Preface
Read
+
Publisher
Nainoia, Inc.
PO Box 462, Bellefonte, PA 16823
(814) 470-8028
Nainoia Inc, Publisher
LinkedIn/NAINOIA-INC
Third Party Publisher Resources
Request Custom Formatted Verses
Please contact us below
Submit your proposed corrections
I understand that the Aionian Bible republishes public domain and Creative Commons Bible texts and that volunteers may be needed to present the original text accurately. I also understand that apocryphal text is removed and most variant verse numbering is mapped to the English standard. I have entered my corrections under the verse(s) below. Proposed corrections to the Swahili Contemporary Version, Psalms Chapter 7 https://www.AionianBible.org/Bibles/Swahili---Contemporary/Psalms/7 1) Ombolezo la Daudi kwa Bwana kwa sababu ya Kushi, Mbenyamini. Ee Bwana, Mungu wangu, ninakukimbilia wewe, uniokoe na kunikomboa na wote wanaonifuatia, 2) la sivyo watanirarua kama simba na kunichana vipande vipande, asiwepo wa kuniokoa. 3) Ee Bwana, Mungu wangu, kama nimetenda haya na kuna hatia mikononi mwangu, 4) au ikiwa nimemtenda uovu aliye na amani nami, au nimemnyangʼanya adui yangu pasipo sababu, 5) basi adui anifuatie na kunipata, auponde uhai wangu ardhini na kunilaza mavumbini. 6) Amka kwa hasira yako, Ee Bwana, inuka dhidi ya ghadhabu ya adui zangu. Amka, Mungu wangu, uamue haki. 7) Kusanyiko la watu na likuzunguke. Watawale kutoka juu. 8) Bwana na awahukumu kabila za watu. Nihukumu Ee Bwana, kwa kadiri ya haki yangu, kwa kadiri ya uadilifu wangu, Ewe Uliye Juu Sana. 9) Ee Mungu mwenye haki, uchunguzaye mawazo na mioyo, komesha ghasia za waovu na ufanye wenye haki waishi kwa amani. 10) Ngao langu ni Mungu Aliye Juu Sana, awaokoaye wanyofu wa moyo. 11) Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Mungu aghadhibikaye kila siku. 12) Kama hakutuhurumia, atanoa upanga wake, ataupinda na kuufunga uzi upinde wake. 13) Ameandaa silaha zake kali, ameweka tayari mishale yake ya moto. 14) Yeye aliye na mimba ya uovu na achukuaye mimba ya ghasia huzaa uongo. 15) Yeye achimbaye shimo na kulifukua hutumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe. 16) Ghasia azianzishazo humrudia mwenyewe, ukatili wake humrudia kichwani. 17) Nitamshukuru Bwana kwa ajili ya haki yake, na nitaliimbia sifa jina la Bwana Aliye Juu Sana. Additional comments?
Refresh Captcha
The world's first Holy Bible un-translation!