< Zaburi 7 >

1 Ombolezo la Daudi kwa Bwana kwa sababu ya Kushi, Mbenyamini. Ee Bwana, Mungu wangu, ninakukimbilia wewe, uniokoe na kunikomboa na wote wanaonifuatia,
שגיון לדוד אשר שר ליהוה על דברי כוש בן ימיני יהוה אלהי בך חסיתי הושיעני מכל רדפי והצילני׃
2 la sivyo watanirarua kama simba na kunichana vipande vipande, asiwepo wa kuniokoa.
פן יטרף כאריה נפשי פרק ואין מציל׃
3 Ee Bwana, Mungu wangu, kama nimetenda haya na kuna hatia mikononi mwangu,
יהוה אלהי אם עשיתי זאת אם יש עול בכפי׃
4 au ikiwa nimemtenda uovu aliye na amani nami, au nimemnyangʼanya adui yangu pasipo sababu,
אם גמלתי שולמי רע ואחלצה צוררי ריקם׃
5 basi adui anifuatie na kunipata, auponde uhai wangu ardhini na kunilaza mavumbini.
ירדף אויב נפשי וישג וירמס לארץ חיי וכבודי לעפר ישכן סלה׃
6 Amka kwa hasira yako, Ee Bwana, inuka dhidi ya ghadhabu ya adui zangu. Amka, Mungu wangu, uamue haki.
קומה יהוה באפך הנשא בעברות צוררי ועורה אלי משפט צוית׃
7 Kusanyiko la watu na likuzunguke. Watawale kutoka juu.
ועדת לאמים תסובבך ועליה למרום שובה׃
8 Bwana na awahukumu kabila za watu. Nihukumu Ee Bwana, kwa kadiri ya haki yangu, kwa kadiri ya uadilifu wangu, Ewe Uliye Juu Sana.
יהוה ידין עמים שפטני יהוה כצדקי וכתמי עלי׃
9 Ee Mungu mwenye haki, uchunguzaye mawazo na mioyo, komesha ghasia za waovu na ufanye wenye haki waishi kwa amani.
יגמר נא רע רשעים ותכונן צדיק ובחן לבות וכליות אלהים צדיק׃
10 Ngao langu ni Mungu Aliye Juu Sana, awaokoaye wanyofu wa moyo.
מגני על אלהים מושיע ישרי לב׃
11 Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Mungu aghadhibikaye kila siku.
אלהים שופט צדיק ואל זעם בכל יום׃
12 Kama hakutuhurumia, atanoa upanga wake, ataupinda na kuufunga uzi upinde wake.
אם לא ישוב חרבו ילטוש קשתו דרך ויכוננה׃
13 Ameandaa silaha zake kali, ameweka tayari mishale yake ya moto.
ולו הכין כלי מות חציו לדלקים יפעל׃
14 Yeye aliye na mimba ya uovu na achukuaye mimba ya ghasia huzaa uongo.
הנה יחבל און והרה עמל וילד שקר׃
15 Yeye achimbaye shimo na kulifukua hutumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe.
בור כרה ויחפרהו ויפל בשחת יפעל׃
16 Ghasia azianzishazo humrudia mwenyewe, ukatili wake humrudia kichwani.
ישוב עמלו בראשו ועל קדקדו חמסו ירד׃
17 Nitamshukuru Bwana kwa ajili ya haki yake, na nitaliimbia sifa jina la Bwana Aliye Juu Sana.
אודה יהוה כצדקו ואזמרה שם יהוה עליון׃

< Zaburi 7 >