< Corinthios Ii 3 >
1 incipimus iterum nosmet ipsos commendare aut numquid egemus sicut quidam commendaticiis epistulis ad vos aut ex vobis
Je, tumeanza kujisifia wenyewe tena? Hatuhitaji barua ya mapendekezo kwenu au kutoka kwenu, kama baadhi ya watu, je twahitaji?
2 epistula nostra vos estis scripta in cordibus nostris quae scitur et legitur ab omnibus hominibus
Ninyi wenyewe ni barua yetu ya mapendekezo, iliyoandikwa kwenye mioyo yetu, inayojulikana na kusomwa na watu wote.
3 manifestati quoniam epistula estis Christi ministrata a nobis et scripta non atramento sed Spiritu Dei vivi non in tabulis lapideis sed in tabulis cordis carnalibus
Na mnaonesha kwamba ninyi ni barua kutoka kwa Kristo, iliyotolewa na sisi. Iliandikwa siyo kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai. Haikuandikwa juu ya vibao vya mawe, bali juu ya vibao vya mioyo ya wanadamu.
4 fiduciam autem talem habemus per Christum ad Deum
Na huu ndiyo ujasiri tulio nao katika Mungu kupitia Kristo.
5 non quod sufficientes simus cogitare aliquid a nobis quasi ex nobis sed sufficientia nostra ex Deo est
Hatujiamini wenyewe kwa kudai chochote kama kutoka kwetu. Badala yake, kujiamini kwetu kunatoka kwa Mungu.
6 qui et idoneos nos fecit ministros novi testamenti non litterae sed Spiritus littera enim occidit Spiritus autem vivificat
Ni Mungu ambaye alitufanya tuweze kuwa watumishi wa agano jipya. Hili ni agano sio la barua bali ni la Roho. Kwa kuwa barua huua, lakini roho inatoa uhai.
7 quod si ministratio mortis litteris deformata in lapidibus fuit in gloria ita ut non possent intendere filii Israhel in faciem Mosi propter gloriam vultus eius quae evacuatur
Sasa kazi ya kifo iliyokuwa imechongwa katika herufi juu ya mawe ilikuja kwa namna ya utukufu kwamba watu wa Israeli hawakuangalia moja kwa moja kwenye uso wa Musa. Hii ni kwa sababu ya utukufu wa uso wake, utukufu ambao ulikuwa unafifia.
8 quomodo non magis ministratio Spiritus erit in gloria
Je, kazi ya Roho haitakuwa na utukufu zaidi?
9 nam si ministratio damnationis gloria est multo magis abundat ministerium iustitiae in gloria
Kwa kuwa kama huduma ya hukumu ilikuwa na utukufu, ni mara ngapi zaidi huduma ya haki huzidi sana katika utukufu!
10 nam nec glorificatum est quod claruit in hac parte propter excellentem gloriam
Ni kweli kwamba, kile kilichofanywa utukufu kwanza hakina utukufu tena katika heshima hii, kwa sababu ya utukufu unaouzidi.
11 si enim quod evacuatur per gloriam est multo magis quod manet in gloria est
Kwa kuwa kama kile ambacho kilikuwa kinapita kilikuwa na utukufu, ni kwa kiasi gani zaidi kile ambacho ni cha kudumu kitakuwa na utukufu!
12 habentes igitur talem spem multa fiducia utimur
Kwa kuwa tunajiamini hiyo, tunaujasiri sana.
13 et non sicut Moses ponebat velamen super faciem suam ut non intenderent filii Israhel in faciem eius quod evacuatur
Hatuko kama Musa, aliyeweka utaji juu ya uso wake, ili kwamba watu wa Israel wasiweze kuangalia moja kwa moja kwenye mwisho wa utukufu ambao ulikuwa unatoweka.
14 sed obtusi sunt sensus eorum usque in hodiernum enim diem id ipsum velamen in lectione veteris testamenti manet non revelatum quoniam in Christo evacuatur
Lakini fahamu zao zilikuwa zimefungwa. Hata mpaka siku hii utaji uleule bado unabaki juu ya usomaji wa agano la kale. Haijawekwa wazi, kwa sababu ni katika Kristo pekee inaondolewa mbali.
15 sed usque in hodiernum diem cum legitur Moses velamen est positum super cor eorum
Lakini hata leo, wakati wowote Musa asomwapo, utaji hukaa juu ya mioyo yao.
16 cum autem conversus fuerit ad Deum aufertur velamen
Lakini mtu anapogeuka kwa Bwana, utaji unaondolewa.
17 Dominus autem Spiritus est ubi autem Spiritus Domini ibi libertas
Sasa Bwana ni Roho. Palipo na Roho wa Bwana, kuna uhuru.
18 nos vero omnes revelata facie gloriam Domini speculantes in eandem imaginem transformamur a claritate in claritatem tamquam a Domini Spiritu
Sasa sisi sote, pamoja na nyuso zisizo wekewa utaji, huona utukufu wa Bwana. Tunabadilishwa ndani ya muonekano uleule wa utukufu kutoka shahada moja ya utukufu kwenda nyingine, kama ilivyo kutoka kwa Bwana, ambaye ni Roho.