< Zaburi 120 >

1 Wimbo wa kwenda juu. Katika dhiki yangu namwita Bwana, naye hunijibu.
Katika dhiki yangu nilimuita Yahwe, naye akanijibu.
2 Ee Bwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo na ndimi za udanganyifu.
Uiokoe nasfi yangu, yahwe, dhidi ya wale wadanganyao kwa midomo yao na wanenao hila kwa ndimi zao.
3 Atakufanyia nini, au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu?
Yahwe atawaadhibu vipi, na atawafanyia kitu gani zaidi, ninyi mlio na ulimi mdanganyifu?
4 Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa, kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu.
Atawaadhibu kwa mishale ya shujaa iliyo nolewa kwa makaa ya moto ya mretemu.
5 Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki, kwamba naishi katikati ya hema za Kedari!
Ole wangu mimi kwa sababu ninaishi kwa muda Mesheki; huko nyuma niliishi kati ya maskani ya Kedari.
6 Nimeishi muda mrefu mno miongoni mwa wale wanaochukia amani.
Kwa muda mrefu sana niliisha na wale waichukiao amani.
7 Mimi ni mtu wa amani; lakini ninaposema, wao wanataka vita.
Nipo kwa ajili ya amani, lakini ninenapo, wao wako kwa ajili ya vita.

< Zaburi 120 >