< Torati 16 >
1 Shikeni mwezi wa Abibu, na kuiadhimisha Pasaka ya Bwana Mungu wenu, kwa sababu katika mwezi wa Abibu, Mungu aliwatoa Misri usiku.
Angalia mwezi wa Abibu, na uishike pasaka ya Yahwe Mungu wako, kwa kuwa katika mwezi wa Abibu Yahwe Mungu wako alikuleta toka Misri usiku.
2 Mtatoa dhabihu ya Pasaka ya mnyama kwa Bwana Mungu wenu kutoka kundi lenu la mbuzi na kondoo au la ngʼombe, mahali pale ambapo Bwana atapachagua kama makao kwa ajili ya Jina lake.
Utamtolea dhabibu ya pasaka Yahwe Mungu wako na baadhi ya mifugo na wanyama kwenye eneo ambalo Yahwe atachagua kama patakatifu pake.
3 Msile nyama hiyo pamoja na mikate iliyotiwa chachu, lakini kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu, mikate ya kujitesa, kwa sababu mliondoka Misri kwa haraka, ili kwamba siku zote za maisha yenu mpate kukumbuka wakati wenu wa kuondoka Misri.
Hautakula mkate wa chachu pamoja nayo, siku saba utakula mkate usio na chachu, mkate wa mateso; kwa kuwa mlitoka katika nchi ya Misri kwa haraka. Fanya haya katika siku zako zote za maisha yako ili uweze kukumbuka akilini siku mliotoka nchi ya Misri.
4 Chachu isionekane katika mali zenu katika nchi yenu yote kwa siku saba. Nyama yoyote ya dhabihu mtakayotoa jioni ya siku ya kwanza isibakizwe mpaka asubuhi.
Hakuna chachu inapaswa kuonekana miongoni mwenu ndani ya mipaka yenu wakati wa siku saba; wala nyama yoyote mnayotoa dhabihu jioni kwa siku ya kwanza inabaki mpaka asubuhi.
5 Kamwe msitoe dhabihu ya Pasaka katika mji wowote ambao Bwana Mungu wenu amewapa,
Msitoe dhabihu ya pasaka kati ya malango yenu ya ndani ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa.
6 isipokuwa mahali atakapopachagua kama makao kwa ajili ya Jina lake. Hapo ndipo lazima mtoe dhabihu ya Pasaka jioni, jua litakapotua, iwe kumbukumbu yenu ya kutoka Misri.
Badala yake, toa dhabihu katika eneo ambalo Yahwe Mungu wenu atachagua kama patakatifu pake. Hapo mtatoa dhabihu ya pasaka jioni wakati jua linazama, kwa wakati huo wa mwaka mlitoka Misri.
7 Okeni na mle mahali pale ambapo Bwana Mungu wenu atakapopachagua, kisha asubuhi mrudi kwenye mahema yenu.
Mtapaswa kuichoma na kuila katika eneo ambalo Yahwe Mungu wenu atachagua; asubuhi mtageuka na kwenda kwenye mahema yenu.
8 Kwa siku sita mtakula mikate isiyotiwa chachu na siku ya saba fanyeni kusanyiko kwa ajili ya Bwana Mungu wenu na msifanye kazi.
Kwa siku sita mtakula mkate usiotia chachu; katika siku ya saba kutakuwa na kusanyiko makini kwa ajili ya Yahwe Mungu wenu; katika siku hiyo hamtafanya kazi.
9 Mhesabu majuma saba tangu wakati mnapoanza kuchukua mundu kuvuna nafaka.
Mtahesabu wiki saba kwa ajili yenu; tangu wakati mlipoanza kuweka mundu kwenye nafaka iliyosimama mtapaswa kuanza kuhesabu wiki saba.
10 Kisha msherehekee Sikukuu ya Majuma kwa Bwana Mungu wenu kwa kutoa sadaka ya hiari kwa kadiri ya baraka ambayo Bwana Mungu wenu amewapa.
Mtapaswa kushika wiki za sherehe ya Yahwe Mungu wenu pamoja na mchango wa sadaka ya utayari kutoka mkono wako ambayo utatoa, kulingana na Yahwe alivyokubariki.
11 Shangilieni mbele za Bwana Mungu wenu mahali atakapopachagua kama makao ya Jina lake, ninyi, wana wenu na binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, Walawi walio katika miji yenu, na wageni, yatima na wajane waishio miongoni mwenu.
Utafurahi mbele ya Yahwe Mungu wako- wewe, kijana wako, binti wako, mjakazi wako wa kiume, mjakazi wako wa kike, Mlawi aliye katika malango yako, na mgeni, yatima, na mjane alio miongoni mwenu, katika eneo ambalo Yahwe Mungu wako atachagua kwa ajili ya patakatifu pake.
12 Kumbukeni kwamba mlikuwa watumwa kule Misri na mfuate amri hizi kwa uangalifu.
Utakumbuka akilini kwamba ulikuwa mtumwa Misri; unapaswa kuangalia na kuzishika amri hizi.
13 Adhimisheni sikukuu ya vibanda kwa siku saba baada ya kukusanya mazao yenu ya nafaka na kukamua zabibu.
Unapaswa kushika sherehe za vibanda kwa siku saba baada ya kuwa mmekusanya mavuno toka kwenye sakafu ya mapura na kutoka kwenye kinu chako cha divai.
14 Mfurahie sikukuu yenu, ninyi, wana wenu, binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, Walawi, wageni, yatima na wajane ambao wanaishi katika miji yenu.
Utafurahi wakati wa sherehe- wewe, kijana wako, binti wako, mjakazi wako wa kiume, mjakazi wako wa kike, Mlawi, na mgeni, na yatima na mjane walio ndani ya malango yako.
15 Kwa siku saba mtaiadhimisha sikukuu ya Bwana Mungu wenu katika mahali atakapopachagua Bwana. Kwa kuwa Bwana Mungu wenu atawabariki katika mavuno yenu na katika kazi zote za mikono yenu na furaha yenu itakamilika.
Kwa siku saba unapaswa kuangalia sherehe ya Yahwe Mungu wako katika eneo ambalo Yahwe atachagua, kwa sababu Yahwe Mungu wako atakubariki katika mavuno yako yote na kazi ya mikono yako yote, na unapaswa kuwa na furaha kabisa.
16 Wanaume wenu wote lazima wajitokeze mara tatu kwa mwaka mbele za Bwana Mungu wenu mahali atakapopachagua: kwa ajili ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, Sikukuu ya Majuma, na Sikukuu ya Vibanda. Hakuna mtu atakayejitokeza mbele za Bwana mikono mitupu:
Mara tatu kwa mwaka wanaume wako wote wanapaswa kuonekana mbele za Yahwe Mungu wako katika eneo ambalo atachagua: katika sherehe ya mkate usiotiwa chachu, katika sherehe za wiki, na sherehe ya vibanda; na hawataonekana mbele za Yahwe mikono mitupu;
17 Kila mmoja wenu ni lazima alete zawadi kulingana na jinsi ambavyo Bwana Mungu wenu alivyowabariki.
badala yake, kila mtu atatoa kama awezavyo, kwamba mtajua baraka kwamba Yahwe Mungu wako amekupa.
18 Wateue waamuzi na maafisa kwa kila kabila lenu katika kila mji ambao Bwana Mungu wenu anawapa, nao watawaamua watu kwa usawa.
Unapaswa kufanya waamuzi na maakida ndani ya malango yako ambayo Yahwe Mungu wako anakupa; watachukuliwa toka kila kabila, and watahukumu watu kwa hukumu ya haki.
19 Msipotoshe haki wala msifanye upendeleo. Msikubali rushwa kwa sababu rushwa hupofusha macho ya wenye busara na kugeuza maneno ya wenye haki.
Haupaswi kuiondoa haki kwa nguvu; haupaswi kuonesha upendeleo wala kuchukua rushwa, kwa kuwa rushwa upofusha macho ya hekima na kupotosha maneno ya haki.
20 Mfuate haki na haki peke yake, ili mweze kuishi na kuimiliki nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa.
Unapaswa kufata baada ya haki, baada ya haki peke yake, ili kwamba uishi na kurithi nchi ambayo Yahwe Mungu wako anakupa.
21 Msisimamishe nguzo yoyote ya Ashera kando ya madhabahu mliyomjengea Bwana Mungu wenu,
Haupaswi kujitengenezea Asherahi, aina yoyote ya mti, kando ya madhabahu ya Yahwe Mungu wako ambayo utakayojitengenezea.
22 wala msisimamishe jiwe la kuabudu, kwa maana Bwana Mungu wenu anavichukia vitu hivi.
Wala usijitengenezee jiwe takatifu la nguzo, ambalo Yahwe Mungu wako anachukia.