< Malaki 2 >

1 “Sasa onyo hili ni kwa ajili yenu, enyi makuhani.
Sasa, ninyi makuhani, amri hii ni kwa ajili yenu.
2 Kama hamtasikiliza, na kama hamtaki kuielekeza mioyo yenu kuheshimu Jina langu, nitatuma laana juu yenu, nami nitalaani baraka zenu. Naam, nimekwisha kuzilaani, kwa sababu hamkuielekeza mioyo yenu kuniheshimu mimi,” Asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.
Kama hamtasikiliza, na kama hamtalichukua hili mioyoni mwenu na kunipa utukufu kwa jina langu, “asema Bwana wa Majeshi, Kisha nitatuma laana kwenu, na nitalaani baraka zenu. Kiukweli, nilishawalaani tayari, kwa sababu hujaweka sheria zangu moyoni.
3 “Kwa sababu yenu nitawakatilia mbali wazao wenu. Nitazipaka nyuso zenu mavi, mavi ya dhabihu zenu. Nanyi mtafukuzwa pamoja nazo mtoke mbele zangu.
Tazama, nitakikemea kizazi chako, na nitapaka mavi juu ya uso wako, mavi ya dhabihu zenu, na mtachukuliwa pamoja nayo.
4 Nanyi mtajua kuwa nimewapelekea onyo hili ili kwamba Agano langu na Lawi lipate kuendelea,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.
Na mtajua kwamba nimetuma hii sheria kwenu, kwamba agano langu litakuwa ni juu yangu na Lawi,” asema Bwana wa Majeshi.
5 “Agano langu lilikuwa pamoja naye, agano la uhai na amani, nami nilimpa yote, ili aniche na kuniheshimu, naye akaniheshimu na kusimama akilicha Jina langu.
Agano langu na yeye lilikuwa agano la uhai na amani, na nilimpa vitu hivi kama njia ya kuniheshimu. aliniheshima na alisimama akawa na hofu kwa jina langu.
6 Fundisho la kweli lilikuwa kinywani mwake, wala hakuna uongo wowote uliopatikana katika midomo yake. Alitembea nami katika amani na unyofu, naye akawageuza wengi kutoka dhambini.
Mafundisho ya kweli yalikuwa kwenye kinywa chake, na uovu haukupatikana kinywani mwake. Alitembea na mimi kwa amani na unyoofu, na aliwarudisha wengi kutoka dhambini.
7 “Kwa maana yapasa midomo ya kuhani kuhifadhi maarifa. Tena kutoka kinywani mwake watu wangepaswa kutafuta mafundisho, kwa sababu yeye ni mjumbe wa Bwana Mwenye Nguvu Zote.
kwa sababu midomo ya makuhani huhifadhi maarifa, na watu watatafuta maagizo kutoka kwenye kichwa chake, kwa sababu ni mjumbe wa Bwana wa Majeshi.
8 Lakini mmegeuka mkaiacha njia, na kwa mafundisho yenu mmesababisha wengi kujikwaa. Mmevunja agano na Lawi,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.
lakini umepita mbali na njia ya kweli. Umesababisha wengi kuwa na mashaka ya kutii sheria. umeliharifu agano la Lawi,” asema Bwana wa Majeshi.
9 “Kwa hiyo nimewasababisha ninyi kudharauliwa na kufedheheshwa mbele ya watu wote, kwa sababu hamkufuata njia zangu, bali mmeonyesha upendeleo katika mambo ya sheria.”
Kwa hiyo nimewafanya ninyi nanyi kudharauliwa mbele ya watu, kwa sababu hamkutunza njia zangu, lakini badala yake mnapendelea katika maagizo yenu.
10 Je, sote hatuna Baba mmoja? Hatukuumbwa na Mungu mmoja? Kwa nini basi tunalinajisi Agano la baba zetu kwa kukosa uaminifu kila mmoja kwa mwenzake?
Sisi sote hatuna baba mmoja? Siyo Mungu yule mmoja aliyetuumba sote? kwa nini tunafanyiana hila kila mtu na ndugu yake, mnariharibu agano la baba zetu?
11 Yuda amevunja uaminifu. Jambo la kuchukiza limetendeka katika Israeli na katika Yerusalemu: Yuda amepanajisi mahali patakatifu apendapo Bwana, kwa kuoa binti wa mungu mgeni.
Yuda amefanya hila na ameona kinyaa kwa vitu vilivyowekwa katika Israeli na Yerusalem. Yuda amenajisi mahali patakatifu pa Bwana ambapo anapapenda, na ameoa binti wa miungu migeni.
12 Kwa maana kwa mtu yeyote atendaye jambo hili, Bwana na amkatilie mbali kutoka hema za Yakobo, hata kama huwa anamletea Bwana Mwenye Nguvu Zote sadaka.
Mungu akukatilie mbali kutoka kwenye hema ya Yakobo na uzao wa mtu aliyefanya haya, hata yule anayeleta sadaka kwa Bwana wa Majeshi.
13 Kitu kingine mnachokifanya: Mnaifurikisha madhabahu ya Bwana kwa machozi. Mnalia na kuugua kwa sababu yeye haziangalii tena sadaka zenu wala hazikubali kwa furaha kutoka mikononi mwenu.
Na wewe pia fanya hivyo. Unafunika madhabahu ya Bwana kwa machozi, kwa kilio na kuugua, kwa sababu hatakubali sadaka na kuzipokea kutoka mikononi mwako.
14 Mnauliza, “Kwa nini?” Ni kwa sababu Bwana ni shahidi kati yako na mke wa ujana wako, kwa sababu umevunja uaminifu naye, ingawa yeye ni mwenzako, mke wa agano lako la ndoa.
Lakini wasema, ni kwa sababu gani?” Kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati yako wewe na mke wako wa ujana wako, kinyume chake umekuwa si mwaminifu, ingawa yeye ni mwenzako na mke wa agano lako.
15 Je, Bwana hakuwafanya wao kuwa mmoja? Katika mwili na katika roho wao ni wa Mungu. Kwa nini wawe mmoja? Kwa sababu Mungu alikuwa akitafuta mzao mwenye kumcha Mungu. Kwa hiyo jihadharini wenyewe katika roho zenu, mtu asivunje uaminifu kwa mke wa ujana wake.
Je yeye hakuwafanya kuwa mmoja, hata kwa sehemu ya roho yake? Sasa ni kwanini aliwafanya ninyi kuwa mmoja? Kwa sababu alikuwa anategemea kupata watoto wacha Mungu. Kwa hiyo jiepushe mwenyewe ndani ya moyo wako, na asiwepo mtu asiye mwaminifu kwa mke wa ujana wake.
16 “Ninachukia kuachana,” asema Bwana, Mungu wa Israeli, “pia nachukia mtu anayejivika jeuri kama vazi,” asema Bwana Mwenye Nguvu Zote. Kwa hiyo jihadharini wenyewe katika roho zenu, wala msije mkavunja uaminifu.
“Nakuchukia kuachana,” asema Bwana, Mungu wa Israel, “afunikizaye nguo yake kwa udhalimu,” asema Bwana wa Majeshi. “Kwa hiyo jilinde ewe mwenyewe ndani ya roho yako na usiwe mtu asiye mwaminifu.”
17 Mmemchosha Bwana kwa maneno yenu. Nanyi mnauliza, “Tumemchosha kwa namna gani?” Mmemchosha kwa kusema, “Wote watendao mabaya ni wema machoni pa Bwana, naye anapendezwa nao” au “Mungu wa haki yuko wapi?”
Mmechosha Bwana na maneno. Lakini mwasema, “Tumekuchoshaje?” Kwa kusema Kila mmoja aliyefanya uovu ni mzuri kwa upande wa Bwana, na anafuraha nao;” au “Yuko wapi Mungu wa Haki?”

< Malaki 2 >