< Ayubu 16 >

1 Kisha Ayubu akajibu:
Job replied,
2 “Nimepata kusikia mambo mengi kama haya, nanyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha!
“I've heard all this before. You are comforters who just cause trouble!
3 Je, maneno yenu mengi yasiyo na maana hayana mwisho? Mna nini hata mwendelee kushindana kwa maneno?
Will your windy speeches never cease? What's bothering you that you have to answer me?
4 Mimi pia ningeweza kuzungumza kama ninyi, kama mngekuwa katika hali yangu; ningeweza kutoa hotuba nzuri dhidi yenu, na kuwatikisia ninyi kichwa changu.
I could talk like you do if you were in my place, stringing words together to criticize you, ridiculing you with a toss of my head.
5 Lakini kinywa changu kingewatia moyo; faraja kutoka midomoni mwangu, ingewaletea nafuu.
I could build you up by my mouth speaking words; the movement of my lips would ease your pain.
6 “Lakini kama nikisema, maumivu yangu bado hayatulizwi; nami kama nikijizuia, wala hayaondoki.
For me, if I speak it doesn't ease my pain, and if I don't speak the pain is still there.
7 Ee Mungu, hakika umenichakaza; umewaangamiza kabisa watu wa nyumbani mwangu wote.
God, you have worn me out. You have destroyed my whole family.
8 Umenikunjakunja, nalo limekuwa ushahidi; nako kukonda kwangu kumeongezeka sana na kushuhudia dhidi yangu.
You have made me shrivel up, which is a witness against me; my thin body testifies against me.
9 Mungu amenishambulia na kunirarua katika hasira yake, na kunisagia meno yake; adui yangu hunikazia macho yake makali.
He has torn me apart in his anger; in his hostility he has gnashed his teeth at me; my enemy pierces me with his fierce look.
10 Watu wamenifumbulia vinywa vyao kunidhihaki; hunipiga shavuni mwangu kwa dharau, na kuungana pamoja dhidi yangu.
People stare at me with their mouths wide open, they slap me on my cheeks to mock me, they crowd around me to attack me.
11 Mungu amenigeuzia kwa watu wabaya, na kunitupa katika makucha ya waovu.
God has handed me over to evil people; he has thrown me into their hands.
12 Mambo yote yalikuwa mazuri, lakini alinivunjavunja; amenikamata shingo na kuniponda. Amenifanya mimi kuwa shabaha yake;
I was living in peace and he smashed me to pieces. He grabbed me by the neck and dashed me to pieces. He set me up as his target.
13 wapiga upinde wake wananizunguka. Bila huruma, huchoma figo zangu, na kuimwaga nyongo yangu juu ya nchi.
His archers surround me. His arrows pierce my kidneys without mercy. He pours out my gall on the ground.
14 Huniponda tena na tena; hunishambulia kama shujaa wa vita.
Like a wall he breaks me down, breach upon breach, rushing at me like a warrior.
15 “Nimejishonea nguo ya gunia juu ya mwili wangu nami nimekizika kipaji cha uso wangu kwenye vumbi.
I have sown sackcloth to cover my skin; my strength lies broken in the dust.
16 Uso wangu umekuwa mwekundu kwa kulia, macho yangu yamepigwa na giza kuu.
My face is red from crying and dark shadows surround my eyes,
17 Hata hivyo mikono yangu haijafanya jeuri, na maombi yangu ni safi.
although I have done nothing wrong and my prayer is pure.
18 “Ee nchi, usiifunike damu yangu, nacho kilio changu kisinyamazishwe kamwe.
Earth, do not cover up my blood. May my cry find no place to hide.
19 Hata sasa shahidi wangu yuko mbinguni; wakili wangu yuko juu.
Look, right now my witness is in heaven; the one who speaks for me is on high.
20 Mwombezi wangu ni rafiki yangu macho yangu yamwagapo machozi kwa Mungu;
My friends scorn me, but my eyes pour out tears to God.
21 kwa niaba ya mtu anamsihi Mungu kama mtu anavyosihi kwa ajili ya rafiki yake.
I want my witness to speak for me with God as someone does for their friend.
22 “Ni miaka michache tu itapita kabla sijaenda safari ambayo sitarudi.
For in a few short years I shall go down that road from which I shall not return.

< Ayubu 16 >