< Zaburi 19 >

1 Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu, anga zahubiri kazi ya mikono yake.
למנצח מזמור לדוד ב השמים מספרים כבוד-אל ומעשה ידיו מגיד הרקיע
2 Siku baada ya siku zinatoa habari, usiku baada ya usiku zinatangaza maarifa.
יום ליום יביע אמר ולילה ללילה יחוה-דעת
3 Hakuna msemo wala lugha, ambapo sauti zao hazisikiki.
אין-אמר ואין דברים בלי נשמע קולם
4 Sauti yao imeenea duniani pote, nayo maneno yao yameenea hadi miisho ya ulimwengu. Katika mbingu amepiga hema kwa ajili ya jua,
בכל-הארץ יצא קום ובקצה תבל מליהם לשמש שם-אהל בהם
5 linafanana na bwana arusi akitoka chumbani mwake, kama shujaa afurahiavyo kukamilisha kushindana kwake.
והוא--כחתן יצא מחפתו ישיש כגבור לרוץ ארח
6 Huchomoza upande mmoja wa mbingu, na kufanya mzunguko wake hadi upande mwingine. Hakuna kilichojificha joto lake.
מקצה השמים מוצאו--ותקופתו על-קצותם ואין נסתר מחמתו
7 Sheria ya Bwana ni kamilifu, ikihuisha nafsi. Shuhuda za Bwana ni za kuaminika, zikimpa mjinga hekima.
תורת יהוה תמימה משיבת נפש עדות יהוה נאמנה מחכימת פתי
8 Maagizo ya Bwana ni kamili, nayo hufurahisha moyo. Amri za Bwana huangaza, zatia nuru machoni.
פקודי יהוה ישרים משמחי-לב מצות יהוה ברה מאירת עינים
9 Kumcha Bwana ni utakatifu, nako kwadumu milele. Amri za Bwana ni za hakika, nazo zina haki.
יראת יהוה טהורה--עומדת לעד משפטי-יהוה אמת צדקו יחדו
10 Ni za thamani kuliko dhahabu, kuliko dhahabu iliyo safi sana, ni tamu kuliko asali, kuliko asali kutoka kwenye sega.
הנחמדים--מזהב ומפז רב ומתוקים מדבש ונפת צופים
11 Kwa hizo mtumishi wako anaonywa, katika kuzishika kuna thawabu kubwa.
גם-עבדך נזהר בהם בשמרם עקב רב
12 Ni nani awezaye kutambua makosa yake? Nisamehe makosa yangu nisiyoyajua.
שגיאות מי-יבין מנסתרות נקני
13 Mlinde mtumishi wako na dhambi za makusudi, nazo zisinitawale. Ndipo nitakapokuwa sina lawama, wala sitakuwa na hatia ya kosa kubwa.
גם מזדים חשך עבדך-- אל-ימשלו-בי אז איתם ונקיתי מפשע רב
14 Maneno ya kinywa changu na mawazo ya moyo wangu, yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu na Mkombozi wangu.
יהיו לרצון אמרי-פי והגיון לבי לפניך יהוה צורי וגאלי

< Zaburi 19 >