< Zaburi 44 >

1 Kwa mwimbishaji. Utenzi wa wana wa Kora. Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu, baba zetu wametueleza yale uliyotenda katika siku zao, siku za kale.
Mungu, tumesikia kwa masikio yetu, baba zetu wametuambia kazi uliyofanya katika siku zao, siku za kale.
2 Kwa mkono wako uliwafukuza mataifa na ukawapanda baba zetu, uliangamiza mataifa na kuwastawisha baba zetu.
Uliwafukuza mataifa kwa mkono wako, lakini ukawafanya watu wetu kuishi humo; wewe uliwataabisha mataifa, lakini ukawaeneza watu wetu katika nchi.
3 Sio kwa upanga wao waliipata nchi, wala si mkono wao uliwapatia ushindi; ilikuwa ni kitanga cha mkono wako wa kuume, na nuru ya uso wako, kwa kuwa uliwapenda.
Kwa maana hawakupata umiliki wa nchi kwa upanga wao, wala mkono wao wenyewe haukuwaokoa; bali mkono wako wakuume, mkono wako, na nuru ya uso wako, na kwa sababu uliwaridhia.
4 Wewe ni mfalme wangu na Mungu wangu, unayeamuru ushindi kwa Yakobo.
Mungu, wewe ni Mfalme wangu, amuru ushindi kwa ajili ya Yakobo.
5 Kwa uwezo wako tunawasukuma nyuma watesi wetu; kwa jina lako tunawakanyaga adui zetu.
Kwa uweza wako tutawaangusha chini maadui zetu; kwa jina lako tutatembea juu yao, wale wanao inuka dhidi yetu.
6 Siutumaini upinde wangu, upanga wangu hauniletei ushindi;
Kwa maana sitauamini upinde wangu, wala upanga wangu hautaniokoa.
7 bali wewe unatupa ushindi juu ya adui zetu, unawaaibisha watesi wetu.
Bali wewe ndeye uliyetuokoa na adui zetu, na umewaaibisha wale watuchukiao.
8 Katika Mungu wetu tunajivuna mchana kutwa, nasi tutalisifu jina lako milele.
Katika Mungu tumefanywa kujivuna siku zote, nasi tutalishukuru jina lako milele. (Selah)
9 Lakini sasa umetukataa na kutudhili, wala huendi tena na jeshi letu.
Lakini sasa umetutupa na kutufedhehesha, na hauendi na majeshi yetu.
10 Umetufanya turudi nyuma mbele ya adui, nao watesi wetu wametuteka nyara.
Umetufanya kuwakimbia maadui zetu; na wale watuchukiao huchukua vitu vyetu vya thamani kwa ajili yao wenyewe.
11 Umetuacha tutafunwe kama kondoo na umetutawanya katika mataifa.
Umetufanya kama kondoo aliyeandaliwa kwa ajili ya chakula na umetutawanya kati ya mataifa.
12 Umewauza watu wako kwa fedha kidogo, wala hukupata faida yoyote kwa mauzo yao.
Wewe unawauza watu wako bure; kwa kufanya hivyo haukupata faida.
13 Umetufanya lawama kwa jirani zetu, dharau na dhihaka kwa wale wanaotuzunguka.
Wewe umetufanya kukemewa na majirani zetu, kuchekwa, na kudhihakiwa na wale wanao tuzunguka.
14 Umetufanya kuwa mithali miongoni mwa mataifa, mataifa hutikisa vichwa vyao.
Umetufaya kituko kati ya mataifa, .......................................................
15 Fedheha yangu iko mbele yangu mchana kutwa, na uso wangu umejaa aibu tele,
Siku zote fedheha yangu iko mbele yangu, na aibu ya uso wangu imenifunika
16 kwa ajili ya dhihaka ya wale wanaonilaumu na kunitukana, kwa sababu ya adui, ambaye anatamani kulipiza kisasi.
kwa sababu ya sauti yake iliyo kemea na kutukana, kwa sababu ya adui na kisasi.
17 Hayo yote yametutokea, ingawa tulikuwa hatujakusahau wala hatujaenda kinyume na agano lako.
Yote haya yametupata sisi; bado hatukukusahau wewe wala kulikosea agano lako.
18 Mioyo yetu ilikuwa haijarudi nyuma; nyayo zetu zilikuwa hazijaiacha njia yako.
Mioyo yetu haikukengeuka; hatua zetu hazikuiacha njia yako.
19 Lakini ulituponda na kutufanya makao ya mbweha, na ukatufunika kwa giza nene.
Bali wewe umetuadhibu vikali katika mahali pa mbweha na kutufunika na uvuli wa mauti.
20 Kama tungalikuwa tumelisahau jina la Mungu wetu au kunyooshea mikono yetu kwa mungu mgeni,
Ikiwa tumelisahau jina la Mungu wetu au kueneza mikono yetu kwa Mungu mgeni,
21 je, Mungu hangaligundua hili, kwa kuwa anazijua siri za moyo?
Mungu asingeligundua hili? Kwa maana yeye anazijua siri za moyo.
22 Hata hivyo kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa; tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa.
Hakika, kwa ajili ya jina lako tutauawa siku zote; tunahesabiwa kuwa kondoo kwa ajili ya kuchinjwa.
23 Amka, Ee Bwana! Kwa nini unalala? Zinduka! Usitukatae milele.
Bwana, amka, kwa nini unalala? Inuka, usitutupe moja kwa moja.
24 Kwa nini unauficha uso wako na kusahau taabu na mateso yetu?
Kwa nini unaficha uso wako na kusahau mateso yetu na kukandamizwa kwetu?
25 Tumeshushwa hadi mavumbini, miili yetu imegandamana na ardhi.
Kwa maana tumeyeyushwa kwenye mavumbi; miili yetu imeshikamana na ardhi.
26 Inuka na utusaidie, utukomboe kwa sababu ya upendo wako usio na mwisho.
Inuka utusaidie na utuokoe kwa ajili ya uaminifu wa agano lako.

< Zaburi 44 >