< Ezekieli 18 >
1 Neno la Bwana likanijia kusema:
Neno la Yahwe likanijia tena, kusema,
2 “Je, ninyi watu mna maana gani kutumia mithali hii inayohusu nchi ya Israeli: “‘Baba wamekula zabibu zenye chachu, nayo meno ya watoto yametiwa ganzi’?
“Je mnamaana gani, ninyi mliotumia hii mithali kuhusiana na nchi ya Israeli na kusema, 'Wababa wamekula zabibu mbichi, na meno ya watoto imetiwa ganzi'?
3 “Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, hamtatumia tena mithali hii katika Israeli.
Kama nishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-bila shaka hakutakuwa na fursa yoyote tena kwa ajili yenu kuitumia hii mithali katika Israeli.
4 Kwa kuwa kila roho ni mali yangu, kama vile ilivyo roho ya baba, vivyo hivyo roho ya mtoto ni mali yangu. Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa.
Tazama! Kila uhai ni mali yangu-uhai wa baba na uhai wa mwana pia, ni mali yangu! roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa!
5 “Mtu aweza kuwa ni mwenye haki atendaye yaliyo haki na sawa.
Itasemwaje kuhusu mtu mwenye haki na achukuaye yaliyo halali na haki-
6 Hakula katika mahali pa ibada za miungu kwenye milima wala hakuziinulia macho sanamu za nyumba ya Israeli. Hakumtia unajisi mke wa jirani yake, wala hakukutana kimwili na mwanamke wakati wa siku zake za hedhi.
kama asipokula juu ya milima au kuinua macho yake kwa sananmu za nyumba ya Israeli, na hakumnajisi mke wa jirani yake, wala kumsemesha mwanamke katika kipindi chake cha mwezi, je! Yu mwenye haki?
7 Hamwonei mtu yeyote, bali hurudisha kilichowekwa rehani kwake. Hanyangʼanyi, bali huwapa wenye njaa chakula chake na huwapa nguo walio uchi.
Je! Itasemwaje kuhusu mtu ambaye hakumkandamiza yeyote, na kumrudisha mdeni wake kwa kile kilichokuwa kimewekwa kwa ajili ya rehani, na hakuiba lakini kuwapatia chakula wenye njaa na kuwafunika uchi kwa nguo, je yu mwenye haki?
8 Hakopeshi kwa riba wala hajipatii faida ya ziada. Huuzuia mkono wake usifanye mabaya, naye huhukumu kwa haki kati ya mtu na mtu.
Je! Itasemwaje kuhusu mtu ambaye hakuchukua faida kubwa kwa ile pesa aliyokopa, na hakuchukua faida kubwa kwa kile alichokiuza?
9 Huzifuata amri zangu na kuzishika sheria zangu kwa uaminifu. Huyo mtu ni mwenye haki; hakika ataishi, asema Bwana Mwenyezi.
Amesemwa kwamba amechukua yaliyo halali na kuimarisha uaminifu kati ya watu. Kama huyo mtu akitembea katika sheria zangu na kuzishika hukumu zangu kufanya kwa uaminifu, kisha ahadi kwa ajili ya mtu mwenye haki ni hii: Ataishi hakika! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
10 “Aweza kuwa ana mwana jeuri, amwagaye damu au atendaye mojawapo ya mambo haya
Lakini akizaa mwana mnyang'anyi mmwaga damu na kufanya mengi katika haya mambo kama yalivyotajwa hapa,
11 (ingawa baba yake hakufanya mojawapo ya haya): “Hula katika mahali pa ibada za miungu kwenye milima. Humtia unajisi mke wa jirani yake.
hata kama baba yake hakufanya mojawapo katika haya mambo, lakini akala juu ya milima na akamnajisi mke wa jirani yake, Je! itasemwaje juu yake?
12 Huwaonea maskini na wahitaji. Hunyangʼanyana. Harudishi kile kilichowekwa rehani kwake. Huziinulia sanamu macho. Hufanya mambo ya machukizo.
Huyu mtu huwakandamiza maskini na wahitaji, na huwakamata na kuwanyang'anya, na hawarudishii dhamana, na huyanua macho yake kwa sanamu na kufanya matendo maovu,
13 Hukopesha kwa riba na kutafuta faida ya ziada. Je, mtu wa namna hii ataishi? Hapana, hataishi! Kwa sababu amefanya mambo haya yote ya machukizo, hakika atauawa na damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe.
na hukopesha pesa kwa faida ya juu sana na kufanya faida kubwa juu ya anachokiuza, Je! huyo mtu ataishi? Hakika hataishi! Atakufa hakika na damu yake itakuwa juu yake kwa sababu amefanya haya mambo ya chuki.
14 “Lakini yawezekana mwana huyo ana mwana aonaye dhambi hizi zote anazofanya baba yake, naye ingawa anaziona, yeye hafanyi mabaya kama haya:
Lakini Tazama! tuseme kuna mtu aliyezaa mwana, na mwana wake huona dhambi zote za baba yake alizozifanya, na kupitia kuziona, hakuyafanya hayo mambo.
15 “Hakula katika mahali pa ibada za miungu kwenye milima, wala hainulii macho sanamu za nyumba ya Israeli. Hakumtia unajisi mke wa jirani yake.
Huyo mwana hakula juu ya milima, na hakuinua macho yake kwa sanamu za nyumba ya Israeli, na hakumtia unajisi mke wa jirani yake, Je! itasemwaje juu yake?
16 Hakumwonea mtu yeyote wala hakutaka rehani kwa ajili ya mkopo. Hanyangʼanyi, bali huwapa wenye njaa chakula chake na huwapa nguo walio uchi.
Yule mwana hakumkandamiza yeyote, au kutwaa dhamana, au kupoteza vitu, lakini badala yake kutoa chakula chake kwa wenye njaa na kuwafunika wenye uchi kwa nguo.
17 Huuzuia mkono wake usitende dhambi, hakopeshi kwa riba wala hajipatii faida ya ziada. Huzishika amri zangu na kuzifuata sheria zangu. Hatakufa kwa ajili ya dhambi za baba yake; hakika ataishi.
Huyo mwana hakumkandamiza yeyote au au kuchukua faida ambayo ni ya juu sana au kufanya manufaa kwa ajili ya mkopo, lakini ameyashika maagizo yangu na kuenenda sawa sawa na sheria zangu; huyo mwana hatakufa kwa ajili ya dhambi za baba yake: Ataishi hakika!
18 Lakini baba yake atakufa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe, kwa sababu alitoza bei isiyo halali kwa nguvu, akamnyangʼanya ndugu yake na kufanya yaliyo mabaya miongoni mwa watu wake.
Baba yake, kwa kuwa aliwakandamiza wengine kwa nguvu nyingi na kumnyang'anya ndugu yake, na kufanya yasiyo mema miongoni mwa watu wake-tazama, atakufa katika uovu wake.
19 “Lakini mnauliza, ‘Kwa nini mwana asiadhibiwe kwa uovu wa baba yake?’ Kwa vile mwana ametenda yaliyo haki na sawa na amekuwa mwangalifu kuzishika amri zangu zote, hakika ataishi.
Lakini ninyi husema, 'Kwa nini mwana asibebe uovu wa baba yake?' Kwa sababu mwana hubeba yaliyo halali na haki na kuzitunza amri zangu; huzifanya. Ataishi hakika!
20 Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa. Mwana hataadhibiwa kwa ajili ya makosa ya baba yake, wala baba hataadhibiwa kwa ajili ya makosa ya mwanawe. Haki ya mtu mwenye haki itahesabiwa juu yake na uovu wa mtu mwovu utalipizwa juu yake.
Yule atendaye dhambi, ndiye ambaye atakufa. Mwana hatabeba uovu wa baba yake, na baba hatabeba uovu wa mwana wake. Haki ya yule atendaye haki itakuwa juu yakwe mwenyewe, na uovu wa mwenye uovu utakuwa juu yake mwenyewe.
21 “Lakini mtu mwovu akiacha dhambi zake zote alizozitenda na kushika amri zangu zote na kufanya lililo haki na sawa, hakika ataishi, hatakufa.
Lakini kama mwovu ageukapo kutoka dhambi zake zote alizofanya, na kuzitunza sheria zangu zote na kufanya yaliyo halali na haki, kisha hakika ataishi na hatakufa.
22 Hakuna kosa lolote alilotenda litakalokumbukwa juu yake. Kwa ajili ya mambo ya haki aliyoyatenda, ataishi.
Makosa yote aliyoyafanya hayatakumbukwa juu yake. Ataishi kwa hiyo haki aliyoitenda.
23 Je, mimi ninafurahia kifo cha mtu mwovu? Asema Bwana Mwenyezi. Je, si mimi ninafurahi wanapogeuka kutoka njia zao mbaya na kuishi?
Je! Nitafurahia juu ya kifo cha mwovu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-na sio katika kugeuka kwake kutoka njia yake ili kwamba aweze kuishi?
24 “Lakini kama mtu mwenye haki akiacha haki yake na kutenda dhambi na kufanya mambo ya machukizo ambayo mtu mwovu hufanya, Je, ataishi? Hakuna hata mojawapo ya matendo ya haki aliyotenda litakalokumbukwa. Kwa sababu ya kukosa uaminifu kwake anayo hatia na kwa sababu ya dhambi alizozitenda, atakufa.
Lakini kama mtu mwenye haki ageukapo kutoka kwenye haki yake na kufanya maovu na kutenda machukizo kama machukizo yote ambayo mtu mwovu afanyayo, basi ataishi? Haki yake yote aliyoifanya haitakumbukwa wakati atakaponisaliti katika uhaini wake. Hivyo atakufa katika dhambi alizofanya.
25 “Lakini mnasema, ‘Njia ya Bwana si ya haki.’ Sikia, ee nyumba ya Israeli: Njia yangu siyo iliyo ya haki? Je, si njia zenu ndizo ambazo si za haki?
Lakini ninyi husema, 'Njia ya Bwana si sawa!' sikilizeni, nyumba ya Israeli! Je njia zangu haziko sawa? Je si njia ambazo haziko sawa?
26 Kama mtu mwenye haki akiacha haki yake na kutenda dhambi, atakufa kwa ajili ya dhambi yake, kwa sababu ya dhambi alizotenda, atakufa.
Wakati mtu mwenye haki ageukapo kutoka kwenye makosa yake, na kufanya maovu na kufa kwa sababu ya hayo, kisha atakufa katika uovu ambao alioufanya.
27 Lakini mtu mwovu akigeuka kutoka maovu aliyoyatenda na kufanya yaliyo haki na sawa, ataokoa maisha yake.
Lakini wakati mtu mwovu ageukapo kutoka uovu wake alioufanya na kufanya yaliyo halali na haki, kisha ataulinda uhai wake.
28 Kwa kuwa anayafikiria na kugeuka kutoka makosa yake yote aliyoyatenda na kuyaacha, hakika ataishi, hatakufa.
Kwa kuwa ameona na kugeuka kutokana na makosa yake yote ambayo aliyoyafanya. Hakika ataishi, na hatakufa.
29 Lakini nyumba ya Israeli inasema, ‘Njia za Bwana si haki.’ Je, njia zangu si za haki, ee nyumba ya Israeli? Je, si njia zenu ndizo ambazo si za haki?”
Lakini nyumba ya Israeli husema, 'Njia ya Bwana haiko sawa!' Ni namna gani njia zangu si sawa, nyumba ya Israeli? Ni njia zenu ndizo si sawa.
30 “Kwa hiyo, ee nyumba ya Israeli, nitawahukumu, kila mmoja sawasawa na njia zake, asema Bwana Mwenyezi. Tubuni! Geukeni kutoka makosa yenu yote, ndipo dhambi haitakuwa anguko lenu.
Kwa hiyo nitamuhukumu kila mtu miongoni mwenu kulingana na njia zake, nyumba ya Israeli! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo. Tubuni na rudini kutoka kwenye makosa yenu yote ili kwamba wasiwe kikwazo cha uovu dhidi yenu.
31 Tupilieni mbali makosa yenu yote mliyoyatenda, nanyi mpate moyo mpya na roho mpya. Kwa nini mfe, ee nyumba ya Israeli?
Tupilia mbali makosa yenu yote mliyoyafanya; jifanyieni moyo mpya na roho mpya. Kwa nini mfe, nyumba ya Israeli?
32 Kwa maana sifurahii kifo cha mtu awaye yote afaye katika uovu, asema Bwana Mwenyezi. Tubuni basi, mkaishi!
Kwa kuwa sifurahii kifo cha yule afaye-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-hivyo tubuni na muishi!”