< Zaburi 49 >

1 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. Sikieni haya, enyi mataifa yote, sikilizeni, ninyi wote mkaao dunia hii.
Sikieni hili, ninyi watu wote; tegeni masikio, ninyi wenyeji wa dunia,
2 Wakubwa kwa wadogo, matajiri na maskini pamoja:
wote walio chini na walio juu, tajiri na masikini wote pamoja.
3 Kinywa changu kitasema maneno ya hekima, usemi wa moyo wangu utatoa ufahamu.
Mdomo wangu utazungumza hekima na tafakari ya moyo wangu itakuwa ya uelewa.
4 Nitatega sikio langu nisikilize mithali, nitafafanua kitendawili kwa zeze:
Nitaelekeza sikio langu kwenye mfano; nitaanza mfano wangu kwa kinubi.
5 Kwa nini niogope siku mbaya zinapokuja, wakati wadanganyifu waovu wanaponizunguka,
Kwa nini nilazimike kuziogopa siku za uovu, wakati uovu umenizunguka kwenye visigino vyangu?
6 wale wanaotegemea mali zao na kujivunia utajiri wao mwingi?
Kwa nini niwaogope wale wanao amini katika mali zao na kujivuna kuhusu utajiri wao?
7 Hakuna mwanadamu awaye yote awezaye kuukomboa uhai wa mwingine, au kumpa Mungu fidia kwa ajili yake.
Ni hakika kuwa hakuna yeyote atakaye muokoa ndugu yake au kumpa Mungu pesa kwa ajili yake,
8 Fidia ya uhai ni gharama kubwa, hakuna malipo yoyote yanayotosha,
Kwa maana ukombozi wa uhai wa mtu ni gharama kubwa, na hakuna awezaye kulipa kile tunacho daiwa.
9 ili kwamba aishi milele na asione uharibifu.
Hakuna yeyote atakaye ishi milele ili mwili wake usioze.
10 Wote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa; wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia na kuwaachia wengine mali zao.
Maana yeye ataona uozo. Watu wenye hekima hufa; wajinga pia huangamia na kuacha mali zao kwa wengine.
11 Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele, makao yao vizazi vyote; ingawa walikuwa na mashamba na kuyaita kwa majina yao.
Mawazo yao ya ndani ni kuwa familia zao zitaishi milele, na mahali waishipo, kwa vizazi vyote; wanaita ardhi zao kwa majina yao wenyewe.
12 Lakini mwanadamu, licha ya utajiri wake, hadumu; anafanana na mnyama aangamiaye.
Lakini mtu, kuwa na mali, haimaanishi atabaki hai; kama wanyama walioangamia.
13 Hii ndiyo hatima ya wale wanaojitumainia wenyewe, pia ya wafuasi wao, waliothibitisha misemo yao.
Hii ni hatma ya wafanyao ujinga baada ya kufa, .................
14 Kama kondoo, wamewekewa kwenda kaburini, nacho kifo kitawala. Wanyofu watawatawala asubuhi, maumbile yao yataozea kaburini, mbali na majumba yao makubwa ya fahari. (Sheol h7585)
Kama kondoo wamechaguliwa kwa ajili ya kuzimu na kifo kitakuwa mchungaji wao. Nao watatawaliwa na wenye haki ifikapo asubuhi, na miili yao italiwa kuzimuni, wakiwa hawana afasi ya kuishi kwa ajili yao. (Sheol h7585)
15 Lakini Mungu atakomboa uhai wangu na kaburi, hakika atanichukua kwake. (Sheol h7585)
Bali Mungu ataufufua uhai wangu kutoka katika nguvu ya kuzimu; naye atanipokea. (Selah) (Sheol h7585)
16 Usitishwe mtu anapotajirika, fahari ya nyumba yake inapoongezeka,
Msifadhaike mtu awapo tajiri, utukufu wa nyumba yake uongezekapo.
17 kwa maana hatachukua chochote atakapokufa, fahari yake haitashuka pamoja naye.
Maana atakapo kufa hataondoka na chochote; utukufu wake hautamfuata yeye.
18 Ingawa alipokuwa akiishi alijihesabu kuwa heri, na wanadamu wanakusifu unapofanikiwa,
Yeye huifurahisha nafsi yake awapo hai na watu hukusifu wewe uishipo maisha yako mwenyewe-
19 atajiunga na kizazi cha baba zake, ambao hawataona kamwe nuru ya uzima.
naye atakwenda kwenye ukoo wa baba zake naye kamwe hataiona nuru tena.
20 Mwanadamu mwenye utajiri bila ufahamu ni kama wanyama waangamiao.
Yule ambaye ana mali lakini hana ufahamu ni kama wanyama, ambao wataangamia.

< Zaburi 49 >