< Ayubu 25 >
1 Ndipo Bildadi Mshuhi akajibu:
Kisha Bilidadi Mshuhi akajibu na kusema,
2 “Mamlaka na kuheshimiwa ni vyake Mungu; yeye huthibitisha amani katika mbingu juu.
“Utawala na hofu vipo naye; anaagiza mahali pa juu pake mbinguni.
3 Je, majeshi yake yaweza kuhesabika? Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake?
Je kuna idadi ya majeshi yake? Ni wapi pasipo na nuru yake?
4 Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu? Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi?
Jinsi gani basi mtu awe mwenye haki kama Mungu? Jinsi gani aliyezaliwa na mwanamke awe safi, amekubaliwa naye?
5 Ikiwa hata mwezi sio mwangavu nazo nyota si safi machoni pake,
Tazama, hata mwezi kwake haungazii; nyota hazikosafi mbele zake.
6 sembuse mtu ambaye ni funza: mwanadamu ambaye ni buu tu!”
Ni vipi mtu, aliyemdudu - mwana wa mtu, aliye mdudu!”