< Wimbo wa Sulemani 1 >

1 Wimbo ulio bora wa Solomoni.
Wimbo ulio Bora, ambao ni wa Sulemani. Wanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake
2 Unibusu kwa busu la kinywa chako, kwa maana upendo wako unafurahisha kuliko divai.
O, laiti ungenibusu na mabasu ya mdomo wako, kwa kuwa upendo wako ni bora kuliko mvinyo.
3 Manukato yako yananukia vizuri, jina lako ni kama manukato yaliyomiminwa. Ndiyo sababu wanawali wanakupenda!
Mafuta yako ya upako yana manukato mazuri; jina lako ni kama marashi yaeleayo, hivyo wanawake wadogo wanakupenda.
4 Nichukue twende nawe, na tufanye haraka! Mfalme na anilete ndani ya vyumba vyake. Marafiki Tunakushangilia na kukufurahia, tutasifu upendo wako zaidi kuliko divai. Mpendwa Tazama jinsi ilivyo bora wakupende!
Nichukuwe kwako, na tutakimbia. Mwanamke akizungumza mwenyewe Mfalme amenipeleka vyumbani mwake. Mwanamke akizungumza na mpenzi wake nina furuha; nina furahi kuhusu wewe; acha ni shereheke upendo wako; ni bora kuliko mvinyo. Ni halisi kwa wanawake wengine kupenda. Mwanamke akizungumza na wanawake wengine.
5 Mimi ni mweusi, lakini napendeza, enyi binti za Yerusalemu, mweusi kama mahema ya Kedari, kama mapazia ya hema la Solomoni.
Mimi ni mweusi lakini mzuri, enyi mabinti wa wanaume wa Yerusalemu - mweusi kama hema za Kedari, muzuri kama mapazia ya Sulemani.
6 Usinikazie macho kwa sababu mimi ni mweusi, kwa sababu nimefanywa mweusi na jua. Wana wa mama yangu walinikasirikia na kunifanya niwe mtunza mashamba ya mizabibu. Shamba langu mwenyewe la mizabibu nimeliacha.
Usinishangae kwasababu ni mweusi, kwasababu jua limeniunguza. Wana wa mama yangu walikuwa na hasira juu yangu; walinifanya mtunzi wa mashamba ya mizabibu, lakini mshamba langu la mizabibu sijatunza. Wanamke akizungumza na mpenzi wake.
7 Niambie, wewe ambaye ninakupenda, unalisha wapi kundi lako la kondoo na ni wapi unapowapumzisha kondoo wako adhuhuri. Kwa nini niwe kama mwanamke aliyefunikwa shela karibu na makundi ya rafiki zako?
Niambie, wewe ninaye kupenda, wapi unalisha mifugo yako? Wapi unapumzisha mifugo yako mchana? Kwa nini niwe kama mtu anaye akangaika miongoni mwa mifugo ya marafiki zako? Mpenzi wake anamjibu
8 Kama hujui, ewe mwanamke mzuri kuliko wote, fuata nyayo za kondoo, na kulisha wana-mbuzi wako karibu na hema za wachungaji.
Kama haujui, uliye mzuri miongoni mwa wanawake, fuata nyayo za mifugo yangu, na ulishe watoto wako wa mbuzi karibu na hema za wachungaji.
9 Mpenzi wangu, ninakufananisha na farasi jike aliyefungwa katika mojawapo ya magari ya vita ya Farao.
Nina kulinganisha, mpenzi wangu, na farasi mzuri wakike miongoni mwa farasi wa magari ya Farao.
10 Mashavu yako yanapendeza yakiwa na vipuli, shingo yako ikiwa na mikufu ya vito.
Mashavu yako ni mazuri na mapambo, shingo yako na mikufu ya madini.
11 Tutakufanyia vipuli vya dhahabu, vyenye kupambwa kwa fedha.
Nitakufanyia mapambo ya dhahabu yaliochanganywa na fedha. Mwanamke akiongea mwenyewe.
12 Wakati mfalme alipokuwa mezani pake, manukato yangu yalisambaza harufu yake nzuri.
Wakati mfalme akiwa amelala kitandani mwake, marashi yangu yakasambaza arufu.
13 Mpenzi wangu kwangu mimi ni kifuko cha manemane kati ya matiti yangu.
Mpenzi wangu ni kwangu kama mkebe wa marashi unao lala usiku katika ya maziwa yangu.
14 Mpenzi wangu kwangu mimi ni kama kishada cha maua ya mhina kutoka mashamba ya mizabibu ya En-Gedi.
Mpenzi wangu ni kwangu kama kifurushi cha maua ya hena katika mashamba ya mizabibu ya Eni Gedi. Mpenzi wake anazungumza naye
15 Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu! Tazama jinsi ulivyo mzuri! Macho yako ni kama ya hua.
Ona, wewe ni mzuri, mpenzi wangu; ona, wewe ni mzuri; macho yako ni kama ya hua. Mwanamke anazungumza na mpenzi wake.
16 Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu! Ee, tazama jinsi unavyopendeza! Na kitanda chetu ni cha majani mazuri.
Ona, wewe ni mtanashati, mpenzi wangu, jinsi mtanashati.
17 Nguzo za nyumba yetu ni mierezi, na mapao yetu ni miberoshi.
Nguzo za nyumba yetu ni za matawi ya mierezi, na dari letu ni la matawi ya miberoshi.

< Wimbo wa Sulemani 1 >