< Corinthios I 1 >
1 Paulus vocatus apostolus Christi Iesu per voluntatem Dei et Sosthenes frater
Paulo, aliyeitwa na Kristo Yesu kuwa mtume kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu,
2 ecclesiae Dei quae est Corinthi sanctificatis in Christo Iesu vocatis sanctis cum omnibus qui invocant nomen Domini nostri Iesu Christi in omni loco ipsorum et nostro
kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, kwa wale ambao wamewekwa wakfu katika Yesu Kristo, ambao wameitwa kuwa watu watakatifu. Tunawaandikia pia wale wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo katika mahali pote, Bwana wao na wetu.
3 gratia vobis et pax a Deo Patre nostro et Domino Iesu Christo
Neema na amani iwe kwenu kutoka kwa Mungu baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo.
4 gratias ago Deo meo semper pro vobis in gratia Dei quae data est vobis in Christo Iesu
Siku zote namshukru Mungu wangu kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu ambayo Kristo Yesu aliwapa.
5 quia in omnibus divites facti estis in illo in omni verbo et in omni scientia
Amewafanya kuwa matajiri katika kila njia, katika usemi na pamoja maarifa yote.
6 sicut testimonium Christi confirmatum est in vobis
Amewafanya matajiri, kama ushuhuda kuhusu Kristo ya kwamba amethibitishwa kuwa kweli miongoni mwenu.
7 ita ut nihil vobis desit in ulla gratia expectantibus revelationem Domini nostri Iesu Christi
Kwa hiyo hampungukiwi karama za kiroho, kama mlivyo na hamu ya kusubiri ufunuo wa Bwana wetu Yesu Kristo.
8 qui et confirmabit vos usque ad finem sine crimine in die adventus Domini nostri Iesu Christi
Atawaimarisha ninyi pia hadi mwisho, ili msilaumiwe siku ya Bwana wetu Yesu Kristo.
9 fidelis Deus per quem vocati estis in societatem Filii eius Iesu Christi Domini nostri
Mungu ni mwaminifu ambaye aliwaita ninyi katika ushirika wa mwana wake, Yesu Kristo Bwana wetu.
10 obsecro autem vos fratres per nomen Domini nostri Iesu Christi ut id ipsum dicatis omnes et non sint in vobis scismata sitis autem perfecti in eodem sensu et in eadem sententia
Sasa nawasihi kaka na dada zangu, kupitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba wote mkubali, na kwamba kusiwe na migawanyiko miongoni mwenu. Nawasihi kwamba muungane pamoja katika nia moja na katika kusudi moja.
11 significatum est enim mihi de vobis fratres mei ab his qui sunt Chloes quia contentiones inter vos sunt
Kwani watu wa nyumba ya Kloe wamenitaarifu kuwa kuna mgawanyiko unaoendelea miongoni mwenu.
12 hoc autem dico quod unusquisque vestrum dicit ego quidem sum Pauli ego autem Apollo ego vero Cephae ego autem Christi
Nina maana hii: Kila mmoja wenu husema, “Mimi ni wa Paulo,” au “Mimi ni wa Apolo”, au “Mimi ni wa Kefa” au “Mimi ni wa Kristo”.
13 divisus est Christus numquid Paulus crucifixus est pro vobis aut in nomine Pauli baptizati estis
Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulubiwa kwa ajili yenu? Je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?
14 gratias ago Deo quod neminem vestrum baptizavi nisi Crispum et Gaium
Namshukuru Mungu kuwa sikumbatiza yeyote, isipokuwa Krispo na Gayo.
15 ne quis dicat quod in nomine meo baptizati sitis
Hii ilikuwa kwamba hakuna yeyote angesema mlibatizwa kwa jina langu.
16 baptizavi autem et Stephanae domum ceterum nescio si quem alium baptizaverim
(Pia niliwabatiza wa nyumba ya Stephania. Zaidi ya hapo, sijui kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote).
17 non enim misit me Christus baptizare sed evangelizare non in sapientia verbi ut non evacuetur crux Christi
Kwa kuwa, Kristo hakunituma kubatiza bali kuhubiri injili. Hakunituma kuhubiri kwa maneno ya hekima ya kibinadamu, ili kwamba nguvu ya msalaba wa Kristo isiondolewe.
18 verbum enim crucis pereuntibus quidem stultitia est his autem qui salvi fiunt id est nobis virtus Dei est
Kwa kuwa ujumbe wa msalaba ni upuuzi kwa wale wanaokufa. Lakini kwa wale ambao Mungu anawaokoa, ni nguvu ya Mungu.
19 scriptum est enim perdam sapientiam sapientium et prudentiam prudentium reprobabo
Kwa kuwa imeandikwa, “Nitaiharibu hekima ya wenye busara. Nitauharibu ufahamu wa wenye akili.”
20 ubi sapiens ubi scriba ubi conquisitor huius saeculi nonne stultam fecit Deus sapientiam huius mundi (aiōn )
Yuko wapi mtu mwenye busara? Yuko wapi mwenye elimu? Yuko wapi msemaji mshawishi wa dunia hii? Je, Mungu hakuigeuza hekima ya dunia hii kuwa ujinga? (aiōn )
21 nam quia in Dei sapientia non cognovit mundus per sapientiam Deum placuit Deo per stultitiam praedicationis salvos facere credentes
Tangu dunia imekuwa katika hekima yake haikumjua Mungu, ilimpendeza Mungu katika ujinga wao wa kuhubiri ili kuokoa wale wanaoamini.
22 quoniam et Iudaei signa petunt et Graeci sapientiam quaerunt
Kwa Wayahudi huuliza ishara za miujiza na kwa Wayunani hutafuta hekima.
23 nos autem praedicamus Christum crucifixum Iudaeis quidem scandalum gentibus autem stultitiam
Lakini tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa, aliye kikwazo kwa Wayahudi na ni ujinga kwa Wayunani.
24 ipsis autem vocatis Iudaeis atque Graecis Christum Dei virtutem et Dei sapientiam
Lakini kwa wale ambao waliitwa na Mungu, Wayahudi na Wayunani, tunamhubiri Kristo kama nguvu na hekima ya Mungu.
25 quia quod stultum est Dei sapientius est hominibus et quod infirmum est Dei fortius est hominibus
Kwa kuwa ujinga wa Mungu una hekima kuliko ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.
26 videte enim vocationem vestram fratres quia non multi sapientes secundum carnem non multi potentes non multi nobiles
Angalia wito wa Mungu juu yenu, kaka na dada zangu. Si wengi wenu mlikuwa na hekima katika viwango vya kibinadamu. Si wengi wenu mlikuwa na nguvu. Si wengi wenu mlizaliwa katika ukuu.
27 sed quae stulta sunt mundi elegit Deus ut confundat sapientes et infirma mundi elegit Deus ut confundat fortia
Lakini Mungu alichagua vitu vijinga vya dunia ili kuviaibisha vyenye hekima. Mungu alichagua kilicho dhaifu katika dunia kukiaibisha chenye nguvu.
28 et ignobilia mundi et contemptibilia elegit Deus et quae non sunt ut ea quae sunt destrueret
Mungu alichagua kile kilicho cha hali ya chini na kilichodharauliwa katika dunia. Alichagua hata vitu ambavyo havikuhesabiwa kuwa kitu, kwa kuvifanya si kitu vitu vilivyo na thamani.
29 ut non glorietur omnis caro in conspectu eius
Alifanya hivi ili asiwepo yeyote aliye na sababu ya kujivuna mbele zake.
30 ex ipso autem vos estis in Christo Iesu qui factus est sapientia nobis a Deo et iustitia et sanctificatio et redemptio
Kwa sababu ya kile Mungu alichofanya, sasa mko ndani ya Kristo Yesu, ambaye amefanyika hekima kwa ajili yetu kutoka kwa Mungu. Alikuwa haki yetu, utakatifu na ukombozi.
31 ut quemadmodum scriptum est qui gloriatur in Domino glorietur
Kama matokeo, kama andiko lisemavyo, “Anayejisifu, ajisifu katika Bwana.”