< Zaburi 28 >
1 Zaburi ya Daudi. Ninakuita wewe, Ee Bwana, Mwamba wangu; usiwe kwangu kama kiziwi. Kwa sababu ukinyamaza nitafanana na walioshuka shimoni.
Yahwe, ninalia; mwamba wangu, usinipuuze. Ikiwa haunijibu, nitaungana na wale waendao chini kaburini.
2 Sikia kilio changu unihurumie ninapokuita kwa ajili ya msaada, niinuapo mikono yangu kuelekea Patakatifu pa Patakatifu pako.
Sikia kilio cha kusihi kwangu pale niitapo msaada kutoka kwako, niinuapo mikono yangu mbele ya mahali patakatifu zaidi!
3 Usiniburute pamoja na waovu, pamoja na hao watendao mabaya, ambao huzungumza na jirani zao maneno mazuri, lakini mioyoni mwao wameficha chuki.
Usiniburute pamoja na waovu, wale wafanyao uovu, waongeao amani na majirani zao lakini mioyoni mwao mna uovu.
4 Walipe sawasawa na matendo yao, sawasawa na matendo yao maovu; walipe sawasawa na kazi za mikono yao, uwalipe wanavyostahili.
Uwape kulingana na sitahili ya matendo yao na uwalipe kulingana na madai ya maovu yao, uwalipe kwa ajili ya kazi ya mikono yao na uwape kile wanachostahili.
5 Kwa kuwa hawaheshimu kazi za Bwana, na yale ambayo mikono yake imetenda, atawabomoa na kamwe hatawajenga tena.
Kwa sababu hawayaelewi matendo ya Yahwe wala kazi ya mikono yake, atawakanyaga kanyaga chini na hata wajenga tena wao.
6 Bwana asifiwe, kwa maana amesikia kilio changu nikimwomba anihurumie.
Abarikiwe Yahwe kwa sababu yeye amesikia sauti ya kusihi kwangu!
7 Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu, moyo wangu umemtumaini yeye, nami nimesaidiwa. Moyo wangu unarukaruka kwa furaha nami nitamshukuru kwa wimbo.
Yahwe ni nguvu yangu na ngao yangu; moyo wangu wa humwamini yeye, na ninasaidiwa. Kwa hiyo moyo wangu hufurahia sana, nami nitamsifu yeye kwa kuimba.
8 Bwana ni nguvu ya watu wake, ngome ya wokovu kwa mpakwa mafuta wake.
Yahwe ni nguvu ya watu wake, naye ni mkombozi salama wa wapakwa mafuta wake.
9 Waokoe watu wako na uubariki urithi wako; uwe mchungaji wao na uwabebe milele.
Uwaokoe watu wako na uwabariki warithi wako. Uwe mchungaji wao na uwabebe milele.