< Torati 15 >

1 Kila mwisho wa miaka saba ni lazima mfute madeni.
Kila mwisho wa kila miaka saba, mnapaswa kufuta madeni.
2 Hivi ndivyo itakavyofanyika: Kila mkopeshaji atafuta mkopo aliomkopesha Mwisraeli mwenzake. Hatamtaka Mwisraeli mwenzake au ndugu yake amlipe hilo deni, kwa sababu wakati wa Bwana wa kufuta madeni umetangazwa.
Hii ni tabia ya ukombozi. Kila mkopeshaji atafuta kile alichompa jirani yake, hata dai kutoka kwa jirani yake au ndugu yake kwa sababu ufutaji wa madeni wa Yahwe umetangazwa.
3 Unaweza kudai malipo kwa mgeni, lakini lazima ufute kila deni ambalo unamdai ndugu yako.
Kutoka kwa mgeni mnaweza kudai; lakini kwa chochote chenu kilicho na ndugu yenu mnapaswa mkitoe.
4 Hata hivyo, hapatakuwepo maskini miongoni mwenu, kwa kuwa katika nchi Bwana Mungu wenu anayowapa kuimiliki kama urithi wenu, atawabariki sana,
Hata hivyo, pasiwepo maskini miongoni mwenu (kwa kuwa Yahwe kwa hakika atawabariki kwenye nchi ambayo anawapa kama urithi kumiliki)
5 ikiwa tutamtii Bwana Mungu wenu kikamilifu na kuwa waangalifu kuyafuata maagizo haya yote ninayowapa leo.
kama peke yenu mnasikiliza kwa bidii sauti ya Yahwe Mungu wenu, kuzishika amri zote ambazo anawaamuru leo.
6 Kwa kuwa Bwana Mungu wenu atawabariki kama alivyoahidi, nanyi mtawakopesha mataifa mengi lakini hamtakopa kwa yeyote. Mtatawala mataifa mengi lakini hakuna taifa litakalowatawala ninyi.
Kwa kuwa Yahwe Mungu wenu atawabariki, kama alivyowaahidia; mtakopesha mataifa mengi, lakini hamtaazima; mtaongoza juu ya mataifa mengi, lakini hayatawaongoza ninyi.
7 Ikiwa kuna mtu maskini miongoni mwa ndugu zenu, katika mji wowote wa hiyo nchi ambayo Bwana Mungu wenu anawapa, msiwe na moyo mgumu wala usimfumbie mkono ndugu yako aliye maskini.
Kama kuna mtu maskini miongoni mwenu, moja wa ndugu zenu, ndani ya malango yenu yoyote kwenye nchi yenu ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa, msifanye migumu mioyo yenu wala kufunga mkono wenu toka kwa ndugu yenu,
8 Afadhali fungua mikono yako na umkopeshe kwa hiari chochote anachohitaji.
Lakini mnapaswa hakika kufungua mkono wenu kwake na hakika mkopeshe yeye vya kutosha hitaji lake.
9 Jihadhari usijiwekee wazo hili ovu: “Mwaka wa saba, mwaka wa kufuta madeni umekaribia,” usije ukaonyesha nia mbaya kwa ndugu yako mhitaji na ukaacha kumpa chochote. Anaweza kumlalamikia Bwana dhidi yako nawe utakuwa umepatikana na hatia ya dhambi.
Muwe makini kutokuwa na wazo ovu au potovu katika moyo wenu, kusema, “Mwaka wa saba, mwaka wa ukombozi u karibu; ili kwamba msiwe wachoyo kuhusiana na ndugu zenu maskini na haumpi chochote; anaweza kumlilia Yahwe kuhusu nyie, na itakuwa dhambi yenu.
10 Mpe kwa ukarimu na ufanye hivyo bila kinyongo moyoni, ndipo kwa sababu ya hili Bwana Mungu wenu atakubariki katika kazi zako zote na kwa kila kitu utakachokiwekea mkono wako.
Mnapaswa kwa hakika mmpe, na moyo wenu hampaswi kuhuzunika wakati mnampa, kwa sababu kurudishiwa kwa Yahwe huyu Mungu wenu atawabariki katika kazi zenu zote na katika chochote mnaweka mkono wenu.
11 Siku zote watakuwepo watu maskini katika nchi. Kwa hiyo ninawaamuru mwe na mikono iliyokunjuliwa kuwaelekea ndugu zenu, kuwaelekea maskini na wahitaji katika nchi yenu.
Kwa kuwa maskini kamwe hatakoma kuishi katika nchi, kwa hiyo nakuamuru wewe na kusema, “Unapaswa kwa hakika ufungue mkono wako kwa ndugu yako, kwa mhitaji wako, na kwa maskini wako katika nchi yako.
12 Kama Mwebrania mwenzako, mwanaume au mwanamke, akijiuza kwako na kukutumikia miaka sita, katika mwaka wa saba ni lazima umwache aende zake akiwa huru.
Kama ndugu yako, ni mwebrania wa kiume au mwebrania wa kike, ameuzwa kwako na anakutumikia kwa miaka saba, basi katika mwaka wa saba unapaswa umwache aende zake huru.
13 Nawe wakati utakapomwachia usimwache aende mikono mitupu.
Unapomwacha aende zake huru, usimwache aende mkono mtupu.
14 Mpe kwa uhuru kutoka zizi lako la kondoo na mbuzi, kutoka sakafu yako ya kupuria nafaka na kutoka mashinikizo yako ya kukamulia divai. Mpe kama vile ambavyo Bwana Mungu wako alivyokubariki.
Unapaswa kwa ukarimu hutoe kwake kutoka mifugo yako, kutoka pura iliyo chini, na kinu chako cha mvinyo. Kama Yahwe Mungu wako alivyokubariki, unapaswa umpe yeye.
15 Kumbukeni kuwa ninyi mlikuwa watumwa huko Misri naye Bwana Mungu wenu aliwakomboa. Ndiyo sababu nimewapa agizo hili leo.
Unapaswa kukumbuka kwamba ulikuwa mtumwa kwenye nchi ya Misri, na kwamba Yahwe Mungu wako alikukomboa; kwa hiyo ninakuamuru leo kufanya hivi.
16 Lakini mtumishi wako akikuambia, “Sitaki kukuacha,” kwa sababu anakupenda wewe na jamaa yako naye anaridhika nawe,
Itakuwa kwamba kama atasema kwako, “Sitaenda mbali yako; kwa sababu anakupenda na nyumba yako, na kwa sababu ni mzuri kwako,
17 ndipo utachukua chuma kidogo utoboe sikio lake mpaka hicho chuma kiingie kwenye ubao wa mlango, naye atakuwa mtumishi wako wa maisha. Ufanye vivyo hivyo kwa mtumishi wa kike.
basi unapaswa kuchukua uma na msukumo kupitia sikio lake kwenye mlango, na atakuwa mtumwa wako milele. Na pia kwa mtumwa wako wa kike utafanya vilevile.
18 Usifikiri kuwa kuna ugumu kumwacha mtumishi wako huru, kwa sababu utumishi wake kwako kwa miaka hii sita umekuwa wa thamani mara mbili ya ujira wa mtumishi wa kuajiriwa. Naye Bwana Mungu wenu atakubarikia kwa kila kitu utakachofanya.
Isionekane kuwa vigumu kwako kumwachia aende zake huru, kwa sababu amekutumikia kwa miaka sita na amekupa mara mbili udhamani wa mtu aliyeajiriwa. Yahwe Mungu wako atakubariki katika yote unayofanya.
19 Wekeni wakfu kwa Bwana Mungu wenu kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa makundi yenu ya ngʼombe na ya mbuzi na kondoo. Maksai walio wazaliwa wa kwanza msiwafanyize kazi, wala msinyoe manyoya ya wazaliwa wa kwanza wa kondoo.
Wazao wote wa kwanza wa kiume katika wanyama na mifugo wako unapaswa uwatenge kwa Yahwe Mungu wako. Hautafanya kazi na mzao wa kwanza wa wanyama wako wala kumnyoa mzao wa kwanza wa mfugo wako.
20 Kila mwaka ninyi na jamaa zenu mtapaswa kuwala mbele za Bwana Mungu wenu pale mahali atakapopachagua.
Unapaswa umle mzaliwa wa kwanza mbele ya Yahwe Mungu wako kila mwaka katika eneo ambalo Yahwe atachagua, wewe na nyumba yako.
21 Kama mnyama ana dosari, akiwa ni kilema au kipofu au kama ana kilema kibaya, kamwe usimtoe dhabihu kwa Bwana Mungu wenu.
Kama ina kasoro yoyote- kwa mfano, kama ni kilema au kipofu, au ana kasoro yoyote- haupaswi kumtoa dhabihu kwa Yahwe Mungu wako.
22 Itawapasa kumla ninyi wenyewe katika miji yenu. Wote wasio safi na walio safi kwa desturi za kiibada mwaweza kula kama vile mnavyokula paa au kulungu.
Utamla ndani ya malango yako; mtu asiye najisi na aliye najisi ni sawa unapaswa kula, kama ungekula paa au kulungu.
23 Lakini kamwe msinywe damu; imwageni ardhini kama maji.
Pekee haupaswi kunywa damu yake; unapaswa kuimwanga damu yake juu ya ardhi kama maji.

< Torati 15 >