< Zaburi 49 >
1 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. Sikieni haya, enyi mataifa yote, sikilizeni, ninyi wote mkaao dunia hii.
可拉后裔的诗,交与伶长。 万民哪,你们都当听这话! 世上一切的居民,
2 Wakubwa kwa wadogo, matajiri na maskini pamoja:
无论上流下流,富足贫穷, 都当留心听!
3 Kinywa changu kitasema maneno ya hekima, usemi wa moyo wangu utatoa ufahamu.
我口要说智慧的言语; 我心要想通达的道理。
4 Nitatega sikio langu nisikilize mithali, nitafafanua kitendawili kwa zeze:
我要侧耳听比喻, 用琴解谜语。
5 Kwa nini niogope siku mbaya zinapokuja, wakati wadanganyifu waovu wanaponizunguka,
在患难的日子,奸恶随我脚跟,四面环绕我, 我何必惧怕?
6 wale wanaotegemea mali zao na kujivunia utajiri wao mwingi?
那些倚仗财货自夸钱财多的人,
7 Hakuna mwanadamu awaye yote awezaye kuukomboa uhai wa mwingine, au kumpa Mungu fidia kwa ajili yake.
一个也无法赎自己的弟兄, 也不能替他将赎价给 神,
8 Fidia ya uhai ni gharama kubwa, hakuna malipo yoyote yanayotosha,
叫他长远活着,不见朽坏; 因为赎他生命的价值极贵, 只可永远罢休。
9 ili kwamba aishi milele na asione uharibifu.
10 Wote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa; wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia na kuwaachia wengine mali zao.
他必见智慧人死, 又见愚顽人和畜类人一同灭亡, 将他们的财货留给别人。
11 Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele, makao yao vizazi vyote; ingawa walikuwa na mashamba na kuyaita kwa majina yao.
他们心里思想: 他们的家室必永存, 住宅必留到万代; 他们以自己的名称自己的地。
12 Lakini mwanadamu, licha ya utajiri wake, hadumu; anafanana na mnyama aangamiaye.
但人居尊贵中不能长久, 如同死亡的畜类一样。
13 Hii ndiyo hatima ya wale wanaojitumainia wenyewe, pia ya wafuasi wao, waliothibitisha misemo yao.
他们行的这道本为自己的愚昧; 但他们以后的人还佩服他们的话语。 (细拉)
14 Kama kondoo, wamewekewa kwenda kaburini, nacho kifo kitawala. Wanyofu watawatawala asubuhi, maumbile yao yataozea kaburini, mbali na majumba yao makubwa ya fahari. (Sheol )
他们如同羊群派定下阴间; 死亡必作他们的牧者。 到了早晨,正直人必管辖他们; 他们的美容必被阴间所灭,以致无处可存。 (Sheol )
15 Lakini Mungu atakomboa uhai wangu na kaburi, hakika atanichukua kwake. (Sheol )
只是 神必救赎我的灵魂脱离阴间的权柄, 因他必收纳我。 (细拉) (Sheol )
16 Usitishwe mtu anapotajirika, fahari ya nyumba yake inapoongezeka,
见人发财、家室增荣的时候, 你不要惧怕;
17 kwa maana hatachukua chochote atakapokufa, fahari yake haitashuka pamoja naye.
因为,他死的时候什么也不能带去; 他的荣耀不能随他下去。
18 Ingawa alipokuwa akiishi alijihesabu kuwa heri, na wanadamu wanakusifu unapofanikiwa,
他活着的时候,虽然自夸为有福 (你若利己,人必夸奖你);
19 atajiunga na kizazi cha baba zake, ambao hawataona kamwe nuru ya uzima.
他仍必归到他历代的祖宗那里, 永不见光。
20 Mwanadamu mwenye utajiri bila ufahamu ni kama wanyama waangamiao.
人在尊贵中而不醒悟, 就如死亡的畜类一样。