< Maombolezo 1 >
1 Tazama jinsi mji ulivyoachwa ukiwa, mji ambao zamani ulikuwa umejaa watu! Jinsi ambavyo umekuwa kama mama mjane, ambaye wakati fulani alikuwa maarufu miongoni mwa mataifa! Yule ambaye alikuwa malkia miongoni mwa majimbo sasa amekuwa mtumwa.
Mji ambao mwanzo ulikuwa na watu wengi sasa umekaa peke yake. Amekuwa kama mjane, japo alikuwa taifa kubwa. Alikuwa mtoto wa mfalme miongoni mwa mataifa, lakini sasa amelazimishwa utumwani.
2 Kwa uchungu, hulia sana usiku, machozi yapo kwenye mashavu yake. Miongoni mwa wapenzi wake wote hakuna yeyote wa kumfariji. Rafiki zake wote wamemsaliti, wamekuwa adui zake.
Analia na kuomboleza usiku, na machozi yake yanafunika mashavu yake. Hamna ata mpenzi wake anaye mliwaza. Marafiki wake wote wamemsaliti. wamekuwa maadui wake.
3 Baada ya mateso na kufanyishwa kazi kikatili, Yuda amekwenda uhamishoni. Anakaa miongoni mwa mataifa, hapati mahali pa kupumzika. Wote ambao wanamsaka wamemkamata katikati ya dhiki yake.
Baada ya umaskini na mateso, Yuda ameenda matekani. Anaishi miongoni mwa mataifa na hapati pumziko lolote. Wanao wakimbiza wamewapata katika upweke wake.
4 Barabara zielekeazo Sayuni zaomboleza, kwa kuwa hakuna yeyote anayekuja kwenye sikukuu zake zilizoamriwa. Malango yake yote yamekuwa ukiwa, makuhani wake wanalia kwa uchungu, wanawali wake wanahuzunika, naye yuko katika uchungu wa maumivu makuu.
Barabara za Sayuni zinaomboleza kwasababu hakuna anaye kuja kwenye sherehe iliyo andaliwa. Malango yake yote ni ukiwa. Makuhani wake wote wana sononeka. Mabikra wake wana uzuni na yeye mwenyewe yupo katika ugumu.
5 Adui zake wamekuwa mabwana zake, watesi wake wana raha. Bwana amemletea huzuni kwa sababu ya dhambi zake nyingi. Watoto wake wamekwenda uhamishoni, mateka mbele ya adui.
Maadui wake wamekuwa bwana zake; maadui wake wana fanikiwa. Yahweh amemuadhibu kwa dhambi zake nyingi. Watoto wake wadogo wanaenda matekani kwa maadui zake.
6 Fahari yote imeondoka kutoka kwa Binti Sayuni. Wakuu wake wako kama ayala ambaye hapati malisho, katika udhaifu wamekimbia mbele ya anayewasaka.
Uzuri umemwacha binti wa Sayuni. Watoto wa mfalme wamekuwa kama ayala ambaye haoni malisho, na wanaenda bila uwezo kwa wanao wakimbiza.
7 Katika siku za mateso yake na kutangatanga, Yerusalemu hukumbuka hazina zote ambazo zilikuwa zake siku za kale. Wakati watu wake walipoanguka katika mikono ya adui, hapakuwepo na yeyote wa kumsaidia. Watesi wake walimtazama na kumcheka katika maangamizi yake.
Katika siku za mateso yake na kutokuwa na nyumba, Yerusalemu itakumbuka hazina zake za dhamani alizo kuwa nazo awali. Wakati watu wake walipo angukia mikononi mwa adui, hakuna aliye msaidia. Maadui waliwaona na kucheka maangamizo yake.
8 Yerusalemu ametenda dhambi sana kwa hiyo amekuwa najisi. Wote waliomheshimu wanamdharau, kwa maana wameuona uchi wake. Yeye mwenyewe anapiga kite na kugeukia mbali.
Yerusalemu ili tenda dhambi sana, hivyo basi, amedhalillika kama kitu kichafu. Wote walio mheshimu sasa wana mdharau kwa kuwa wameona uchi wake. Anasononeka na kujaribu kugeuka pembeni.
9 Uchafu wake umegandamana na nguo zake; hakuwaza juu ya maisha yake ya baadaye. Anguko lake lilikuwa la kushangaza, hapakuwepo na yeyote wa kumfariji. “Tazama, Ee Bwana, teso langu, kwa maana adui ameshinda.”
Amekuwa mchafu chini ya sketi yake. Hakuwaza hatima yake. Anguko lake lilikuwa baya. Hakukuwa na wakumliwaza. Alilia, “Angalia mateso yangu, Yahweh, kwa kuwa adui amekuwa mkuu sana.”
10 Adui ametia mikono juu ya hazina zake zote, aliona mataifa ya kipagani wakiingia mahali patakatifu pake, wale uliowakataza kuingia kwenye kusanyiko lako.
Adui ameeka mkono wake kwenye hazina zetu za dhamani. Ameona mataifa yakiingia sehemu yake takatifu, japo uliamuru wasiingie katika sehemu yako ya kukusanyikia.
11 Watu wake wote wanalia kwa uchungu watafutapo chakula; wanabadilisha hazina zao kwa chakula ili waweze kuendelea kuishi. “Tazama, Ee Bwana, ufikiri, kwa maana nimedharauliwa.”
Watu wote wana sononeka wanapo tafuta mkate. Wametoa hazina zao za dhamani kwa ajili ya chakula cha kurejesha uhai wao. Tazama, Yahweh, ni kumbuke mimi, kwa kuwa nimekuwa sina faida.
12 “Je, si kitu kwenu, ninyi nyote mpitao kando? Angalieni kote mwone. Je, kuna maumivu kama maumivu yangu yale yaliyotiwa juu yangu, yale Bwana aliyoyaleta juu yangu katika siku ya hasira yake kali?
Sio kitu kwako, wote mnao pita? Angalia na uone kama kuna mtu mwenye uzuni kama uzuni ninao teswa nao, tangu Yahweh amenitesa mimi katika siku ya hasira yake kali.
13 “Kutoka juu alipeleka moto, akaushusha katika mifupa yangu. Aliitandia wavu miguu yangu na akanirudisha nyuma. Akanifanya mkiwa, na mdhaifu mchana kutwa.
Ni kutoka juu ndipo alipo tuma moto kwenye mifupa yangu na umenishinda. Ametanda nyavu kwa miguu yangu na kunigeuza. Amenifanya ukiwa na dhahifu.
14 “Dhambi zangu zimefungwa kwenye nira, kwa mikono yake zilifumwa pamoja. Zimefika shingoni mwangu na Bwana ameziondoa nguvu zangu. Amenitia mikononi mwa wale ambao siwezi kushindana nao.
Nira ya makosa yangu imefungwa na mikono yake. Zimesokotwa na kuekwa shingoni mwangu. Amefanya uweza wangu kushindwa. Bwana amenikabidhi mikononi mwa, na siwezi kusimama.
15 “Bwana amewakataa wapiganaji wa vita wote walio kati yangu, ameagiza jeshi dhidi yangu kuwaponda vijana wangu wa kiume. Katika shinikizo lake la divai Bwana amemkanyaga Bikira Binti Yuda.
Bwana ametupa pembeni wanaume wangu hodari walio niokoa. Ameitisha kusanyiko dhidi yangu kuponda wanaume wangu imara. Bwana amewakanyaga binti bikra wa Yuda kwenye chombo cha kusagia mvinyo.
16 “Hii ndiyo sababu ninalia na macho yangu yanafurika machozi. Hakuna yeyote aliye karibu kunifariji, hakuna yeyote wa kuhuisha roho yangu. Watoto wangu ni wakiwa kwa sababu adui ameshinda.”
Kwa vitu hivi ninalia. Macho yangu, maji yanashuka chini ya macho yangu tangu mfariji aliye paswa kurejesha maisha yangu yuko mbali na mimi. Watoto wangu wamekuwa ukiwa kwasababu adui yangu ameshinda.
17 Sayuni ananyoosha mikono yake, lakini hakuna yeyote wa kumfariji. Bwana ametoa amri kwa ajili ya Yakobo kwamba majirani zake wawe adui zake; Yerusalemu umekuwa kitu najisi miongoni mwao.
Sayuni ametandaza mikono yake; hakuna wakuwa mliwaza. Yahweh ameamuru hao karibu na Yakobo wawemaadui wake. Yerusalemu ni kitu kichafu kwao.
18 “Bwana ni mwenye haki, hata hivyo niliasi dhidi ya amri yake. Sikilizeni, enyi mataifa yote, tazameni maumivu yangu. Wavulana wangu na wasichana wangu wamekwenda uhamishoni.
Yahweh ni mwenye haki, kwa kuwa nimeasi dhidi ya amri zake. Sikia, ninyi watu, na muone uzuni wangu. Mabikra wangu na wanaume imara wameenda matekani.
19 “Niliita washirika wangu lakini walinisaliti. Makuhani wangu na wazee wangu waliangamia mjini walipokuwa wakitafuta chakula ili waweze kuishi.
Niliita marafiki zangu, lakini walikuwa na hila kwangu. Makuhani wangu na wazee waliangamia kwenye mji, walipo kuwa wanatafuta chakula cha kurejesha uhai wao.
20 “Angalia, Ee Bwana, jinsi nilivyo katika dhiki! Nina maumivu makali ndani yangu, nami ninahangaika moyoni mwangu, kwa kuwa nimekuwa mwasi sana. Huko nje, upanga unaua watu, ndani, kipo kifo tu.
Tazama, Yahweh, kwa kuwa nipo kwenye ugumu; tumbo langu lina nguruma, moyo wangu umetibuka ndani yangu, kwa kuwa nimekuwa muasi sana. Nje, upanga umemliza mama, ndani ya nyumba kuna mauti tu.
21 “Watu wamesikia ninavyolia kwa uchungu, lakini hakuna yeyote wa kunifariji. Adui zangu wote wamesikia juu ya dhiki yangu, wanafurahia lile ulilolitenda. Naomba uilete siku uliyoitangaza ili wawe kama mimi.
Wamesikia sononeko langu, lakini hakuna wakuni liwaza. Maadui zangu wote wamesikia shida zangu na wamefurahi umenifanyia hivi. Umeleta siku uliyo ahidi; sasa acha wawe kama mimi.
22 “Uovu wao wote na uje mbele zako; uwashughulikie wao kama vile ulivyonishughulikia mimi kwa sababu ya dhambi zangu zote. Kulia kwangu kwa uchungu ni kwingi na moyo wangu umedhoofika.”
Acha uovu wote uje mbele zako. Shughulika nao kama ulivyo shughulika na mimi kwasababu ya makosa yangu yote. Masononeko yangu ni mengi na moyo umezimia.