Preface
Read
+
Publisher
Nainoia, Inc.
PO Box 462, Bellefonte, PA 16823
(814) 470-8028
Nainoia Inc, Publisher
LinkedIn/NAINOIA-INC
Third Party Publisher Resources
Request Custom Formatted Verses
Please contact us below
Submit your proposed corrections
I understand that the Aionian Bible republishes public domain and Creative Commons Bible texts and that volunteers may be needed to present the original text accurately. I also understand that apocryphal text is removed and most variant verse numbering is mapped to the English standard. I have entered my corrections under the verse(s) below. Proposed corrections to the Swahili Contemporary Version, Job Chapter 16 https://www.AionianBible.org/Bibles/Swahili---Contemporary/Job/16 1) Kisha Ayubu akajibu: 2) “Nimepata kusikia mambo mengi kama haya, nanyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha! 3) Je, maneno yenu mengi yasiyo na maana hayana mwisho? Mna nini hata mwendelee kushindana kwa maneno? 4) Mimi pia ningeweza kuzungumza kama ninyi, kama mngekuwa katika hali yangu; ningeweza kutoa hotuba nzuri dhidi yenu, na kuwatikisia ninyi kichwa changu. 5) Lakini kinywa changu kingewatia moyo; faraja kutoka midomoni mwangu, ingewaletea nafuu. 6) “Lakini kama nikisema, maumivu yangu bado hayatulizwi; nami kama nikijizuia, wala hayaondoki. 7) Ee Mungu, hakika umenichakaza; umewaangamiza kabisa watu wa nyumbani mwangu wote. 8) Umenikunjakunja, nalo limekuwa ushahidi; nako kukonda kwangu kumeongezeka sana na kushuhudia dhidi yangu. 9) Mungu amenishambulia na kunirarua katika hasira yake, na kunisagia meno yake; adui yangu hunikazia macho yake makali. 10) Watu wamenifumbulia vinywa vyao kunidhihaki; hunipiga shavuni mwangu kwa dharau, na kuungana pamoja dhidi yangu. 11) Mungu amenigeuzia kwa watu wabaya, na kunitupa katika makucha ya waovu. 12) Mambo yote yalikuwa mazuri, lakini alinivunjavunja; amenikamata shingo na kuniponda. Amenifanya mimi kuwa shabaha yake; 13) wapiga upinde wake wananizunguka. Bila huruma, huchoma figo zangu, na kuimwaga nyongo yangu juu ya nchi. 14) Huniponda tena na tena; hunishambulia kama shujaa wa vita. 15) “Nimejishonea nguo ya gunia juu ya mwili wangu nami nimekizika kipaji cha uso wangu kwenye vumbi. 16) Uso wangu umekuwa mwekundu kwa kulia, macho yangu yamepigwa na giza kuu. 17) Hata hivyo mikono yangu haijafanya jeuri, na maombi yangu ni safi. 18) “Ee nchi, usiifunike damu yangu, nacho kilio changu kisinyamazishwe kamwe. 19) Hata sasa shahidi wangu yuko mbinguni; wakili wangu yuko juu. 20) Mwombezi wangu ni rafiki yangu macho yangu yamwagapo machozi kwa Mungu; 21) kwa niaba ya mtu anamsihi Mungu kama mtu anavyosihi kwa ajili ya rafiki yake. 22) “Ni miaka michache tu itapita kabla sijaenda safari ambayo sitarudi. Additional comments?
Refresh Captcha
The world's first Holy Bible un-translation!