< 1 Wafalme 11 >
1 Hata hivyo, Mfalme Solomoni akawapenda wanawake wengi wa kigeni zaidi, mbali na binti Farao: wanawake wa Wamoabu, Waamoni, Waedomu, Wasidoni na Wahiti.
Basi mfalme Sulemani aliwapenda wanawake wengi wa kigeni: binti wa Farao na wanawake wa Wamoabu, Waamori, Waedomu, Wasidoni, na Wahiti - Haya na
2 Walitoka katika mataifa ambayo Bwana aliwaambia Waisraeli, “Msije mkaoana nao, kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu mgeukie miungu yao.” Hata hivyo, Solomoni akakaza kuwapenda.
mataifa ambayo BWANA alikuwa amewaambia Waisraeli kwamba, “Msiwaoe, wala binti zenu kuolewa nao, kwani kwa hakika wataigeuza mioyo yenu ili mfuate miungu yao.” Lakini Sulemani aliwapenda wanawake hao.
3 Alikuwa na wake 700 mabinti wa uzao wa kifalme, na masuria 300, nao wake zake wakampotosha.
Sulemani alikuwa na wanawake halali mia saba na masuria mia tatu. Wake zake waliugeuza moyo wake.
4 Kadiri Solomoni alivyozidi kuzeeka, wake zake wakaugeuza moyo wake kuelekea miungu mingine, na moyo wake haukujitolea kikamilifu kwa Bwana Mungu wake, kama ulivyokuwa moyo wa Daudi baba yake.
Kwa kuwa Sulemani alipozeeka, wake zake waliugeuza moyo wake kwa miungu mingine; hakuutoa moyo wake wote kwa BWANA, Mungu wake, kama ulivyokuwa moyo wa Daudi baba yake.
5 Solomoni akafuata Ashtorethi mungu mke wa Wasidoni, na Moleki mungu aliyekuwa chukizo la Waamoni.
Kwani Sulemani alimfuata Ashtoreth, mungu mke wa Wasidoni, na alimfuata Milkom, ambayo ni sanamu chukizo ya Waamori.
6 Kwa hiyo Solomoni akafanya uovu machoni pa Bwana; hakumfuata Bwana kikamilifu kama alivyofanya Daudi baba yake.
Sulemani akafanya maovu mbele ya BWANA; hakumfuata BWANA kwa moyo wake wote, kama alivyofanya Daudi baba yake.
7 Kwenye kilima mashariki mwa Yerusalemu, Solomoni akajenga mahali pa juu kwa ajili ya Kemoshi chukizo la Wamoabu, na kwa Moleki mungu chukizo la Waamoni.
Kisha Sulemani akajenga mahali pa juu pa Kemoshi, ambayo ni sanamu chukizo ya Wamoabu, mashariki mwa Yerusalemu juu ya kilima, na vivyo hivyo na Moleki, Sanamu chukizo ya Waamoni.
8 Akafanya hivyo kwa wake zake wote wa kigeni, ambao walifukiza uvumba na kutoa dhabihu kwa miungu yao.
Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa kigeni, ambao walifukiza uvumba na kutoa sadaka kwa miungu yao.
9 Bwana akamkasirikia Solomoni kwa sababu moyo wake uligeuka mbali na Bwana, Mungu wa Israeli, ambaye alikuwa amemtokea mara mbili.
BWANA alichukizwa na Sulemani, kwa sababu moyo wake ulikuwa umemwacha Mungu wa Israeli, ingawa alikuwa amejionyesha kwake mara mbili
10 Ingawa alikuwa amemkataza Solomoni kufuata miungu mingine, Solomoni hakutii amri ya Bwana.
na kumwamuru juu ya mambo haya, kwamba asiwaendee miungu wengine. Bali Sulemani hakutii kile ambacho BWANA alikuwa amemwamuru.
11 Kwa hiyo Bwana akamwambia Solomoni, “Kwa kuwa hii ndiyo hali yako na hukushika Agano langu na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme kutoka kwako na kumpa mmoja wa walio chini yako.
Kwa hiyo BWANA akamwambia Sulemani, “Kwa kuwa umeyafanya haya haukulishika agano langu na maagizo ambayo nilikuamuru, basi nitaugawa ufalme kutoka kwako na kuwapatia watumishi wako.
12 Hata hivyo, kwa ajili ya Daudi baba yako, sitafanya jambo hili wakati wa uhai wako. Nitaurarua kutoka mikononi mwa mwanao.
Hata hivyo, kwa ajili ya Daudi, sitalifanya hilo wakati wa uhai wako, bali nitaugawa wakati ukiwa chini ya mwanao.
13 Lakini pia sitaurarua ufalme wote kutoka kwake, bali nitampa kabila moja kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu na kwa ajili ya Yerusalemu, ambao nimeuchagua.”
Bado sitaugawanya ufalme wote; Nitampa mwanao kabila moja kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, na kwa ajili ya Yerusalemu, ambayo nimeichagua.”
14 Kisha Bwana akamwinua adui dhidi ya Solomoni, Hadadi, Mwedomu, kutoka ukoo wa ufalme wa Edomu.
Kisha BWANA akamwinulia uadui Sulemani, Hadadi Mwedomu. Alikuwa anatoka kwenye familiia ya mfalme wa Edomu.
15 Huko nyuma wakati Daudi alipokuwa akipigana na Edomu, Yoabu jemadari wa jeshi, aliyekuwa amekwenda kuzika waliouawa, alikuwa amewaua wanaume wote waliokuwako Edomu.
Daudi alipokuwa Edomu, Yoabu mkuu wa jeshi alikuwa ameenda kuzika mfu, kila mtu aliyekuwa ameuawa kule Edomu.
16 Yoabu na Waisraeli wote walikaa huko kwa miezi sita, mpaka walipomaliza kuwaangamiza wanaume wote huko Edomu.
Yoabu na Israeli yote walibaki huko kwa miezi sita mpaka alipokuwa amewaua wanaume wote wa Edomu.
17 Lakini Hadadi, akiwa bado mvulana mdogo, alikimbilia Misri akiwa na baadhi ya maafisa wa Kiedomu waliokuwa wakimhudumia baba yake.
Lakini Hadadi alichulukuliwa na Waedomu wengine na watumishi wa baba yake hadi Misri, kuanzia Hadadi alipokuwa mtoto mdogo.
18 Wakaondoka Midiani wakaenda Parani. Basi wakichukua pamoja nao wanaume kutoka Parani, wakaenda Misri, kwa Farao mfalme wa Misri, ambaye alimpa Hadadi nyumba, ardhi na akampatia chakula.
Waliondoka Midiani wakaja Parani, ambapo walichukuliwa na wanaume mpaka Misri, kwa Farao wa Misri, ambaye alimpa nyumba na ardhi yenye chakula.
19 Farao akapendezwa sana na Hadadi hata akampa ndugu wa mkewe mwenyewe, Malkia Tapenesi, ili aolewe na Hadadi.
Hadadi alipata neema kubwa machoni pa Farao, kwa hiyoFarao akampatia mke, umbu wa mke wake mwenyewe, umbu la Tapenesi aliyekuwa Malkia.
20 Huyo ndugu wa Tapenesi akamzalia mwana aliyeitwa Genubathi, ambaye alilelewa na Tapenesi katika jumba la kifalme. Huko Genubathi aliishi pamoja na watoto wa Farao mwenyewe.
Naye huyo umbu la Tapenesi alimzalia Hadadi mwana. Wakamwita jina lake Genubathi. Tapenesi akamlea katika ikulu ya Farao. Kwa hiyo Genubathi alikulia kwenye ikulu ya Farao pamoja na watoto wa Farao.
21 Alipokuwa huko Misri, Hadadi alisikia kwamba Daudi amepumzika na baba zake na ya kwamba pia Yoabu aliyekuwa jemadari wa jeshi amekufa. Ndipo Hadadi akamwambia Farao, “Niruhusu niende ili niweze kurudi katika nchi yangu.”
Naye alipokuwa huko Misri, Hadadi alisikia kuwa Daudi alishalala na mababu zake na kwamba Yoabu mkuu wa majeshi alishakufa, Hadadi akamwambia Farao, “Acha niondoke nirudi nchini kwangu.”
22 Farao akauliza, “Umekosa nini hapa, kwamba unataka kurudi katika nchi yako?” Hadadi akajibu, “Hakuna, lakini niruhusu niende!”
Lakini Farao alimwambia, “Umepungukiwa nini kwangu, kwamba sasa unatafuta kurudi nchini kwako?” Naye Hadadi akamjibu, “Hapana kitu lakini tafadhali niache niende.”
23 Mungu akamwinua adui mwingine dhidi ya Solomoni, Rezoni mwana wa Eliada, ambaye alikuwa amemkimbia bwana wake Hadadezeri, mfalme wa Soba.
Pia Mungu akamwinulia Sulemani adui mwingine, Rezoni mwana wa Eliada, aliyekuwa amemkimbia bwana wake Hadadezeri mfalme wa Soba.
24 Akawakusanya watu, naye akawa kiongozi wa kundi la waasi, wakati Daudi alipoangamiza majeshi ya Soba; waasi walikwenda Dameski, mahali walipokaa na kumiliki.
Rezoni alijikusanyia wanaume naye akawa mkuu wa jeshi dogo, Daudi ali owapiga wanaume wa Soba. Wale wanume Rezoni walienda Dameski kuishi huko, na Rezoni aliitawala Dameski.
25 Rezoni alikuwa adui wa Israeli kwa muda wote alioishi Solomoni, ukiongezea matatizo yaliyosababishwa na Hadadi. Kwa hiyo Rezoni akatawala katika Aramu na alikuwa mkatili kwa Israeli.
Yeye akawa adui wa Israeli katika siku zote za mfalme Sulemani, zaidi ya madhara ambayo Hadadi alisababisha. Rezoni akawachukia Israeli na akawa juu ya Shamu
26 Pia, Yeroboamu mwana wa Nebati aliasi dhidi ya mfalme. Alikuwa mmoja wa maafisa wa Solomoni, Mwefraimu kutoka Sereda, ambaye mama yake alikuwa mjane aliyeitwa Serua.
Kisha Yeroboamu mwana wa Nebati, mwefraimu wa Sereda, akida wa Sulemani, ambaye jina la mama yake lilikuwa Serua, mjane, pia akainua mkono wake dhidi ya mfalme.
27 Haya ndiyo maelezo ya jinsi alivyomwasi mfalme: Solomoni alikuwa amejenga Milo naye akawa ameziba mwanya katika ukuta wa mji wa Daudi baba yake.
Kisa cha kuinua mkono wake kinyume cha mfalme ilikuwa ni mfalme Sulemani kujenga Milo na kufunga mahali palipobomoka katika mji wa Daudi baba yake.
28 Basi Yeroboamu alikuwa mtu shujaa na hodari, naye Solomoni alipoona jinsi kijana alivyofanya kazi yake, akamweka kuwa kiongozi wa kazi yote ya mikono ya nyumba ya Yosefu.
Yeroboamu alikuwa mtu hodari na shujaa. Sulemani akaona kuwa huyo kijana alikuwa na bidii, kwa hiyo akampa kuwa na mamlaka juu ya wafanyakazi katika nyumba ya Yusufu.
29 Karibu na wakati ule Yeroboamu alikuwa anatoka nje ya Yerusalemu, Ahiya nabii Mshiloni akakutana naye njiani, akiwa amevaa joho jipya. Hawa wawili walikuwa peke yao mashambani,
Wakati huo, Yeroboamu alipokuwa akitoka katika Yerusalemu, nabii Ahiya Mshilo akamkuta barabarani. Sasa Ahiya alikuwa amevaa vazi jipya na kwamba hawa wawili walikuwa pekee yao kondeni.
30 naye Ahiya akachukua joho jipya alilokuwa amevaa akalirarua vipande kumi na viwili.
Kisha Ahiya akalishika lile vazi jipya ambalo alikuwa nalo na akalichana katika vipande kumi na viwili.
31 Kisha akamwambia Yeroboamu, “Chukua vipande kumi kwa ajili yako, kwa kuwa hivi ndivyo Bwana, Mungu wa Israeli asemavyo: ‘Tazama, ninakwenda kuuchana ufalme kutoka mikononi mwa Solomoni na kukupa wewe makabila kumi.
Akamwambia Yeroboamu. “Chukua vipande kumi, kwani BWANA, Mungu wa Israeli, anasema, 'Tazama, Nitaugawa ufalme toka katika mkono wa Sulemani nami nitakupa makabila kumi.
32 Lakini kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi na mji wa Yerusalemu, ambao nimeuchagua miongoni mwa makabila yote ya Israeli, atakuwa na kabila moja.
(lakini Sulemani atabaki na kabila moja, kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi na kwa ajili ya mji wangu Yerusalemu - mji ambao nimeuchagua toka kwenye kabila zote za Israeli),
33 Nitafanya hivi kwa sababu wameniacha mimi na kuabudu Ashtorethi mungu mke wa Wasidoni, Kemoshi mungu wa Wamoabu, na Moleki mungu wa Waamoni, nao hawakwenda katika njia zangu ili kufanya yaliyo sawa machoni pangu, wala kushika amri na sheria zangu kama Daudi, babaye Solomoni, alivyofanya.
kwa kuwa ameniacha na kumwabudu Ashtorethi mungu mke wa Wasidoni, Kemoshi Mungu wa Wamoabu, na Milikomu mungu wa watu wa Amoni. Wameziacha njia zangu, hawakufanya kilicho chema katika macho yangu, wala hawa kuzishika amri na maagizo yangu, kama alivyofanya Daudi baba yake.
34 “‘Lakini sitauondoa ufalme wote kutoka mikononi mwa Solomoni, nimemfanya mtawala siku zote za maisha yake kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, niliyemchagua na ambaye aliyatunza maagizo na amri zangu.
Hata hivyo. Stauchukua ufalme wote toka kwenye mkono wa Sulemani. Badala yake, nimemfanya kuwa mtawala katika siku zake zote za uhai wake, kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu ambaye nilimchagua, mtu ambaye alizishika amri na maagizo yangu.
35 Nitauondoa ufalme kutoka mikononi mwa mwanawe na kukupa wewe makabila kumi.
Bali nitauchukua ufalme ukiwa chini ya mkono wa mwanae na nitakupa wewe, makabila kumi.
36 Nitampa mwanawe kabila moja ili kwamba Daudi mtumishi wangu awe na taa mbele zangu daima katika Yerusalemu, mji ambao nimeuchagua kuweka Jina langu.
Nitampa kabila moja mwana wa Sulemani ili kwamba Daudi mtumishi wagu atabaki kuwa nuru mbele yangu huko Yerusalemu, mji ambao nimeuchagua ili niweke jina langu.
37 Hata hivyo, kukuhusu wewe Yeroboamu, nitakutwaa, nawe utatawala juu ya yote yale moyo wako unayotamani, utakuwa mfalme juu ya Israeli.
Nami nitakuchukua, nawe utatawala ili kutimiza haja yako, nawe utakuwa mfalme juu ya Israeli.
38 Ikiwa utafanya kila nitakalokuamuru, kuenenda katika njia zangu na kufanya yaliyo sawa mbele za macho yangu kwa kuzishika amri zangu na maagizo yangu kama alivyofanya Daudi mtumishi wangu, nitakuwa pamoja nawe. Nitakujengea ufalme utakaodumu kama ule niliomjengea Daudi, nami nitakupa Israeli.
Kama utasikiliza yote ninayokuagaza, na kama utatembea katika njia zangu na kufanya kinachopendeza mbele ya macho yangu, ukayashika maagizo na amri zangu, kama Daudi mtumishi wangu alivyofanya, ndipo nitakapokuwa na wewe na nitakujengea nyumba ya uhakika, kama niliyomjengea Daudi, nami nitakupa Israeli.
39 Nitawatesa wazao wa Daudi kwa ajili ya hili, lakini siyo milele.’”
Nitawaadhibu uzao wa Daudi, lakini si milele.”
40 Solomoni akajaribu kumuua Yeroboamu, lakini Yeroboamu akakimbilia Misri, kwa Mfalme Shishaki, naye akakaa huko mpaka Solomoni alipofariki.
Kwa hiyo Sulemani akajaribu kumwua Yeroboamu. Lakini Yeroboamu akaamka na kukimbilia Misri, Kwa Shishaki mfalme wa Misri, naye akabaki Misri mpaka Sulemani alipokufa.
41 Kwa habari za matukio mengine ya utawala wa Solomoni, yote aliyoyafanya na hekima aliyoionyesha, je hayakuandikwa yote katika kitabu cha matendo cha Solomoni?
Na kwa mambo mengine yanayomhusu Sulemani, Yote ambayo alifanya na hekima zake, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya
42 Solomoni alitawala Israeli yote miaka arobaini, akiwa Yerusalemu.
Sulemani? Sulemani alitawala Yerusalemu juu ya Israeli yote kwa miaka arobaini.
43 Kisha Solomoni akalala pamoja na baba zake, naye akazikwa katika mji wa Daudi baba yake. Naye Rehoboamu mwanawe akawa mfalme baada yake.
Naye akalala na mababu zake na alizikwa katika mji wa Daudi baba yake. Rehoboamu mwanae akawa mfalme mahali pake.