< Ezekieli 17 >
1 Neno la Bwana likanijia kusema:
Neno la Yahwe likanijia, kusema,
2 “Mwanadamu, tega kitendawili, ukawaambie nyumba ya Israeli fumbo.
“Mwanadamu, tega kitendawili na sema fumbo kwa nyumba ya Israeli.
3 Waambie hivi, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Tai mkubwa mwenye mabawa yenye nguvu, yaliyojaa manyoya marefu ya rangi mbalimbali, alikuja Lebanoni. Akatua kwenye kilele cha mwerezi,
Sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tai mkubwa pamoja na mabawa makubwa na vipapatio virefu, mwenye kujaa manyoya, na aliyekuwa na rangi nyingi alienda Lebanoni na kuchukua kilele cha mti wa mkangazi.
4 akakwanyua ncha yake na kuichukua mpaka nchi ya wafanyabiashara, akaipanda huko katika mji wa wachuuzi.
Akakata ncha za matawi na kuzichukua hata nchi ya Kanaani; akaipanda katika mji wa manahodha.
5 “‘Akachukua baadhi ya mbegu za nchi yako na kuziweka katika udongo wenye rutuba. Akazipanda kama mti umeao kando ya maji mengi,
Pia akachukua mbegu ya nchi na kuipanda katika udongo wenye rutuba. Akaiweka kando ya maji mengi kama mti umeao karibu na maji.
6 nazo zikaota na kuwa mzabibu mfupi, unaoeneza matawi yake. Matawi yake yakamwelekea huyo tai, mizizi yake ikabaki chini ya huo mzabibu. Kwa hiyo ukawa mzabibu na kutoa matawi na vitawi vyenye majani mengi.
Kisha ukachipusha na mzabibu wenye kusambaa chini kwenye aridhi. Matawi yake yakamwelekea yeye, na mizizi yake ikakua chini yake. Hivyo ukawa mzabibu na kuzaa matawi na kutoa matawi.
7 “‘Lakini kulikuwa na tai mwingine mkubwa, mwenye mabawa yenye nguvu yaliyojaa manyoya. Tazama! Huu mzabibu ukatoa mizizi yake kumwelekea huyo tai kutoka mle kwenye shamba lile ulikopandwa na kutanda matawi yake kumwelekea kwa ajili ya kupata maji.
Lakini kulikuwa na tai mwingine mkubwa wenye mabawa makubwa na manyoya mengi. Tazama! Huu mzabibu ukabadilisha mizizi yake kumwelekea tai, na ukasamabaza matawi yake kumwelekea tai kutoka mahali ulipokuwa umepandwa basi upate kumwagiliwa.
8 Ulikuwa umepandwa katika udongo mzuri wenye maji mengi ili uweze kutoa matawi, kuzaa matunda na uweze kuwa mzabibu mzuri sana.’
Ulikuwa umepandwa kwenye udongo mzuri kando ya maji mengi hivyo ungezaa matawi na kuanza kutoa matunda, ili kuwa mzabibu mzuri kabisa.'
9 “Waambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Je, utastawi? Je, hautangʼolewa na kuondolewa matunda yake, ili uweze kunyauka? Majani yake mapya yanayochipua yote yatanyauka. Hautahitaji mkono wenye nguvu au watu wengi kuungʼoa na mizizi yake.
Waambie watu, 'Bwana Yahwe asema hivi: Je! huo utafanikiwa? Je! Haitaing'oa mizizi yake na kuyakata matunda yake ili kwamba unyauke, na majani yake yote mabichi yanyauke? Hakuna jeshi imara au watu wengi watahitajika kuivuta kwa mizizi yake.
10 Hata kama utapandwa pengine, Je, utastawi? Je, hautanyauka kabisa wakati upepo wa mashariki utakapoupiga, yaani, hautanyauka kabisa katika udongo mzuri ambamo ulikuwa umestawi vizuri?’”
Basi tazama! Baada ya kuwa umepandwa, je utakuwa? Je hautanyauka wakati upepo wa mashariki utakapoupiga? Utanyauka kabisa katika kiwanja chake.”'
11 Ndipo neno la Bwana likanijia kusema:
Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
12 “Waambie nyumba hii ya kuasi, ‘Je, mnajua hii ina maana gani?’ Waambie: ‘Mfalme wa Babeli alikwenda Yerusalemu na kumchukua mfalme na watu maarufu, akarudi nao na kuwaleta mpaka Babeli.
“Waambie nyumba ya uasi, 'Je! hamjui haya mambo yana gana gani? Tazama! Mfalme wa Babeli amekuja Yerusalemu na kumchukua mfalme wake na wakuu wake na kuwaleta kwake mpaka Babebli.
13 Ndipo akamchukua mmoja wa jamaa ya mfalme na kufanya mapatano naye, akamfanya aape. Akawachukua pia viongozi wa nchi,
Kisha akauchukua ukoo wa kifalme, akafanya agano pamoja naye, na kumleta chini ya kiapo. Akawachukua watu wa nchi wenye nguvu,
14 ili kuudhoofisha ufalme huo, usiweze kuinuka tena, ila uweze kuendelea tu chini ya mapatano yake.
basi ufalme uwe duni na usijiinue wenyewe. Kwa kulitunza agano lake nchi itaokoka.
15 Lakini mfalme aliasi dhidi yake kwa kutuma wajumbe wake kwenda Misri ili kupatiwa farasi na jeshi kubwa. Je, atashinda? Je, atafanikiwa? Je, mtu afanyaye mambo kama hayo ataokoka? Je, atavunja mapatano na bado aokoke?
Lakini mfalme wa Yerusalemu ameasi juu yake kwa kupeleka mabalozi kwenda Misri ili kujipatia farasi na jeshi. Je! Atafanikiwa? Je! yeye anayeyafanya haya mambo ataokoka?
16 “‘Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, atafia huko Babeli, katika nchi ya mfalme aliyemketisha katika kiti cha enzi, ambaye alidharau kiapo chake na kuvunja mapatano yake.
Kama niishivyo! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-atakufa hakika katika nchi ya mfalme aliyemfanya mfalme, yule mfalme ambaye aliyekidharau kiapo chake, na ambaye aliyevunja agano lake. atakufa kati ya Babeli.
17 Farao na jeshi lake kubwa, na wingi wake wa watu hawataweza kusaidia chochote katika vita, wakati watakapozungukwa na jeshi ili kukatilia mbali maisha ya watu wengi.
Farao na jeshi lake lenye nguvu na kusanyiko la watu wengi kwa ajili ya vita hawatamlinda katika vita, wakati jeshi la Wababeli watakapojenga tuta la ngome na kuta za ngome ili kuyaharibu maisha ya wengi.
18 Alidharau kiapo kwa kuvunja Agano. Kwa sababu aliahidi kwa mkono wake mwenyewe na bado akafanya mambo haya yote, hataokoka.
Kwa kuwa mfalme amedharau kiapo chake kwa kulivunja agano. Tazama, ameunyoosha kwa mkono wake ili kufanya ahadi na bado ameyafanya haya mambo yote. Hataokoka.
19 “‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Hakika kama niishivyo, nitaleta juu ya kichwa chake kiapo changu, alichokidharau na Agano langu lile alilolivunja.
Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Kama niishivyo, Je! hiki hakikuwa kiapo changu kwamba alidharau agano langu alilo livunja? Basi nitaleta nitamwadhibu juu ya kichwa chake!
20 Nitautandaza wavu wangu kwa ajili yake, naye atanaswa katika mtego wangu. Nitamleta mpaka Babeli na kutekeleza hukumu juu yake huko kwa kuwa hakuwa mwaminifu kwangu.
Nitausambaza wavu wangu juu yake, na atanaswa katika wavu wangu wa kutegea. Kisha nitamleta hata Babeli na kuzitekeleza hukumu juu yake huko kwa ajili ya uhaini wake alioufanya amenisaliti!
21 Askari wake wote wanaotoroka wataanguka kwa upanga, nao watakaonusurika watatawanyika katika pande zote za dunia. Ndipo utakapojua kuwa Mimi Bwana nimesema.
Wakimbizi wake wote katika majeshi yake yataanguka kwa upanga, na wale watakaobakia watatawanyika kila mahali. Kisha utajua yakwamba mimi ni Yahwe; nimesema hili litatokea.”
22 “‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi mwenyewe nitachukua chipukizi kutoka kwenye kilele cha juu sana cha mwerezi na kukipanda, nitavunja kitawi kichanga kutoka matawi yake ya juu kabisa na kukipanda juu ya mlima mrefu ulioinuka sana.
Bwana Yahwe asema hivi, 'Basi mimi mwenyewe nitaichukua sehemu ya juu ya mti wa mkangazi, na nitaupanda mbali na matawi yake laini. Nitaukata, na mimi mwenyewe nitaupanda juu ya mlima mrefu.
23 Katika vilele vya mlima mrefu wa Israeli nitakipanda, kitatoa matawi na kuzaa matunda na kuwa mwerezi mzuri sana. Ndege wa kila aina wataweka viota vyao ndani yake, nao watapata makazi katika kivuli cha matawi yake.
Nitaupanda juu ya milima ya Israeli hivyo utazaa matawi na kuzaa matunda, na utakuwa mkangazi wa fahari ili kwamba kila ndege arukaye ataishi chini ya huo. Watajenga viota chini ya kivuli cha matawi yake.
24 Miti yote ya kondeni itajua kuwa Mimi Bwana ninaishusha miti mirefu na kuikuza miti mifupi kuwa miti mirefu. Mimi naikausha miti mibichi na kuifanya miti mikavu istawi. “‘Mimi Bwana nimesema, nami nitatenda.’”
Kisha miti yote ya shambani itajua kwamba mimi ni Yahwe. Nimeishusha miti mirefu na nimeiinua juu miti mifupi. Naunyausha mti mbichi na kuufanya mti mkavu kuchanua. Mimi Yahwe, nimesema hivyo hii itatokea; nami nimelifanya hili.'”