Preface
Read
+
Publisher
Nainoia, Inc.
PO Box 462, Bellefonte, PA 16823
(814) 470-8028
Nainoia Inc, Publisher
LinkedIn/NAINOIA-INC
Third Party Publisher Resources
Request Custom Formatted Verses
Please contact us below
Submit your proposed corrections
I understand that the Aionian Bible republishes public domain and Creative Commons Bible texts and that volunteers may be needed to present the original text accurately. I also understand that apocryphal text is removed and most variant verse numbering is mapped to the English standard. I have entered my corrections under the verse(s) below. Proposed corrections to the Swahili Contemporary Version, Job Chapter 20 https://www.AionianBible.org/Bibles/Swahili---Contemporary/Job/20 1) Ndipo Sofari Mnaamathi akajibu: 2) “Mawazo yanayonisumbua yananisukuma kujibu, kwa sababu nimehangaika sana. 3) Ninasikia makaripio ambayo yananivunjia heshima, nao ufahamu wangu unanisukuma kujibu. 4) “Hakika unajua jinsi ilivyokuwa tangu zamani, tangu zamani mwanadamu alipowekwa duniani, 5) macheko ya mtu mwovu ni ya muda mfupi, nayo furaha ya wasiomcha Mungu hudumu kwa kitambo tu. 6) Ingawa kujikweza kwake hufikia mbinguni na kichwa chake hugusa mawingu, 7) ataangamia milele kama mavi yake mwenyewe. Wale waliomwona watauliza, ‘Yuko wapi?’ 8) Kama ndoto hutoweka, wala hapatikani tena, amefukuziwa mbali kama maono ya usiku. 9) Jicho lililomwona halitamwona tena; mahali pake hapatamwona tena. 10) Watoto wake watalipa yote baba yao aliyowadhulumu maskini, nayo mikono yake itarudisha mali yote aliyonyangʼanya watu. 11) Nguvu za ujana zilizoijaza mifupa yake, zitalala naye mavumbini. 12) “Ingawa uovu ni mtamu kinywani mwake naye huuficha chini ya ulimi wake, 13) ingawa hawezi kukubali kuuachia uende, lakini huuweka kinywani mwake. 14) Hata hivyo chakula chake kitakuwa kichungu tumboni mwake, nacho kitakuwa sumu kali ya nyoka ndani yake. 15) Atatema mali alizozimeza; Mungu atalifanya tumbo lake kuzitapika. 16) Atanyonya sumu za majoka; meno ya nyoka mwenye sumu kali yatamuua. 17) Hatafurahia vijito, mito inayotiririsha asali na siagi. 18) Vile alivyovitaabikia atavirudisha bila kuvila; hatafurahia faida itokanayo na biashara yake. 19) Kwa kuwa aliwaonea maskini na kuwaacha pasipo kitu; amenyangʼanya kwa nguvu nyumba asizozijenga. 20) “Hakika hatakuwa na raha katika kutamani kwake sana; hawezi kujiokoa mwenyewe kwa hazina zake. 21) Hakuna chochote kitakachosalia kwa ajili yake ili ale; kufanikiwa kwake hakutadumu. 22) Katikati ya wingi wa ustawi wake, dhiki itampata; taabu itamjia kwa nguvu zote. 23) Atakapokuwa amelijaza tumbo lake, Mungu ataionyesha ghadhabu kali dhidi yake, na kumnyeshea mapigo juu yake. 24) Ijapokuwa aikimbia silaha ya chuma, mshale wa shaba utamchoma. 25) Atauchomoa katika mgongo wake, ncha ingʼaayo kutoka ini lake. Vitisho vitakuja juu yake; 26) giza nene linavizia hazina zake. Moto usiopepewa na mtu utamteketeza, na kuangamiza yaliyosalia nyumbani mwake. 27) Mbingu zitaweka wazi hatia yake, nayo nchi itainuka kinyume chake. 28) Mafuriko yataichukua nyumba yake, maji yaendayo kasi katika siku ya ghadhabu ya Mungu. 29) Hili ndilo fungu Mungu alilowagawia waovu, urithi uliowekwa kwa ajili yao na Mungu.” Additional comments?
Refresh Captcha
The world's first Holy Bible un-translation!