukahaba kwa miungu yao na kuwatolea kafara, watakualika wewe nawe utakula sadaka za matambiko yao.
16 na kisha utachukuwa baadhi ya mabinti zake kwa wanao, na mabinti wake watafanya ukahaba kwa miungu yao, na watafanya wanao kufanya ukahaba kwa miungu yao.
Unapowachagua baadhi ya binti zao kuwa wake wa wana wenu na binti hao wakajifanyia ukahaba kwa miungu yao, watawaongoza wana wenu kufanya vivyo hivyo.
17 Usifanye Miungu ya chuma ya kuyayusha.
“Usijifanyie sanamu za kusubu.
18 Laziam ushike Sherehe ya Mkate Usiotiwachachu. Kama nilivyo kuamuru, lazima ule mkate usio na hamira kwa siku saba kwa muda uliotengwa wa mwezi wa Abibu, maana nikatika mwezi wa Abibu ulitoka Misri.
“Utaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu, kama nilivyokuamuru. Fanya hivi kwa wakati ulioamriwa, katika mwezi wa Abibu, ndio mwezi wa nne, kwa kuwa katika mwezi huo ndipo wewe ulipotoka Misri.
19 Wazaliwa wote ni mwangu, ata mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mifugo, yote ya ng'ombe na kondoo.
“Mzaliwa wa kwanza wa kila tumbo ni mali yangu, pamoja na wazaliwa wa kwanza wote wa kiume wa mifugo yako, ikiwa ni wa ngʼombe au wa kondoo au mbuzi.
20 Lazima umnunue tena mzaliwa kwanza wa punda kwa kondoo, lakini usipo mnunua tena, kisha uivunje shingo yake. Lazima ununue tena wazaliwa wa kwanza wote wa wanao. Hakuna ata mmoja atakye kuja kwangu mikono mitupu.
Utakomboa mzaliwa wa kwanza wa punda kwa mwana-kondoo, lakini kama humkomboi, utavunja shingo yake. Utakomboa wazaliwa wako wa kwanza wote wa kiume. “Mtu yeyote asije mbele zangu mikono mitupu.
21 Utafanya kazi kwa siku sita, lakini siku ya saba utapumzika. Ata wakati wakilimo na wa mavuno, lazima upumzike.
“Kwa siku sita utafanya kazi, lakini siku ya saba utapumzika, hata ikiwa ni majira ya kulima au ya kuvuna lazima upumzike.
22 Lazima uadhimishe Sherehe ya Majuma kwa mazao ya kwanza ya mavuno ya ngano, na lazima uadhimishe Sherehe ya Makusanyo mwisho wa mwaka.
“Utaadhimisha Sikukuu ya Majuma kwa malimbuko ya mavuno ya ngano, na Sikukuu ya Mavuno mwishoni mwa mwaka.
23 Mara tatu kwa mwaka wanaume wenu wote watajitokeza kwa Bwana Yahweh, Mungu wa Israeli.
Mara tatu kwa mwaka wanaume wako wote watakuja mbele za Bwana Mwenyezi, Mungu wa Israeli.
24 Kwa kuwa nitaondoa mataifa mbele yenu na kutanua mipika. Hakuna atakaye tamani kuwa na ardhi yenu kama yao utakapo toka mbele za Yahweh mara tatu kwa mwaka.
Nitawafukuza mataifa mbele yako na kupanua mipaka ya nchi yako, wala hakuna mtu yeyote atakayeitamani nchi yako wakati unapokwenda mara tatu kila mwaka kuonana na Bwana Mungu wako.
25 Hautatoa damu ya dhabihu yangu na hamira yeyote, wala nyama yeyote kutoka dhabihu za Sherehe ya Pasaka kubaki hadi asubui.
“Usinitolee damu ya dhabihu pamoja na kitu chochote chenye chachu, wala usibakize dhabihu yoyote ya Sikukuu ya Pasaka mpaka asubuhi.
26 Lazima ulete matunda ya kwanza yalio bora kutoka nyumbani kwako. Usimchemshe mbuzi mtoto katika maziwa ya mama yake.”
“Leta matunda ya kwanza yaliyo bora zaidi ya ardhi yako katika nyumba ya Bwana Mungu wako. “Usimchemshe mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.”
27 Yahweh akamwabia Musa, “Andika chini haya maneno, kwa kuwa nimejiahidi haya maneno niliyo yasema, na nimefanya agano kwako na Israeli.”
Kisha Bwana akamwambia Mose, “Andika maneno haya, kwa maana kulingana na maneno haya, nimefanya Agano na wewe pamoja na Israeli.”
28 Musa alikuwa huko na Yahweh kwa siku arobaini na usiku; hakula chakula chochote wala kunywa maji yeyote. Aliandika katika mbao maneno ya agano, Amri kumi.
Mose alikuwa huko pamoja na Bwana kwa siku arobaini usiku na mchana bila kula chakula wala kunywa maji. Naye akaandika juu ya vibao maneno ya Agano, yaani zile Amri Kumi.
29 Musa alipo shuka chini ya Mlima Sinai na mbao mbili za agano za ushuhuda mikononi mwake, hakujua kuwa ngozi ya kuwa uso wake ulikuwa wa'ngaa akizungumza na Mungu.
Mose alipoteremka kutoka Mlima Sinai akiwa na vile vibao viwili vya Ushuhuda mikononi mwake, hakujua kuwa uso wake ulikuwa ukingʼaa, kwa sababu alikuwa amezungumza na Bwana.
30 Wakati Aruni na Waisraeli walipo muona Musa, ngozi ya uso wake ulikuwa wa ng'aa, na waliogopa kuja karibu yake.
Aroni na Waisraeli wote walipomwona Mose, kuwa uso wake unangʼaa, waliogopa kumkaribia.
31 Lakini Musa aliwaita, na Aruni na viongozi wa jamii wakaja kwake. Kisha Musa akasema nao.
Lakini Mose akawaita, kwa hiyo Aroni na viongozi wote wa jumuiya wakarudi, naye akazungumza nao.
32 Baada ya haya, watu wote wa Israeli wakaja kwa Musa, na akawambia amri zote Yahweh alizo mpa katika Mlima Sinai.
Baadaye Waisraeli wote wakamkaribia, naye akawapa amri zote Bwana alizompa katika Mlima wa Sinai.
33 Musa alipo maliza kuzungumza nao, alifunika uso wake kwa kitambaa.
Mose alipomaliza kuzungumza nao, akaweka utaji kwenye uso wake.
34 Wakati Musa alipoenda mbele za Yahweh kusema naye, aliondoa kitambaa, hadi alipo toka. Alipo toka, aliwaambia Waisraeli alicho amriwa kusema.
Lakini kila wakati Mose alipoingia mbele za Bwana kuzungumza naye, aliondoa ule utaji mpaka alipotoka nje. Naye alipotoka nje na kuwaambia Waisraeli lile ambalo ameagizwa,
35 Waisraeli walipo muona Musa ana'ngaa uso, alirudisha kitambaa tena usoni mpaka alipokuwa anaenda kuongea na Yahweh.
waliona kuwa uso wake unangʼaa. Kisha Mose angeliweka tena utaji juu ya uso wake mpaka alipokwenda kuzungumza na Bwana.