< Zaburi 34 >

1 Zaburi ya Daudi, alipojifanya mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimfukuza, naye akaondoka. Nitamtukuza Bwana nyakati zote, sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote.
Nitamsifu Yahwe wakati wote, siku zote sifa zake zitakuwa mdomoni mwangu.
2 Nafsi yangu itajisifu katika Bwana, walioonewa watasikia na wafurahi.
Nitamsifu Yahwe! walio onewa wasikie na kufurahi.
3 Mtukuzeni Bwana pamoja nami, naam, na tulitukuze jina lake pamoja.
Msifuni Yahwe pamoja nami, kwa pamoja tuliinue jina lake.
4 Nilimtafuta Bwana naye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote.
Nilimuomba Yahwe msaada naye akanijibu, akanipa ushindi juu ya hofu yangu yote.
5 Wale wamtazamao hutiwa nuru, nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe.
Wale wanao mtazama yeye wana furaha, na nyuso zao hazina aibu.
6 Maskini huyu alimwita Bwana, naye akamsikia, akamwokoa katika taabu zake zote.
Huyu mtu aliye onewa alilia na Yahwe akamsikia na kumuokoa kwenye matatizo yake yote.
7 Malaika wa Bwana hufanya kituo akiwazunguka wale wamchao, naye huwaokoa.
Malaika wa Yahwe huweka kambi wakiwazunguka wale wanao muogopa yeye na kuwaokoa.
8 Onjeni mwone kwamba Bwana ni mwema, heri mtu yule anayemkimbilia.
Onjeni muone Yahwe ni mzuri. Amebarikiwa mtu yule ambaye Yahwe ni kimbilio lake.
9 Mcheni Bwana enyi watakatifu wake, kwa maana wale wamchao hawapungukiwi na chochote.
Muogopeni Yahwe, ninyi watu watakatifu wake. Hakuna kupungukikwa kwa wale wanao mhofu yeye.
10 Wana simba wenye nguvu hutindikiwa na kuona njaa, bali wale wamtafutao Bwana hawatakosa kitu chochote kilicho chema.
Simba wadogo wakati mwingine hukosa chakula na kuteseka kwa njaa, bali wale wamtafutao Yahwe hawatapungukiwa chochote kilicho kizuri.
11 Njooni, watoto wangu, mnisikilize, nitawafundisha kumcha Bwana.
Njoni, wana, mnisikilize mimi. nitawafundisha ninyi hofu ya Yahwe.
12 Yeyote kati yenu anayependa uzima na kutamani kuziona siku nyingi njema,
Mtu nani aliyepo ambaye anatamani maisha na anapenda kuwa na siku nyingi, ili kwamba aweze kuona vizuri?
13 basi auzuie ulimi wake na mabaya, na midomo yake kutokana na kusema uongo.
Hivyo uepushe ulimi wako na uovu na uilinde midomo yako kuongea uongo.
14 Aache uovu, atende mema, aitafute amani na kuifuatilia.
Uache uovu na utende mema. Uitafute amani na kuiendea amani.
15 Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake yako makini kusikiliza kilio chao.
Macho ya Yahwe yako kwenye haki na masikio yake huelekea kulia kwao.
16 Uso wa Bwana uko kinyume na watendao maovu, ili kufuta kumbukumbu lao duniani.
Uso wa Yahwe uko kinyume na wale watendao uovu, kuikatilia mbali kumbukumbu yao duniani.
17 Wenye haki hulia, naye Bwana huwasikia, huwaokoa katika taabu zao zote.
Wenye haki hulia na Yahwe husikia na kuwaokoa kwenye matatizo yao yote.
18 Bwana yu karibu na waliovunjika moyo, na huwaokoa waliopondeka roho.
Yahwe yu karibu nao waliovunjika moyo, naye huwaokoa waliogandamizwa rohoni.
19 Mwenye haki ana mateso mengi, lakini Bwana humwokoa nayo yote,
Mateso ya wenye haki ni mengi, bali Yahwe huwaokoa nayo yote.
20 huhifadhi mifupa yake yote, hata mmoja hautavunjika.
Yeye huitunza mifupa yake yote, hakuna hata mmoja wao utavunjika.
21 Ubaya utamuua mtu mwovu, nao adui za mwenye haki watahukumiwa.
Uovu utawauwa waovu. Wale wachukiao haki watahukumiwa.
22 Bwana huwakomboa watumishi wake, yeyote anayemkimbilia yeye hatahukumiwa kamwe.
Yahwe huokoa maisha ya watumishi wake. Hakuna atakaye hukumiwa hata mmoja atafutaye usalama katika yeye.

< Zaburi 34 >