< Yeremia 32 >
1 Hili ndilo neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Bwana, katika mwaka wa kumi wa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, ambao ulikuwa mwaka wa kumi na nane wa utawala wa Mfalme Nebukadneza.
Neno likaja kwa Yeremia kutoka kwa Yahwe katika mwaka wa kumi wa Sedekia mfalme wa Yuda, katika mwaka wa kumi na nane wa Nebukadreza.
2 Wakati huo jeshi la mfalme wa Babeli lilikuwa limeuzunguka mji wa Yerusalemu, naye nabii Yeremia alikuwa amezuiliwa katika ua wa walinzi katika jumba la kifalme la Yuda.
Katika wakati huo, jeshsi la mfalme wa Babeli lilikuwa limeuzunguka Yerusalemu, na Nehemia nabii alikuwwa amefungwa katika uwanja wa walinzi katika nyumba ya mfalme wa Yuda.
3 Basi Sedekia mfalme wa Yuda alikuwa amemfunga huko akisema, “Kwa nini unatabiri hivyo? Wewe unasema, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Ninakaribia kuutia mji huu mkononi mwa mfalme wa Babeli, naye atauteka.
Sedekia mfalme wa Yuda alikuwa amemfunga na kusema, “Kwa nini unatabiri na kusema, 'Yahwe anasema hivi: Angalia, niko karibu kuweka mji huu katika mikono ya mfalme wa Babeli, na atauteka.
4 Sedekia mfalme wa Yuda hataweza kuponyoka mikononi mwa Wakaldayo, lakini kwa hakika atatiwa mikononi mwa mfalme wa Babeli, naye atazungumza naye ana kwa ana na kumwona kwa macho yake mwenyewe.
Sedekia mfalme wa Yuda hatapona kutoka kwenye mikono ya Wakaldayo, kwa maana hakika atatiwa katika mkono wa mfalme wa Babeli. Mdomo wake utazumzia kwenye mdomo wa mfalme, na macho yake yatayaona macho ya mfalme.
5 Atamchukua Sedekia hadi Babeli, mahali atakapoishi mpaka nitakapomshughulikia, asema Bwana. Kama utapigana dhidi ya Wakaldayo, hutashinda.’”
Atampeleka Sedekia Babeli, na atabaki huko hadi nimuadhibu—hili ni tangazo la Yahwe. Ingawa unapigana dhidi ya Wakaldayo, hautafanikiwa.”
6 Yeremia akasema, “Neno la Bwana lilinijia kusema:
Yeremia akasema, “Neno la Yahwe likaja kwangu, likisema, Angalia, Hanameli mwana wa Shalumu mjomba wako anakuja kwako na atasema,
7 Hanameli mwana wa Shalumu mjomba wako atakuja kwako na kusema, ‘Nunua shamba langu huko Anathothi, kwa sababu wewe kama jamaa ya karibu ni haki na wajibu wako kulinunua.’
“Linunue shamba langu ambalo liko katika Anathothi kwa ajili yako, kwa maana haki ya kununua ni yako.””
8 “Kisha, kama Bwana alivyosema, binamu yangu Hanameli alinijia katika ua wa walinzi na kusema: ‘Nunua shamba langu lililoko Anathothi katika nchi ya Benyamini. Kwa kuwa ni haki yako kulikomboa na kulimiliki, jinunulie.’ “Nilijua kwamba hili lilikuwa neno la Bwana.
Kisha, kama Yahwe alivyotangaza, Hanameli, mwana wa mjomba wangu, akaja kwangu katika uwanja wa walinzi, na akasema kwangu, 'Linunue shamba langu kwa ajili yako ambalo liko Anathothi katika nchi ya Benyamini, kwa maana haki ya urithi ni ya kwako, na haki ya kulinunua ni yako. Linunue kwa ajili yako.' Kisha nilijua kuwa hili lilikuwa neno la Yahwe.
9 Hivyo nikalinunua shamba hilo lililoko Anathothi kutoka kwa binamu yangu Hanameli, nami nikampimia shekeli kumi na saba za fedha.
Kwa hiyo nililinua shamba katika Anathothi kutoka kwa Hanameli, mwana wa mjomba wangu, na nilipima fedha kwa ajili yake, shekeli kumi na saba katika uzito.
10 Nikatia sahihi na kuweka muhuri hati ya kumiliki, nikaweka mashahidi, na kupima ile fedha kwenye mizani.
Kisha niliandika katika barua na kuitia muhuri, na kulikuwa na mashadi wakaishuhudia. Kisha nikampa fedha katika mizani.
11 Nikachukua ile hati ya kununulia, nakala iliyotiwa muhuri yenye makubaliano na masharti, pia pamoja na ile nakala isiyo na muhuri,
Kisha nikaichukua hati ya manunuzi ambayo ilikuwa imepigwa muhuri, kwa kuifuata amri na taratibu, na kama ilivyo ada.
12 nami nikampa Baruku mwana wa Neria, mwana wa Maaseya, hati hii mbele ya binamu yangu Hanameli, na mbele ya mashahidi waliokuwa wameweka sahihi kwenye hati hii na mbele ya Wayahudi wote waliokuwa wameketi katika ua wa walinzi.
Ile barua nikampa Baruku mwana wa Neria wa Maaseya mbele ya Hanameli, mwana wa mjomba wangu, na mashahidi waliotia sahihi kwenye barua iliyopigwa muhuri, na mbele ya Wayahudi wote waliokaa katika uwanja wa walinzi.
13 “Nilimpa Baruku maelezo haya mbele yao:
Kwa hiyo nikampa amri Baruku mbele yao. Nilisema,
14 ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Chukua hati hizi, yaani nakala zote zenye muhuri na zisizo na muhuri za hati ya kununulia, na uziweke kwenye gudulia la udongo wa mfinyanzi ili zidumu kwa muda mrefu.
Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Chukua nyaraka hizi, vyote hati hii ya manunuzi iliyopigwa muhuri na nakala zisizopigwa muhuri za manunuzi, na uziweke katika chungu cha udongo ili vidumu kwa muda mrefu.
15 Kwa kuwa hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Nyumba, mashamba na mashamba ya mizabibu yatanunuliwa tena katika nchi hii.’
Kwa maana Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nyumba, mashamba, na mashamba ya mizabibu vitanunuliwa tena katika nchi hii.
16 “Baada ya kumkabidhi Baruku mwana wa Neria hii hati ya kununulia, nilimwomba Bwana:
Baada ya kumpa Baruki mwana wa Neria ile hati ya manunuzi, nikaomba kwa Yahwe nikasema,
17 “Ee Bwana Mwenyezi, umeumba mbingu na nchi kwa uwezo wako mkuu na kwa mkono ulionyooshwa. Hakuna jambo lililo gumu usiloliweza.
Ole, Bwana Yahwe! Angalia! Wewe peke yako umezitengeneza mbingu na dunia kwa nguvu zako kuu na kwa mkono wako ulioinuka. Hakuna kitu ambacho ukisema kwako ni kigumu sana kukifanya.
18 Wewe huonyesha upendo kwa maelfu, lakini huleta adhabu kwa ajili ya dhambi za baba mapajani mwa watoto wao baada yao. Ee Mungu mkuu na mwenye uweza, ambaye jina lako ni Bwana Mwenye Nguvu Zote,
Wewe huonesha agano la uaminifu kwa maelfu na kumimina makosa ya wanadamu katika mapaja ya watoto wao baada yao. Wewe ni Mungu mkuu na mwenye nguvu.
19 makusudi yako ni makuu, na matendo yako ni yenye uwezo. Macho yako yanaona njia zote za wanadamu, nawe humlipa kila mmoja kulingana na mwenendo wake, na kama yanavyostahili matendo yake.
Wewe ni mkuu katika hekima na una nguvu katika matendo, kwa maana macho yako yanaona njia zote za watu, ili kumlipa kila mtu stahiki ya matendo yake.
20 Ulitenda ishara za miujiza na maajabu huko Misri, na umeyaendeleza mpaka leo, katika Israeli na miongoni mwa wanadamu wote, nawe umejulikana na kufahamika hivyo mpaka leo.
Ulifanya ishara na maajabu katika nchi ya Misiri. Hata leo hapa Israeli na kati ya wanadamu wengine wote, umelifanya jina lako kuwa maarufu.
21 Uliwatoa watu wako Israeli kutoka Misri kwa ishara na maajabu, kwa mkono wenye nguvu na ulionyooshwa na kwa matisho makuu.
Kwa maana uliwanunua watu wako Israeli kwa ishira na maajabu, kwa mkono hodari, kwa mkono ulioinuka, na kwa hofu kuu.
22 Uliwapa nchi hii uliyokuwa umeapa kuwapa baba zao, nchi inayotiririka maziwa na asali.
Kisha uliwapa nchi hii—ambayo uliapa kwa babu zao kwamba utawapa—nchi itiririkayo maziwa na asali.
23 Waliingia na kuimiliki, lakini hawakukutii wala kuifuata sheria yako. Hawakufanya kile ulichowaamuru kufanya. Hivyo ukaleta maafa haya yote juu yao.
Hivyo walingia na kuimiliki. Lakini hawakuitii sauti yako wala kuishi kwa kuitii sheria yako. Hawakufanya chochote ulichowaamuru kufanya, kwa hiyo umeleta juu yao majanga haya yote.
24 “Tazama jinsi tumezungukwa na jeshi ili kuuteka mji huu. Kwa sababu ya upanga, njaa na tauni, mji utatiwa mikononi mwa Wakaldayo ambao wanaushambulia. Ulilosema limetokea kama vile unavyoona sasa.
Angalia! Urefu wa maboma haya umefika hadi kwenye mji ili kuuteka. Kwa sababu ya upanga, njaa, na tauni, mji umetiwa kwenye mikono ya Wakaldayo wanaopigana dhidi yake. Kwa maana ulichosema kitatokea sasa kinatokea, na ona, unatazama.
25 Ingawa mji utatiwa mikononi mwa Wakaldayo, wewe, Ee Bwana Mwenyezi, uliniambia, ‘Nunua shamba kwa fedha, na jambo hilo lishuhudiwe.’”
Kisha wewe mwenyewe uliniambia, “Nunua shamba kwa fedha kwa ajili yako na mashahidi wameshuhudia, ingawa mji huu unatiwa mikononi mwa Wakaldayo.””
26 Ndipo neno la Bwana likamjia Yeremia kusema:
Neno la Mungu likaja kwa Yeremia, likisema,
27 “Mimi ndimi Bwana, Mungu wa wote wenye mwili. Je, kuna jambo lolote lililo gumu nisiloliweza?
“Angalia! Mimi ni Yahwe, Mungu wa wanadamu wote. Kuna kitu cho chote kigumu sana kwangu kukifanya?
28 Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Bwana: Ninakaribia kuutia mji huu mikononi mwa Wakaldayo, na mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli ambaye atauteka.
Kwa hiyo Yahwe anasema hivi, 'Ona, niko karibu kuutia mji huu kwenye mikono ya Wakaldayo na Nebukadreza, mfalme wa Babeli. Atauteka.
29 Wakaldayo ambao wanaushambulia mji huu watakuja na kuuchoma moto na kuuteketeza, pamoja na nyumba ambamo watu wamenikasirisha kwa kumfukizia Baali uvumba katika mapaa na kumimina sadaka za vinywaji kwa miungu mingine.
Wakaldayo wanaopigana dhidi ya mji huu watakuja na kuwasha moto kwenye mji huu na kuunguza, pamoja na nyumba juu ya paa la watu waliomwabudu Baali na kumimina dhabihu kwa miungu wengine ili kunikasirisha.
30 “Watu wa Israeli na wa Yuda hawakufanya kitu kingine ila uovu mbele zangu tangu ujana wao. Naam, watu wa Israeli hawakufanya kitu kingine ila kunikasirisha kwa kazi ambazo mikono yao imetengeneza, asema Bwana.
Kwa maana watu wa Israeli na Yuda hakika wamekuwa watu wanaofanya maovu mbele ya macho yangu tangu ujana wao. Watu wa Israeli hakika wameniudhi kwa matendo ya mikono yao—hili ni tangazo la Yahwe.
31 Tangu siku ulipojengwa hadi sasa, mji huu umenikasirisha na kunighadhibisha kiasi kwamba ni lazima niuondoe machoni pangu.
Yahwe anatangaza kwamba mji huu umekuwa sababu ya hasira yangu na ghadhabu yangu tangu siku walipoujenga. Umekuwa hivyo hata leo. Kwa hiyo nitaundoa mbele ya uso wangu
32 Watu wa Israeli na wa Yuda wamenikasirisha kwa uovu wote waliofanya: wao, wafalme wao na maafisa wao, makuhani wao na manabii wao, watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu.
kwa sababu ya uovu wote wa watu wa Israeli na Yuda, mambo waliyofanya ili kunichukiza—wao, wafalme wao, wana wa wafalme, makuhani, manabii, na kila mtu katika Yuda na wakaaji wa Yerusalemu.
33 Walinigeuzia visogo vyao, wala si nyuso zao. Ingawa niliwafundisha tena na tena, hawakupenda kusikiliza wala kuitikia adhabu.
Wamenigeuzia migongo yao badala ya nyuso zao, ingawa niliwafundisha kwa furaha. Nilijitahidi kuwafundisha, lakini hakuna hata mmoja wao aliyenisikiliza ili kupokea marekebisho.
34 Waliweka miungu yao ya kuchukiza sana katika nyumba iitwayo kwa Jina langu na kuinajisi.
Walisimamisha sanamu zao za ajabu katika nyumba inayoitwa kwa jina langu, ili kunitia unajisi.
35 Wakajenga mahali pa juu pa kuabudia miungu kwa ajili ya Baali katika Bonde la Ben-Hinomu, ambapo walitoa wana wao na binti zao kafara kwa Moleki, ingawa kamwe sikuamuru, wala halikuingia akilini mwangu, kwamba watafanya chukizo kama hilo na kumfanya Yuda atende dhambi.
Wakazijenga sehemu za juu katika Bonde la Beni Hinomu ili kuwatia katika moto wana wao na binti zao kwa ajili ya Moleki. Mimi sikuwaagiza. Sikuweka akilini mwangu kamwe kwamba watafanya mambo maovu na kwa hiyo kuwasabisha Yuda watende dhambi.
36 “Mnasema kuhusu mji huu, ‘Kwa upanga, njaa na tauni, mji utatiwa mkononi mwa mfalme wa Babeli,’ lakini hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli asemalo:
Kwa hiyo sasa, Mimi, Yahwe, Mungu wa Israeli, kuhusu mji huu ninasema hivi, 'mji ambao mnasema, 'Umetiwa mikononi mwa mfalme wa Babeli kwa upanga, njaa, na pigo.'
37 Hakika nitawakusanya kutoka nchi zote nilizowafukuzia katika hasira yangu kali na ghadhabu yangu kuu, nitawarudisha mahali hapa na kuwaruhusu waishi kwa salama.
Ona, niko karibu kuwakusanya kutoka kila nchi nilikowapeleka katika hasira yangu, ghadhabu, hasira kuu. Niko karibu kuwarudisha kwenye sehemu hii na kuwawezesha kuishi katika usalama.
38 Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
Kisha watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.
39 Nitawapa moyo mmoja na kutenda pamoja, ili kwamba waniche daima kwa mema yao wenyewe na kwa mema ya watoto wao baada yao.
Nitawapa moyo mmjoa na na njia moja ya kuniheshimu kila siku ili kwamba yawepo mema kwa ajili yao na uzao wao baada yao.
40 Nitafanya nao agano la milele: Kamwe sitaacha kuwatendea mema, nami nitawavuvia kunicha mimi, ili kamwe wasigeukie mbali nami.
Kisha nitafanya pamoja nao agano la milele, ili nisiache kufanya mema kwa ajili yao. nitajiwekea heshima katika mioyo yao, ili kwamba wasiniache.
41 Nitafurahia kuwatendea mema, na kwa hakika nitawapanda katika nchi hii kwa moyo wangu wote na roho yangu yote.
Kisha nitajifurahisha katika kufanya mema kwao. Kwa uaminifu nitawapanda katika anchi hii kwa moyo wangu wote na maisha yangu yoye.
42 “Hili ndilo asemalo Bwana: Kama nilivyoleta maafa haya makubwa kwa watu hawa, ndivyo nitakavyowapa mafanikio niliyowaahidi.
Kwa amaana Yahwe anasema hivi, 'Kama tu nilivyoyaleta majanga haya makubwa yote juu ya watu hawa, hivyo hivyo nitaleta juu yao mambo mema niliyosema kwamba nitafanya kwa ajili yao.
43 Kwa mara nyingine tena mashamba yatanunuliwa katika nchi hii ambayo mlisema, ‘Imekuwa ukiwa, isiyofaa, isiyo na watu wala wanyama, kwa sababu imetiwa mikononi mwa Wakaldayo.’
Basi mashamba yatanunuliwa katika nchi hii, ambayo mnaisema, “Hii ni nchi iliyoharibiwa, isiyo na mwanadamu wala mnyama. Imetiwa mikononi mwa Wakaldayo”
44 Mashamba yatanunuliwa kwa fedha, na hati zitatiwa sahihi, zitatiwa muhuri na kushuhudiwa katika nchi ya Benyamini, katika vijiji vinavyoizunguka Yerusalemu, katika miji ya Yuda na katika miji ya nchi ya vilima, sehemu za magharibi katika miji ya tambarare na katika Negebu, kwa sababu nitarudisha tena mafanikio yao, asema Bwana.”
Watanunua mashamba kwa fedha na kuandika katika barua zilizopigwa muhuri. Watawakusanya mashahidi katika nchi ya Benyamini, wote kuzunguka Yerusalemu na miji ya Yuda katika miji ya nchi yenye vilima, na katika nchi tambarare, na katika miji ya Negebu. Kwa maana nitawarejesha wafungwa wao—hili ni tangazo la Yahwe.”'