< Kutoka 9 >

1 Ndipo Bwana akamwambia Mose, “Nenda kwa Farao ukamwambie, ‘Hili ndilo Bwana, Mungu wa Waebrania asemalo: “Waachie watu wangu waende ili wapate kuniabudu.”
Kisha Yahweh akamwambia Musa, Nenda kwa Farao na umwambie, 'Yahweh, Mungu wa Waebrania, anasema hivi: “Acha watu wangu waende ili wakaniabudu mimi.”
2 Kama ukikataa kuwaachia waende, nawe ukiendelea kuwashikilia,
Lakini ukikataa kuwaruhusu waende, kama utaendelea kuwa bakiza nyuma,
3 mkono wa Bwana utaleta pigo baya kwa mifugo yako, juu ya farasi wako, punda, ngamia, ngʼombe wako, kondoo na mbuzi.
basi mkono wa Yahweh utakuwa kinyume dhidi ya mifugo yako shambani na kwa farasi, punda, ngamia, ng'ombe na kondoo, naitasababisha ugonjwa mbaya sana.
4 Lakini Bwana ataweka tofauti kati ya mifugo ya Israeli na ile ya Misri, kwamba hakuna mnyama wa Mwisraeli atakayekufa.’”
Yahweh ata tendea tofauti mifugo ya Israeli na mifugo Misri: Haukuna mnyama wa Waisraeli ataye kufa.
5 Bwana akaweka wakati na kusema, “Kesho Bwana atalitenda hili katika nchi.”
Yahweh ametenga muda; amesema, “Ni kesho ambapo nitafanya ilitukio katika nchi."”'
6 Siku iliyofuata Bwana akalitenda: Mifugo yote ya Wamisri ikafa, lakini hakuna hata mnyama mmoja wa wana wa Israeli aliyekufa.
Yahweh akafanya hivi siku iliyofuata: mifugo yote ya Misri ikafa. Lakini hamna mnyama wa Waisraeli aliye kufa, hamna mnyama ata mmoja.
7 Farao akatuma watu kuchunguza, nao wakakuta kuwa hakuna hata mnyama mmoja wa Waisraeli aliyekufa. Lakini moyo wa Farao haukukubali kuwaachia watu waende.
Farao akafanya utafiti, na tazama, hakuna mnyama ata mmoja aliye kufa. Lakini moyo wake ulikuwa mjeuri, hivyo hakuwaacha watu waende.
8 Kisha Bwana akamwambia Mose na Aroni, “Chukueni majivu ya tanuru, naye Mose ayarushe angani mbele ya Farao.
Kisha Yahweh akawambia Musa na Aruni, “Chukuwa majivu na uyajaze mkononi kutoka kwenye tanuru. Wewe, Musa, lazima uyarushe juu wakati Farao akitazama.
9 Yatakuwa vumbi jepesi juu ya nchi yote ya Misri, pia yatatokea majipu yenye kufura juu ya watu na wanyama katika nchi yote.”
Yatakuwa vumbi safi nchi nzima ya Misri. Yatasababisha majipu na mafua kulipuka kwa watu na wanyama katika nchi yote ya Msri.”
10 Basi wakachukua majivu kwenye tanuru na kusimama mbele ya Farao. Mose akayarusha hewani, nayo majipu yenye kufura yakatokea miilini mwa watu na wanyama.
Hivyo Musa na Aruni wakachukuwa majivu kutoka kwenye tanuru na kusimama mbele ya Farao. KIsha Musa akarusha majivu juu. Majivu yakasababisha majipu na mafua kutokea kwa watu na wanyama.
11 Waganga hawakuweza kusimama mbele ya Mose kwa sababu ya majipu yale yaliyokuwa miilini mwao na juu ya miili ya Wamisri wote.
Waganga hawakuweza kumzuia Musa kwasababu ya majipu, kwasababu majipu yalikuwa kwao na kwa Wamisri wote.
12 Lakini Bwana akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, naye hakuwasikiliza Mose na Aroni, sawasawa kama vile Bwana alivyokuwa amemwambia Mose.
Yahweh akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, Farao hakuwasikiliza Musa na Aruni. Hili ndilo Yahweh alilo mwambia Musa Farao atalo fanya.
13 Kisha Bwana akamwambia Mose, “Amka mapema asubuhi, usimame mbele ya Farao, umwambie, ‘Hili ndilo asemalo Bwana, Mungu wa Waebrania: Waachie watu wangu waende, ili kwamba waweze kuniabudu,
Kisha Yahweh akamwambia Musa, Amka asubui mapema, simama mbele ya Farao, na umwambie, 'Yahweh, Mungu wa Waebrania, anasema hivi: Acha watu wangu waende ili wakaniabudu mimi.
14 au wakati huu nitaleta mapigo yangu yenye nguvu dhidi yako, maafisa wako na watu wako, ili upate kujua kuwa hakuna mwingine kama Mimi katika dunia yote.
Kwa muda huu nitatuma mapigo kwako wewe, kwa watumishi wako na watu wako. Nitafanya hivi ili ujue hakuna kama mimi kwenye dunia yote.
15 Kwa kuwa mpaka sasa ningelikuwa nimenyoosha mkono wangu na kukupiga wewe na watu wako kwa pigo ambalo lingekufutilia mbali juu ya nchi.
Mpaka sasa ningeweza kuunyosha mkono wangu na kukushambulia wewe na watu wako kwa ugonjwa, na ungeondelewa kwenye nchi.
16 Lakini nimekuinua wewe kwa kusudi hili hasa, ili nipate kukuonyesha uwezo wangu, na ili Jina langu lipate kutangazwa duniani yote.
Lakini ni kwa sababu hii nimekuruhusu uishi: ili kukuonyesha nguvu zangu, ili kwamba jina langu litangazwe dunia nzima.
17 Bado unaendelea kujiinua juu ya watu wangu, wala hutaki kuwaachia waende.
Bado unajiinua dhidi ya watu wangu kwa kuwaacha wasiende.
18 Kwa hiyo, kesho wakati kama huu nitaleta mvua mbaya sana ya mawe ambayo haijapata kunyesha katika nchi ya Misri, tangu siku ilipoumbwa mpaka leo.
Sikiliza! Kesho muda kama huu nita leta mvua ya mawe ya barafu kubwa, kama ambayo haijawai kuonekana Misri toka ilipo anza hadi sasa.
19 Sasa toa amri urudishe wanyama wote watoke malishoni na chochote ambacho kipo mashambani waje mpaka mahali pa usalama, kwa sababu mvua ya mawe itanyesha juu ya kila mtu na kila mnyama ambaye hajaletwa ndani ambao bado wako nje mashambani, nao watakufa.’”
Kisha sasa, tuma wanaume na ukusanye mifugo yako na vitu vyote ulivyo navyo mashambani sehemu salama. Kila mtu na mnyama aliyeko shambani na hajaletwa nyumbani - mawe ya barufu yatawashukia, na watakufa."”'
20 Wale maafisa wa Farao ambao waliliogopa neno la Bwana wakafanya haraka kuwaleta watumwa wao na mifugo yao ndani.
Kisha hao wa watumishi wa Farao walio amini ujumbe wa Yahweh waka harakisha kuleta watumwa na mifugo yao ndani ya nyumba zao.
21 Lakini wale waliopuuza neno la Bwana wakawaacha watumwa wao na mifugo yao shambani.
Lakini hao ambao hawa kuchukuwa ujumbe wa Yahweh maanani waliacha watumwa wao na mifugo shambani.
22 Ndipo Bwana akamwambia Mose, “Nyoosha mkono wako kuelekea angani ili kwamba mvua ya mawe inyeshe juu ya Misri yote, juu ya watu, wanyama na juu ya kila kitu kiotacho katika mashamba ya Misri.”
Kisha Yahweh akamwambia Musa, “Nyoosha mkono wako kuelekea mbingu ili kuwe na mawe ya barafu katika nchi yote ya Misri, kwa watu, kwa wanyama, na kwenye mimea yote shambani na nchi nzima ya Misri.”
23 Mose alipoinyoosha fimbo yake kuelekea angani, Bwana akatuma ngurumo na mvua ya mawe, umeme wa radi ulimulika hadi nchi. Kwa hiyo Bwana akaifanya mvua ya mawe kunyesha juu ya nchi ya Misri,
Musa akanyoosha mkono na gongo lake kuelekea mbiguni, na Yahweh akatuma mngurumo, mawe ya barafu, na radi kwenye nchi. Pia alinyesha mvua kwenye nchi ya Misri.
24 mvua ya mawe ikanyesha na radi ikamulika pote. Ikawa dhoruba ya kutisha ambayo haijakuwako katika nchi ya Misri, tangu nchi hiyo iwe taifa.
Hivyo kulikuwa na radi iliyo changanyika na mawe ya barafu, ilikuwa hatari sana, kuliko yeyote iliyowai kutokea kwenye nchi ya Misri tangu liwe taifa.
25 Mvua ya mawe ikaharibu kila kitu katika nchi ya Misri kilichokuwa katika mashamba, watu na wanyama, ikaharibu kila kitu kinachoota mashambani na kuvunja kila mti.
Katika nchi yote ya Misri, barafu ya mawe ilipiga kila kitu kwenye shamba, watu na wanyama. Ilipiga kila mmea shambani na kuvunja kila mti.
26 Mahali pekee ambapo mvua ya mawe haikunyesha ni nchi ya Gosheni, ambako Waisraeli waliishi.
Isipo kuwa tu nchi ya Gosheni, walipo ishi Waisraeli, hapakuwa na mawe ya barafu.
27 Ndipo Farao akawaita Mose na Aroni akawaambia, “Wakati huu nimetenda dhambi. Bwana ni mwenye haki, mimi na watu wangu ni wakosaji.
Kisha Farao akatuma wanaume wakawaite Musa na Aruni. Akawaambia, “Nimetenda dhambi wakati huu. Yahweh ni mwenye haki, na mimi na watu wangu ni waovu.
28 Mwombeni Bwana, kwa kuwa tumepata ngurumo na mvua za mawe za kututosha. Nitawaachia mwondoke; hamtahitaji kungoja zaidi.”
Muombe Yahweh, kwasababu radi na barafu ya mawe imezidi. Nitawaacha muende, na hamtabaki tena hapa.”
29 Mose akamjibu, “Nitakapokuwa nimetoka nje ya mji, nitanyoosha mikono yangu juu kumwomba Bwana. Ngurumo zitakoma na hapatakuwepo mvua ya mawe tena, ili upate kujua kuwa, nchi ni mali ya Bwana.
Musa akamwambia, “Nitakapo ondoka tu kwenye mji, nitaitanua mikono yangu kwa Yahweh. Mngurumo utaacha, na hakutakuwa na barafu ya mawe tena. Kwa ili utajua kuwa nchi ni ya Yahweh.
30 Lakini ninajua kuwa wewe na maafisa wako bado hammwogopi Bwana Mungu.”
Lakini kwa wewe na watu wako, najua bado hamu mheshimu Yahweh Mungu.”
31 (Kitani na shayiri viliharibiwa, kwa kuwa shayiri ilikuwa na masuke, na kitani ilikuwa katika kutoa maua.
Sasa kitani na shayiri ziliharibiwa, kwa kuwa shayiri ilikuwa katika kukomaa, na kitani ilikuwa imestawi.
32 Hata hivyo, ngano na jamii nyingine ya ngano hazikuharibiwa kwa sababu zilikuwa hazijakomaa bado.)
Lakini ngano na kusemethu hazikupigwa mana zinachelewa kukua.
33 Kisha Mose akaondoka kwa Farao akaenda nje ya mji. Mose akanyoosha mikono yake kuelekea kwa Bwana, ngurumo na mvua ya mawe vikakoma, mvua haikuendelea tena kunyesha nchini.
Musa alipo muacha Farao na mji, alitanua mikono yake kwa Yahweh; mngurumo na barafu ya mawe ikasimama, na mvua haikunyesha tena.
34 Farao alipoona kwamba mvua ya mawe na ngurumo zimekoma, akafanya dhambi tena. Yeye na maafisa wake wakafanya mioyo yao kuwa migumu.
Farao alipoona mvua, barafu ya mawe, na mngurumo umekatika, akatenda dhambi na kufanya moyo wake kuwa mgumu, pamoja na watumishi wake.
35 Kwa hiyo moyo wa Farao ukawa mgumu, wala hakuwaachia Waisraeli waende, kama vile Bwana alivyokuwa amesema kupitia Mose.
Moyo wa Farao ulikuwa mgumu, hakuacha watu wa Israeli waende. Hivi ndivyo Yahweh alimwambia Musa Farao atafanya.

< Kutoka 9 >