< Zaburi 30 >

1 Utenzi wa kuweka wakfu hekalu. Zaburi ya Daudi. Nitakutukuza wewe, Ee Bwana, kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi, na hukuacha adui zangu washangilie juu yangu.
מזמור שיר חנכת הבית לדוד ארוממך יהוה כי דליתני ולא שמחת איבי לי׃
2 Ee Bwana, Mungu wangu, nilikuita unisaidie na wewe umeniponya.
יהוה אלהי שועתי אליך ותרפאני׃
3 Ee Bwana, umenitoa Kuzimu, umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti. (Sheol h7585)
יהוה העלית מן שאול נפשי חייתני מיורדי בור׃ (Sheol h7585)
4 Mwimbieni Bwana, enyi watakatifu wake; lisifuni jina lake takatifu.
זמרו ליהוה חסידיו והודו לזכר קדשו׃
5 Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi, bali upendo wake hudumu siku zote. Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha, lakini asubuhi kukawa na furaha.
כי רגע באפו חיים ברצונו בערב ילין בכי ולבקר רנה׃
6 Nilipofanikiwa nilisema, “Sitatikiswa kamwe.”
ואני אמרתי בשלוי בל אמוט לעולם׃
7 Ee Bwana, uliponijalia, uliuimarisha mlima wangu, lakini ulipouficha uso wako nilifadhaika.
יהוה ברצונך העמדתה להררי עז הסתרת פניך הייתי נבהל׃
8 Kwako wewe, Ee Bwana, niliita, kwa Bwana niliomba rehema:
אליך יהוה אקרא ואל אדני אתחנן׃
9 “Kuna faida gani katika kuangamia kwangu? Katika kushuka kwangu shimoni? Je, mavumbi yatakusifu? Je, yatatangaza uaminifu wako?
מה בצע בדמי ברדתי אל שחת היודך עפר היגיד אמתך׃
10 Ee Bwana, unisikie na kunihurumia, Ee Bwana, uwe msaada wangu.”
שמע יהוה וחנני יהוה היה עזר לי׃
11 Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza, ulinivua nguo za gunia ukanivika shangwe,
הפכת מספדי למחול לי פתחת שקי ותאזרני שמחה׃
12 ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya. Ee Bwana Mungu wangu, nitakushukuru milele.
למען יזמרך כבוד ולא ידם יהוה אלהי לעולם אודך׃

< Zaburi 30 >