< Waamuzi 5 >
1 Ndipo Debora na Baraka mwana wa Abinoamu wakaimba wimbo huu:
Siku hiyo Debora na Baraka, mwana wa Abinoamu waliimba wimbo huu:
2 “Wakuu katika Israeli wanapoongoza, wakati watu wanapojitoa kwa hiari yao wenyewe: mhimidini Bwana!
'Viongozi wanapoongoza mbele ya Israeli, watu wanapojitolea kupigana vita, tunamsifu Bwana!
3 “Sikieni hili, enyi wafalme! Sikilizeni, enyi watawala! Nitamwimbia Bwana, nitaimba; kwa wimbo nitamhimidi Bwana, Mungu wa Israeli.
Sikiliza, ninyi wafalme! Sikiliza kwa makini, ninyi viongozi! Mimi nitamwimbia Bwana; Nami nitamsifu Bwana, Mungu wa Israeli.
4 “Ee Bwana, ulipotoka katika Seiri, ulipopita katika mashamba ya Edomu, nchi ilitetemeka, mbingu nazo zikamwaga, naam, mawingu yakamwaga maji.
Ee Bwana, wakati ulipotoka Seiri, ulipokwenda kutoka Edomu, nchi ilitetemeka, na mbingu pia ilitetemeka; pia mawingu yalitoa maji.
5 Milima ilitetemeka mbele za Bwana, hata ule wa Sinai, mbele za Bwana, Mungu wa Israeli.
Milima ikatoka mbele ya uso wa Bwana; hata Mlima Sinai ukatetemeka mbele ya uso wa Bwana, Mungu wa Israeli.
6 “Katika siku za Shamgari mwana wa Anathi, katika siku za Yaeli, barabara kuu hazikuwa na watu; wasafiri walipita njia za kando.
Katika siku za Shamgari (mwana wa Anathi), katika siku za Jael, barabara kuu ziliachwa, na wale ambao walitembea tu walitumia njia za upepo.
7 Mashujaa walikoma katika Israeli, walikoma mpaka mimi, Debora, nilipoinuka, nilipoinuka kama mama katika Israeli.
Kulikuwa na mashujaa wachache huko Israeli, mpaka mimi, Debora, nilipochukua amri- mama alichukua amri katika Israeli!
8 Walipochagua miungu migeni, vita vilikuja katika malango ya mji, hapakuonekana ngao wala mkuki miongoni mwa mashujaa 40,000 katika Israeli.
Walichagua miungu mpya, kulikuwa na vita katika malango ya jiji lakini bado hapakuwa na ngao au mikuki iliyoonekana kati ya watu elfu arobaini nchini Israeli.
9 Moyo wangu u pamoja na wakuu wa Israeli, pamoja na wale wanaojitoa wenyewe kwa hiari yao miongoni mwa watu. Mhimidini Bwana!
Moyo wangu unawaendea wakuu wa Israeli, pamoja na watu ambao walijitolea -tunambariki Bwana kwa ajili yao!
10 “Nanyi mpandao punda weupe, mkiketi juu ya matandiko ya thamani, nanyi mtembeao barabarani, fikirini
Fikiria juu ya hili- ninyi ambao hupanda punda weupe mmeketi kwenye mazulia, nanyi mnaotembea njiani.
11 juu ya sauti za waimbaji mahali pa kunyweshea maji. Wanasimulia matendo ya haki ya Bwana, matendo ya haki ya mashujaa wake katika Israeli. “Ndipo watu wa Bwana walipoteremka malangoni pa mji.
Sikiliza sauti za wale wanaoimba kwenye maeneo ya kutekea maji. Huko wanasema tena juu ya matendo ya haki ya Bwana, na matendo ya haki ya wapiganaji wake katika Israeli. Ndipo watu wa Bwana wakashuka kwenye malango ya mji.
12 ‘Amka, amka! Debora! Amka, amka, uimbe! Ee Baraka! Inuka, chukua mateka wako uliowateka, ee mwana wa Abinoamu.’
Amka, amka, Debora! Amka, amka, imba wimbo! Simama, Baraka, na uwakamate wafungwa wako, wewe mwana wa Abinoamu.
13 “Ndipo mabaki ya watu wakashuka dhidi ya wenye nguvu, watu wa Bwana, wakashuka dhidi ya mashujaa wenye nguvu.
Wale waliokoka wakaja chini kwa watu wenye nguvu; watu wa Bwana walikuja kwangu pamoja na mashujaa.
14 Kutoka Efraimu wakaja watu, ambao chimbuko lao ni Amaleki; Benyamini akiwa miongoni mwa watu waliokufuata. Kutoka Makiri wakashuka viongozi, na kutoka Zabuloni wale washikao fimbo ya jemadari.
Walikuja kutoka Efraimu, ambao mizizi yao iko katika Amaleki; watu wa Benyamini walikufuata. Wakuu wa Makiri walitoka, na kutoka Zebuloni wale wanaobeba fimbo ya afisa.
15 Wakuu wa Isakari walikuwa pamoja na Debora; naam, Isakari alikuwa pamoja na Baraka, wakija nyuma yake kwa mbio wakielekea bondeni. Katika jamaa za Reubeni, palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni.
Na wakuu wangu katika Isakari walikuwa pamoja na Debora; na Isakari alikuwa na Baraka waliingia bobdeni kwa kasi chini ya amri yake. Miongoni mwa jamaa za Reubeni kulikuwa na utafutaji mkubwa wa moyo.
16 Kwa nini ulikaa katikati ya mazizi ya kondoo kusikiliza sauti ya filimbi zinazoita makundi? Kwa jamaa za Reubeni, palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni.
Kwa nini uliketi katikati ya moto, ukisikiliza wachungaji wakipiga filimbi yao kwa makundi yao? Na kwa jamaa za Reubeni kulikuwa na utafutaji mkubwa wa moyo.
17 Gileadi alikaa ngʼambo ya Yordani. Naye Dani, kwa nini alikaa kwenye merikebu siku nyingi? Asheri alikaa kwa utulivu ufuoni mwa bahari, akikaa kwenye ghuba zake ndogo.
Gileadi alikaa upande wa pili wa Yordani; na Dani, kwa nini alizunguka juu ya meli? Asheri alibakia pwani na akaishi karibu na bandari zake.
18 Watu wa Zabuloni walihatarisha maisha yao, vilevile nao watu wa Naftali.
Zabuloni lilikuwa kabila ambayo lingeweza kuhatarisha maisha yao mpaka kufikia kifo, Nafthali, pia, katika uwanja wa vita.
19 “Wafalme walikuja na kufanya vita; wafalme wa Kanaani walipigana huko Taanaki karibu na maji ya Megido, lakini hawakuchukua fedha wala nyara.
Wafalme walikuja, wakapigana; wafalme wa Kanaani wakapigana huko Taanaki karibu na maji ya Megido. Lakini hawakuondoa fedha kama nyara.
20 Kutoka mbinguni nyota zilipigana, nyota kutoka njia zake zilipigana na Sisera.
Nyota zilipigana kutoka mbinguni, kutoka katika njia zao za mbinguni zilipigana na Sisera
21 Mto wa Kishoni uliwasomba, ule mto wa zamani, mto wa Kishoni. Songa mbele, ee nafsi yangu, kwa ujasiri!
Mto Kishoni uliwaondoa, mto ule wa kale, Mto Kishoni. Endelea mbele nafsi yangu, jipe nguvu!
22 Ndipo kwato za farasi zikafanya mshindo: farasi wake wenye nguvu huenda mbio kwa kurukaruka.
Kisha sauti za hofu za farasi-kupiga mbio, kupigana kwa watu wake wenye nguvu.
23 Malaika wa Bwana akasema, ‘Merozi alaaniwe. Walaaniwe watu wake kwa uchungu, kwa kuwa hawakuja kumsaidia Bwana, kumsaidia Bwana dhidi ya hao wenye nguvu.’
'Ilaani Meroz!' asema malaika wa Bwana. 'Hakika walaani wenyeji wake!' Kwa sababu hawakuja kumsaidia Bwana, kumsaidia Bwana katika vita dhidi ya mashujaa wenye nguvu.
24 “Yaeli abarikiwe kuliko wanawake wote, mkewe Heberi, Mkeni, abarikiwe kuliko wanawake wote waishio kwenye mahema.
Yaeli amebarikiawa zaidi kuliko wanawake wengine wote, Yaeli (mke wa Heberi Mkeni), amebarikiwa zaidi kuliko wanawake wote wanaoishi katika hema.
25 Aliomba maji, naye akampa maziwa; kwenye bakuli la heshima akamletea maziwa mgando.
Mtu yule aliomba maji, naye akampa maziwa; akamletea siagi katika sahani inayofaa kwa wakuu.
26 Akanyoosha mkono wake akashika kigingi cha hema, mkono wake wa kuume ukashika nyundo ya fundi. Akampiga Sisera kwa nyundo, akamponda kichwa chake, akamvunjavunja na kumtoboa paji lake la uso.
Aliweka mkono wake kwenye kigingi cha hema, na mkono wake wa kuia katika nyundo ya mfanyakazi; kwa nyundo akampiga Sisera, alimpiga kichwani kwake. Aliligawanya fuvu lake vipande vipande wakati alipompiga pembeni ya kichwa chake.
27 Aliinama miguuni pa Yaeli, akaanguka; akalala hapo. Pale alipoinama miguuni pake, alianguka; pale alipoinamia, ndipo alipoanguka, akiwa amekufa.
Akaanguka katikati ya miguu yake, akaanguka akalala pale. Kati ya miguu yake akaanguka. Mahali alipoanguka ni pale ambapo aliuawa kwa ukatili.
28 “Kupitia dirishani mamaye Sisera alichungulia; nyuma ya dirisha alilia, akasema, ‘Mbona gari lake linachelewa kufika? Mbona vishindo vya magari yake vimechelewa?’
Aliangalia dirishani - mama yake Sisera aliangalia kupitia kamba na akasema kwa huzuni, 'Kwa nini gari lakelimechelewa kuja? Kwa nini viboko vya farasi vinavyovuta magari yake vimechelewa? '
29 Wanawake wenye busara kuliko wengine wote wakamjibu; naam, husema moyoni mwake,
Wafalme wake wenye hekima walijibu, na yeye mwenyewe akajibu jibu lile
30 ‘Je, hawapati na kugawanya nyara: msichana mmoja au wawili kwa kila mtu, mavazi ya rangi mbalimbali kwa Sisera kuwa nyara, mavazi ya rangi mbalimbali yaliyotariziwa, mavazi yaliyotariziwa vizuri kwa ajili ya shingo yangu: yote haya yakiwa nyara?’
'Je, hawakupata na kugawanya nyara? Tumbo, matumbo mawili kwa kila mtu; nyara ya kitambaa kilichofunikwa kwa Sisera, nyara ya kitambaa kilichofunikwa, nguo mbili za rangi iliyofunikwa kwa misumari ya wale waliopora?
31 “Adui zako wote na waangamie, Ee Bwana! Bali wote wakupendao na wawe kama jua lichomozavyo kwa nguvu zake.” Hivyo nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini.
Naam, adui zako wote wataangamia, Ee Bwana! Lakini marafiki zako watakuwa kama jua wakati linapoongezeka kwa uwezo wake. Na nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini.