< Zaburi 21 >
1 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Ee Bwana, mfalme huzifurahia nguvu zako. Tazama jinsi ilivyo kuu furaha yake kwa ushindi unaompa!
Kwa kiongozi wa muziki. Zaburi ya Daudi. Mfalme anashangilia katika uweza wako, Yahwe! Ni kwa namna kuu anashangilia katika wokovu uliouleta!
2 Umempa haja ya moyo wake na hukumzuilia maombi ya midomo yake.
Wewe umempa yeye matamanio ya moyo wake na hauja mkatalia maombi midomo yake.
3 Ulimkaribisha kwa baraka tele na kumvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.
Kwa kuwa wewe unamletea baraka nyingi; wewe uliweka katika kichwa chake taji ya dhahabu iliyo safi kabisa.
4 Alikuomba maisha, nawe ukampa, wingi wa siku milele na milele.
Yeye alikuomba wewe maisha; ukampatia maisha; wewe ulimpatia maisha malefu milele na milele.
5 Kutokana na ushindi uliompa, utukufu wake ni mkubwa, umeweka juu yake fahari na utukufu.
Yeye utukufu wake ni mkuu kwa sababu ya ushindi wako; wewe umemuwekea mapambo na enzi.
6 Hakika umempa baraka za milele, umemfanya awe na furaha kwa shangwe ya uwepo wako.
Kwa kuwa unampatia yeye baraka za kudumu; unamfurahisha kwa furaha ya uwepo wako.
7 Kwa kuwa mfalme anamtumaini Bwana; kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa.
Kwa kuwa Mfalme humwamini Yahwe; kwa kupitia uaminifu wa agano la aliye juu zaidi yeye hataondolewa.
8 Mkono wako utawashika adui zako wote, mkono wako wa kuume utawakamata adui zako.
Mkono wako utawakamata adui zangu wote wote; mkono wako wa kuume utawakamata wale wote wanao kuchukia.
9 Wakati utakapojitokeza utawafanya kama tanuru ya moto. Katika ghadhabu yake Bwana atawameza, moto wake utawateketeza.
Wakati wa hasira yako, wewe utawachoma kama katika tanuru la moto. Yahwe atawamaliza wao katika hasira yake, na moto utawateketeza upesi wao.
10 Utawaangamiza wazao wao kutoka duniani, uzao wao kutoka wanadamu.
Wewe utawaangamiza watoto wao duniani na ukoo wao kutoka katika mrorongo wa wanadamu.
11 Ingawa watapanga mabaya dhidi yako na kutunga hila, hawawezi kufanikiwa,
Kwa kuwa walikusudia kukufanyia mambo maovu wewe; wao walitunga njama ambayo kwayo hawawezi kufanikiwa!
12 kwa kuwa utawafanya wakimbie utakapowalenga usoni pao kwa mshale kutoka kwenye upinde wako.
Kwa kuwa wewe utawarudisha nyuma; wewe utafyatua upinde wako mbele yao.
13 Ee Bwana, utukuzwe katika nguvu zako, tutaimba na kusifu nguvu zako.
Uninuliwe, Yahwe, katika uweza wako; tutaimba na kusifu nguvu zako.