< Zaburi 124 >

1 Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi. Kama Bwana asingalikuwa upande wetu; Israeli na aseme sasa:
“Kama Yahwe asingekuwa upande wetu,” Israeli na aseme sasa,
2 kama Bwana asingalikuwa upande wetu, wakati watu walipotushambulia,
“Kama asingekuwa Yahwe ambaye alikuwa upande wetu wakati watu walipoinuka dhidi yetu,
3 wakati hasira yao ilipowaka dhidi yetu, wangalitumeza tungali hai,
basi wangekuwa wametumeza tungali hai hasira yao lipozidi dhidi yetu.
4 mafuriko yangalitugharikisha, maji mengi yangalitufunika,
Maji yangetugharikisha; mto ungetuzidia.
5 maji yaendayo kasi yangalituchukua.
Kisha maji yafurikayo yangetuzamisha.”
6 Bwana asifiwe, yeye ambaye hakuruhusu turaruliwe kwa meno yao.
Atukuzwe Yahwe, ambaye hajaruhusu tuwe mawindo kwa meno yao.
7 Tumeponyoka kama ndege kutoka mtego wa mwindaji; mtego umevunjika, nasi tukaokoka.
Tumetoroka kama ndege mtegoni mwa wawindaji; mtego umevunjika, nasi tumetoroka.
8 Msaada wetu ni katika jina la Bwana, Muumba wa mbingu na dunia.
Msaada wetu uko katika Yahwe, aliyeziumba mbingu na nchi.

< Zaburi 124 >