< Nehemia 10 >
1 Wale waliotia muhuri walikuwa: Nehemia mtawala, mwana wa Hakalia. Sedekia,
Wale ambao waliweka majina yao kwenye nyaraka zilizofunikwa walikuwa Nehemia mwana wa Hakalia gavana, na makuhani waliowekwa walikuwa Sedekia,
2 Seraya, Azaria, Yeremia,
Seraya, Azaria, Yeremia,
3 Pashuri, Amaria, Malkiya,
Pashuri, Amaria, Malkiya,
4 Hatushi, Shebania, Maluki,
Hamshi, Shekania, Maluki,
5 Harimu, Meremothi, Obadia,
Harimu, Meremothi, Obadia,
6 Danieli, Ginethoni, Baruku,
Danieli, Ginethoni, Baruki,
7 Meshulamu, Abiya, Miyamini,
Meshulamu, Abiya, Miyamini,
8 Maazia, Bilgai na Shemaya. Hawa ndio waliokuwa makuhani.
Maazia, Bilgai na Shemaya. Hawa walikuwa makuhani.
9 Walawi: Yeshua mwana wa Azania, Binui wa wana wa Henadadi, Kadmieli,
Walawi walikuwa Yeshua mwana wa Azania, Binui wa jamaa ya Henadadi, Kadmieli,
10 na wenzao: Shebania, Hodia, Kelita, Pelaya, Hanani,
na Walawi wenzake, Shebania, Hodia, Kelita, Pelaya, Hanani,
11 Mika, Rehobu, Hashabia,
Mika, Rehobu, Hashabia,
12 Zakuri, Sherebia, Shebania,
Zakuri, Sherebia, Shebania,
13 Hodia, Bani na Beninu.
Hodiya, Bani na Beninu.
14 Viongozi wa watu: Paroshi, Pahath-Moabu, Elamu, Zatu, Bani,
Viongozi wa watu walikuwa Paroshi, Pahath-Moabu, Elamu, Zatu, Bani,
16 Adoniya, Bigwai, Adini,
Adoniya, Bigwai, Adini,
17 Ateri, Hezekia, Azuri,
Ateri, Hezekia, Azuri,
18 Hodia, Hashumu, Besai,
Hodia, Hashumu, Besai,
19 Harifu, Anathothi, Nebai,
Harifu, Anathothi, Nobai,
20 Magpiashi, Meshulamu, Heziri,
Magpiashi, Meshulamu, Heziri,
21 Meshezabeli, Sadoki, Yadua,
Meshezabeli, Sadoki, Yadua,
22 Pelatia, Hanani, Anaya,
Pelatia, Hanani, AnaYA,
23 Hoshea, Hanania, Hashubu,
Hoshea, Hanania, Hashubu,
24 Haloheshi, Pilha, Shobeki,
Haloheshi, Pilha, Shobeki,
25 Rehumu, Hashabna, Maaseya,
Rehumu, Hashabna, Maaseya,
27 Maluki, Harimu na Baana.
Maluki, Harimu na Baana.
28 “Watu wengine wote, wakiwa ni makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, watumishi wa Hekalu, na wale wote waliojitenga na mataifa jirani kwa ajili ya Sheria ya Mungu, pamoja na wake zao na wana wao na binti zao wote waliokuwa na uwezo wa kufahamu,
Na watu wengine waliokuwa makuhani, na Walawi, na walinzi wa malango, na waimbaji, na watumishi wa hekalu, na wote waliokuwa wamejitenga wenyewe na watu wa nchi za jirani, kwa sheria ya Mungu, na wanawake zao, na wana wao, na Binti zao, wote walio na ujuzi na ufahamu,
29 basi hawa wote wanajiunga na ndugu zao na wakuu wao, na kujifunga kwa laana na kwa kiapo kufuata Sheria ya Mungu iliyotolewa kupitia kwa Mose mtumishi wa Mungu, na kutii kwa uangalifu amri zote, maagizo na sheria za Bwana, Bwana wetu.
walijiunga na ndugu zao, wakuu wao, na kujifunga katika laana na kiapo cha kutembea katika sheria ya Mungu, iliyotolewa na Musa mtumishi wa Mungu, na kuzingatia na kutii amri zote za Bwana Mungu wetu na hukumu zake na sheria zake.
30 “Tunaahidi kutowaoza binti zetu kwa watu wanaotuzunguka, wala kuwaoza wana wetu binti zao.
Tuliahidi kuwa hatuwezi kuwapa binti zetu watu wa nchi au kuchukua binti zao kwa wana wetu.
31 “Wakati mataifa jirani waletapo bidhaa zao au nafaka kuuza siku ya Sabato, hatutazinunua kutoka kwao siku ya Sabato, wala siku nyingine yoyote takatifu. Kila mwaka wa saba, tutaacha kuilima ardhi na tutafuta madeni yote.
Pia tuliahidi kwamba ikiwa watu wa nchi wataleta bidhaa au nafaka yoyote ya kuuza siku ya Sabato, hatuwezi kununua kutoka kwao siku ya Sabato au siku yoyote takatifu. Kila mwaka wa saba tutaacha mashamba yetu kupumzika, na tutafuta madeni yote yaliyotokana na Wayahudi wengine.
32 “Tunakubali wajibu wa kutimiza amri za kutoa theluthi ya shekeli kila mwaka kwa ajili ya utumishi wa nyumba ya Mungu:
Tulikubali amri za kutoa shilingi ya shekeli kila mwaka kwa ajili ya huduma ya nyumba ya Mungu wetu,
33 Kwa ajili ya mikate ya Wonyesho, kwa ajili ya sadaka za kawaida za nafaka na sadaka za kuteketezwa, kwa ajili ya sadaka za siku za Sabato, Sikukuu za Mwandamo wa Mwezi na sikukuu nyingine zilizoamriwa, kwa ajili ya sadaka takatifu, kwa ajili ya sadaka za dhambi ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, na kwa ajili ya kazi zote za nyumba ya Mungu wetu.
kutoa mkate wa uwepo, na sadaka ya nafaka ya kawaida, sadaka za kuteketezwa siku za Sabato, sikukuu mpya za mwezi na sikukuu za kuteketezwa, na sadaka takatifu, na sadaka za dhambi za kufanya upatanisho kwa Israeli, pamoja na kazi yote ya nyumba ya Mungu wetu.
34 “Sisi makuhani, Walawi na watu, tumepiga kura kuamua kuwa kila mmoja wa jamaa zetu lazima alete katika nyumba ya Mungu wetu kwa nyakati maalum kila mwaka mchango wa kuni za kukokea moto katika madhabahu ya Bwana Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika Sheria.
Na makuhani, Walawi, na watu wakapiga kura kwa ajili ya sadaka ya kuni. Kura ilichagua ni nani wa familia zetu ataleta kuni ndani ya nyumba ya Mungu wetu kwa nyakati zilizowekwa kila mwaka. Kuni hizo zilichomwa juu ya madhabahu ya Bwana Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika sheria.
35 “Pia tunachukua wajibu wa kuleta malimbuko ya mazao yetu na matunda ya kwanza ya kila mti wa matunda katika nyumba ya Bwana kila mwaka.
Tuliahidi kuleta nyumbani kwa Bwana matunda ya kwanza yaliyotokana na udongo wetu, na matunda ya kwanza ya mti kila mwaka.
36 “Kama pia ilivyoandikwa katika Sheria, tutawaleta wazaliwa wetu wa kwanza wa kiume, na wa mifugo yetu, yaani wa ngʼombe wetu na wa makundi yetu ya kondoo na mbuzi, katika nyumba ya Mungu wetu, kwa ajili ya makuhani wanaohudumu huko.
Na kama ilivyoandikwa katika sheria, tuliahidi kuleta nyumbani kwa Mungu na kwa makuhani watumikao hapo wazaliwa wa kwanza wa wana wetu ma wanyama wetu.
37 “Zaidi ya hayo, tutaleta katika ghala za nyumba ya Mungu wetu, kwa makuhani, vyakula vya kwanza vya mashamba yetu, sadaka zetu za nafaka, matunda ya miti yetu yote, divai yetu mpya na mafuta. Nasi tutaleta zaka za mazao yetu kwa Walawi, kwa kuwa Walawi ndio ambao hukusanya zaka katika miji yote tunakofanya kazi.
Tutaleta unga wa kwanza na sadaka zetu za nafaka, na matunda ya kila mti, na divai mpya na mafuta tutaleta kwa makuhani, kwenye vyumba vya kuhifadhi vya nyumba ya Mungu wetu. Tutawaletea Walawi sehemu ya kumi kutoka kwenye udongo wetu kwa sababu Walawi hukusanya zaka katika miji yote tunayofanya kazi.
38 Kuhani atokanaye na uzao wa Aroni atashirikiana na Walawi wakati wanapopokea zaka, nao Walawi itawapasa kuleta sehemu ya kumi ya zaka katika nyumba ya Mungu wetu katika ghala za hazina.
Kuhani, mzao wa Haruni, lazima awe na Walawi wakati wanapopokea zaka. Walawi wanapaswa kuleta sehemu ya kumi ya zaka katika nyumba ya Mungu wetu kwenye vyumba vya kuhifadhi hazima.
39 Watu wa Israeli pamoja na Walawi itawapasa kuleta michango yao ya nafaka, divai mpya na mafuta katika vyumba vya ghala, mahali vifaa vya mahali patakatifu vinapohifadhiwa, na wanapokaa makuhani wanaohudumu, na mabawabu na waimbaji. “Hatutaacha kuijali nyumba ya Mungu wetu.”
Kwa maana wana wa Israeli na wana wa Lawi, wataleta sadaka za nafaka, divai mpya, na mafuta katika vyumba vya kuhifadhi ambapo vitu vya patakatifu vinasimamishwa, na mahali pa makuhani watumishi, na walinzi wa mlango, na waimbaji. Hatuwezi kuacha nyumba ya Mungu wetu.