< Ayubu 20 >

1 Ndipo Sofari Mnaamathi akajibu:
ויען צפר הנעמתי ויאמר׃
2 “Mawazo yanayonisumbua yananisukuma kujibu, kwa sababu nimehangaika sana.
לכן שעפי ישיבוני ובעבור חושי בי׃
3 Ninasikia makaripio ambayo yananivunjia heshima, nao ufahamu wangu unanisukuma kujibu.
מוסר כלמתי אשמע ורוח מבינתי יענני׃
4 “Hakika unajua jinsi ilivyokuwa tangu zamani, tangu zamani mwanadamu alipowekwa duniani,
הזאת ידעת מני עד מני שים אדם עלי ארץ׃
5 macheko ya mtu mwovu ni ya muda mfupi, nayo furaha ya wasiomcha Mungu hudumu kwa kitambo tu.
כי רננת רשעים מקרוב ושמחת חנף עדי רגע׃
6 Ingawa kujikweza kwake hufikia mbinguni na kichwa chake hugusa mawingu,
אם יעלה לשמים שיאו וראשו לעב יגיע׃
7 ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe. Wale waliomwona watauliza, ‘Yuko wapi?’
כגללו לנצח יאבד ראיו יאמרו איו׃
8 Kama ndoto hutoweka, wala hapatikani tena, amefukuziwa mbali kama maono ya usiku.
כחלום יעוף ולא ימצאוהו וידד כחזיון לילה׃
9 Jicho lililomwona halitamwona tena; mahali pake hapatamwona tena.
עין שזפתו ולא תוסיף ולא עוד תשורנו מקומו׃
10 Watoto wake watalipa yote baba yao aliyowadhulumu maskini, nayo mikono yake itarudisha mali yote aliyonyangʼanya watu.
בניו ירצו דלים וידיו תשבנה אונו׃
11 Nguvu za ujana zilizoijaza mifupa yake, zitalala naye mavumbini.
עצמותיו מלאו עלומו ועמו על עפר תשכב׃
12 “Ingawa uovu ni mtamu kinywani mwake naye huuficha chini ya ulimi wake,
אם תמתיק בפיו רעה יכחידנה תחת לשונו׃
13 ingawa hawezi kukubali kuuachia uende, lakini huuweka kinywani mwake.
יחמל עליה ולא יעזבנה וימנענה בתוך חכו׃
14 Hata hivyo chakula chake kitakuwa kichungu tumboni mwake, nacho kitakuwa sumu kali ya nyoka ndani yake.
לחמו במעיו נהפך מרורת פתנים בקרבו׃
15 Atatema mali alizozimeza; Mungu atalifanya tumbo lake kuzitapika.
חיל בלע ויקאנו מבטנו יורשנו אל׃
16 Atanyonya sumu za majoka; meno ya nyoka mwenye sumu kali yatamuua.
ראש פתנים יינק תהרגהו לשון אפעה׃
17 Hatafurahia vijito, mito inayotiririsha asali na siagi.
אל ירא בפלגות נהרי נחלי דבש וחמאה׃
18 Vile alivyovitaabikia atavirudisha bila kuvila; hatafurahia faida itokanayo na biashara yake.
משיב יגע ולא יבלע כחיל תמורתו ולא יעלס׃
19 Kwa kuwa aliwaonea maskini na kuwaacha pasipo kitu; amenyangʼanya kwa nguvu nyumba asizozijenga.
כי רצץ עזב דלים בית גזל ולא יבנהו׃
20 “Hakika hatakuwa na raha katika kutamani kwake sana; hawezi kujiokoa mwenyewe kwa hazina zake.
כי לא ידע שלו בבטנו בחמודו לא ימלט׃
21 Hakuna chochote kitakachosalia kwa ajili yake ili ale; kufanikiwa kwake hakutadumu.
אין שריד לאכלו על כן לא יחיל טובו׃
22 Katikati ya wingi wa ustawi wake, dhiki itampata; taabu itamjia kwa nguvu zote.
במלאות שפקו יצר לו כל יד עמל תבואנו׃
23 Atakapokuwa amelijaza tumbo lake, Mungu ataionyesha ghadhabu kali dhidi yake, na kumnyeshea mapigo juu yake.
יהי למלא בטנו ישלח בו חרון אפו וימטר עלימו בלחומו׃
24 Ijapokuwa aikimbia silaha ya chuma, mshale wa shaba utamchoma.
יברח מנשק ברזל תחלפהו קשת נחושה׃
25 Atauchomoa katika mgongo wake, ncha ingʼaayo kutoka ini lake. Vitisho vitakuja juu yake;
שלף ויצא מגוה וברק ממררתו יהלך עליו אמים׃
26 giza nene linavizia hazina zake. Moto usiopepewa na mtu utamteketeza, na kuangamiza yaliyosalia nyumbani mwake.
כל חשך טמון לצפוניו תאכלהו אש לא נפח ירע שריד באהלו׃
27 Mbingu zitaweka wazi hatia yake, nayo nchi itainuka kinyume chake.
יגלו שמים עונו וארץ מתקוממה לו׃
28 Mafuriko yataichukua nyumba yake, maji yaendayo kasi katika siku ya ghadhabu ya Mungu.
יגל יבול ביתו נגרות ביום אפו׃
29 Hili ndilo fungu Mungu alilowagawia waovu, urithi uliowekwa kwa ajili yao na Mungu.”
זה חלק אדם רשע מאלהים ונחלת אמרו מאל׃

< Ayubu 20 >