< Kutoka 6 >

1 Kisha Bwana akamwambia Mose, “Sasa utaona kitu nitakachomfanyia Farao: Kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawaachia watu waende; kwa sababu ya mkono wangu wenye nguvu atawafukuza waondoke nchini mwake.”
Kisha Yahweh akasema na Musa, “Sasa utaona nitakacho fanya kwa Farao. Utaona hili, kwa kuwa ata waacha waenda kwa mkono wangu hodari. Kwasababu ya mkono wangu hodari, ata waondoa nje ya nchi.”
2 Pia Mungu akamwambia Mose, “Mimi ndimi Bwana.
Mungu akasema na Musa na kumwambia, “Mimi ni Yahweh.
3 Nilimtokea Abrahamu, Isaki na Yakobo kama Mungu Mwenyezi, ingawa sikuwajulisha Jina langu, Yehova, Mimi mwenyewe sikujitambulisha kwao.
Nilimtokea Ibrahimu, Isaka, na Yakobo kama Mungu mwenye nguvu; lakini kwa jina langu, Yahweh, sikujuliikana kwao.
4 Pia niliweka Agano langu nao kuwapa nchi ya Kanaani, ambako waliishi kama wageni.
Pia niliimarisha agano langu na wao, ilikuwapatia nchi ya Kanani, nchi walioishi kama sio raia, nchi walio tanga tanga.
5 Zaidi ya hayo, nimesikia kilio cha huzuni cha Waisraeli ambao Wamisri wamewatia utumwani, nami nimelikumbuka Agano langu.
Zaidi ya yote, nimesikia kilio cha Waisraeli ambao wa Misri wame wa chukua watumwa, na nimekumbuka agano langu.
6 “Kwa hiyo, waambie Waisraeli: ‘Mimi ndimi Bwana, nami nitawatoa mtoke katika kongwa la Wamisri. Nitawaweka huru mtoke kuwa watumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyooshwa pamoja na matendo makuu ya hukumu.
Kisha basi, sema kwa Waisraeli, 'Mimi ni Yahweh. Nitawatoa kwenye utumwa chini ya wa Misri, na kuwaweka huru na nguvu zao. Nitawaokoa kwa kudhihirisha nguvu zangu, na kwa matendo ya ajabu ya hukumu.
7 Nitawatwaa mwe watu wangu mwenyewe, nami nitakuwa Mungu wenu. Ndipo mtajua kuwa mimi ndimi Bwana Mungu wenu, niliyewatoa chini ya kongwa la Wamisri.
Nitawaleta kwangu kama watu wangu, na nitakuwa Mungu wenu. Mtajua kuwa mimi ndiye Yahweh Mungu wenu, aliye watoa kwenye utumwa chini ya wa Misri.
8 Nami nitawaleta mpaka nchi niliyoapa kwa mkono ulioinuliwa kumpa Abrahamu, Isaki na Yakobo. Nitawapa iwe milki yenu. Mimi ndimi Bwana.’”
Nitawaleta kwenye nchi niliyo muahidi kumpa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo. Nitawapa kama mali yenu. Mimi ni Yahweh.”'
9 Mose akawaarifu Waisraeli jambo hili, lakini hawakumsikiliza kwa sababu ya maumivu makuu ya moyoni na utumwa wa kikatili.
Musa alipo waambia haya Waisraeli, hawakumsiliza kwasababu ya mateso magumu ya utumwa wao.
10 Ndipo Bwana akamwambia Mose,
Hivyo Yahweh akazungumza na Musa na kumwambia,
11 “Nenda, mwambie Farao mfalme wa Misri awaachie Waisraeli waondoke nchini mwake.”
“Nenda umwambie Farao, mfalme wa Misri, awaache watu wa Israeli waondoke kwenye nchi yake.”
12 Lakini Mose akamwambia Bwana, “Ikiwa Waisraeli hawatanisikiliza, kwa nini yeye Farao anisikilize mimi, ambaye huzungumza kwa kigugumizi?”
Musa akamwambia Yahweh, “Kama Waisraeli hawajanisikiliza mimi, kwa nini Farao anisikillize mimi, tangu mimi sio mzuri wakuzungumza?”
13 Ndipo Bwana akanena na Mose na Aroni kuhusu Waisraeli na Farao mfalme wa Misri, naye akawaamuru wawatoe Waisraeli kutoka Misri.
Yahweh akasema na Musa na Aruni. Akawapa amri ya Waisraeli na Farao, mfalme wa Misri, awatoe Waisraeli kutoka nchi ya Misri.
14 Hawa walikuwa wakuu wa jamaa zao: Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli walikuwa Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi. Hawa walikuwa ndio koo za Reubeni.
Hawa walikuwa vichwa wa nyumba za baba yao: wana wa Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa Hanoki, Palu, Hezroni, na Karmi. Hawa walikuwa mababu wa ukoo wa Rubeni.
15 Wana wa Simeoni walikuwa Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli mwana wa mwanamke Mkanaani. Hawa walikuwa ndio koo za Simeoni.
Wana wa Simeoni walikuwa Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Zohari, na Shauli - mwana wa mwanamke wa Kanani. Hawa walikuwa mababu wa ukoo wa Simeoni.
16 Haya ndiyo majina ya wana wa Lawi kufuatana na orodha zao: Gershoni, Kohathi na Merari. Lawi aliishi miaka 137.
Hapa yameorodheshwa majina ya wana wa Lawi, pamoja na uzo wao. Walikuwa ni Gerishoni, Kohathi, na Merari. Lawi aliishi mpaka alipo kuwa na miaka 137.
17 Wana wa Gershoni kwa koo, walikuwa Libni na Shimei.
Wana wa Gerishoni walikuwa Libni na Shimei.
18 Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. Kohathi aliishi miaka 133.
Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Izhari, Hebroni, na uzieli. Kohathi aliishi hadi miaka 133.
19 Wana wa Merari walikuwa Mahli na Mushi. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Lawi kufuatana na orodha zao.
Wana wa Merari walikuwa Mahli na Mushi. Hawa walikuja kuwa mababu wa ukoo wa Walawi, pamoja na uzao wao.
20 Amramu akamwoa Yokebedi, shangazi yake, ambaye alimzalia Aroni na Mose. Amramu aliishi miaka 137.
Amramu alimuoa Yokebedi, dada yake baba yake. Alimzalia Aruni na Musa. Amramu aliishi miaka 137 na akafa.
21 Wana wa Ishari walikuwa Kora, Nefegi na Zikri.
Wana wa Izhari walikuwa Kora, Nefegi, na Zikri.
22 Wana wa Uzieli walikuwa Mishaeli, Elisafani na Sithri.
Wana wa Uzieli walikuwa Mishaeli, Elizafani na Sithri.
23 Aroni akamwoa Elisheba binti wa Aminadabu ndugu yake Nashoni, naye akamzalia Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
Aruni alimuoa Elisheba, binti wa Aminadabu, dada wa Nashoni. Alimzaa Nadabu na Abihu, Eleazari na Ithamari.
24 Wana wa Kora walikuwa Asiri, Elikana na Abiasafu. Hawa walikuwa ndio koo za Kora.
Wana wa Kora walikuwa Asiri, Elikana na Abiasa. Hawa walikuwa mababu wa ukoo wa Wakora.
25 Eleazari mwana wa Aroni akamwoa mmoja wa binti za Putieli, naye akamzalia Finehasi. Hawa walikuwa ndio wakuu wa jamaa za Walawi, ukoo kwa ukoo.
Eleazari, mwana wa Aruni, alimuoa mmoja wa mabinti Wa Putieli. Alimzalia Fineazi. Hawa walikuwa vichwa wa nyumba za baba yao miongoni mwa Walawi, pamoja na uzao wao.
26 Hawa walikuwa Aroni na Mose wale wale ambao Bwana aliwaambia, “Watoeni Waisraeli katika nchi ya Misri kwa vikosi vyao.”
Hawa wanaume wawili walikuwa Musa na Aruni ambao Yahweh alisema, “Waleteni Waisraeli kutoka nchi ya Misri, kwa makundi ya wanaume wapiganaji.”
27 Ndio hao hao waliozungumza na Farao mfalme wa Misri kuhusu kuwatoa Waisraeli Misri. Ilikuwa ni huyo Mose na huyo Aroni.
Aruni na Musa wakazungumza na Farao, mfalme wa Misri, awaruhusu Waisraeli watoke Misri. Hawa walikuwa Musa na Aruni wale wale.
28 Bwana aliponena na Mose huko Misri,
Pale Yahweh alipo zungumza na Musa katika nchi ya Misri,
29 akamwambia, “Mimi ndimi Bwana. Mwambie Farao mfalme wa Misri kila kitu nikuambiacho.”
alimwambia, “Mimi ni Yahweh. Sema kwa Farao, mfalme wa MIsri, kila kitu nitacho kwambia.”
30 Lakini Mose akamwambia Bwana, “Kwa kuwa mimi huzungumza kwa kigugumizi, Farao atanisikiliza mimi?”
Lakini Musa alimwambia Yahweh, “Mimi sio mzuri wa kuongea, hivyo kwanini Farao anisikilize mimi?”

< Kutoka 6 >