< מִשְׁלֵי 26 >

כשלג בקיץ וכמטר בקציר כן לא נאוה לכסיל כבוד׃ 1
Kama theluji wakati wa kiangazi au mvua wakati wa mavuno, ndivyo asivyostahili heshima mpumbavu.
כצפור לנוד כדרור לעוף כן קללת חנם לא תבא׃ 2
Kama shomoro apigapigavyo mabawa yake au mbayuwayu katika kuruka kwake kasi, ndivyo ilivyo laana isiyo na sababu haimpati mtu.
שוט לסוס מתג לחמור ושבט לגו כסילים׃ 3
Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, nayo fimbo kwa migongo ya wapumbavu!
אל תען כסיל כאולתו פן תשוה לו גם אתה׃ 4
Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama wewe mwenyewe utakuwa kama yeye.
ענה כסיל כאולתו פן יהיה חכם בעיניו׃ 5
Mjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama atakuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe.
מקצה רגלים חמס שתה שלח דברים ביד כסיל׃ 6
Kama vile ilivyo kujikata miguu au kunywa hasara, ndivyo ilivyo kutuma ujumbe kwa mkono wa mpumbavu.
דליו שקים מפסח ומשל בפי כסילים׃ 7
Kama miguu ya kiwete inavyoningʼinia ndivyo ilivyo mithali katika kinywa cha mpumbavu.
כצרור אבן במרגמה כן נותן לכסיל כבוד׃ 8
Kama kufunga jiwe kwenye kombeo, ndivyo ilivyo kumpa mpumbavu heshima.
חוח עלה ביד שכור ומשל בפי כסילים׃ 9
Kama mwiba kwenye mkono wa mlevi ndivyo ilivyo mithali kinywani mwa mpumbavu.
רב מחולל כל ושכר כסיל ושכר עברים׃ 10
Kama mpiga upinde ambaye hujeruhi ovyo, ndivyo alivyo yeye aajiriye mpumbavu au yeyote apitaye njiani.
ככלב שב על קאו כסיל שונה באולתו׃ 11
Kama mbwa ayarudiavyo matapiko yake, ndivyo mpumbavu arudiavyo upumbavu wake.
ראית איש חכם בעיניו תקוה לכסיל ממנו׃ 12
Je, unamwona mtu ajionaye mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Liko tumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko kwake.
אמר עצל שחל בדרך ארי בין הרחבות׃ 13
Mvivu husema, “Yuko simba barabarani, simba mkali anazunguka mitaa!”
הדלת תסוב על צירה ועצל על מטתו׃ 14
Kama vile mlango ugeukavyo kwenye bawaba zake, ndivyo mvivu ajigeuzavyo kitandani mwake.
טמן עצל ידו בצלחת נלאה להשיבה אל פיו׃ 15
Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani, naye huchoka kuupeleka kwenye kinywa chake.
חכם עצל בעיניו משבעה משיבי טעם׃ 16
Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe, kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara.
מחזיק באזני כלב עבר מתעבר על ריב לא לו׃ 17
Kama yeye amkamataye mbwa kwa masikio, ndivyo alivyo mtu apitaye njiani na kujiingiza kwenye ugomvi usiomhusu.
כמתלהלה הירה זקים חצים ומות׃ 18
Kama mtu mwendawazimu atupaye vijinga vya moto au mishale ya kufisha,
כן איש רמה את רעהו ואמר הלא משחק אני׃ 19
ndivyo alivyo mtu amdanganyaye jirani yake na kusema, “Nilikuwa nikifanya mzaha tu!”
באפס עצים תכבה אש ובאין נרגן ישתק מדון׃ 20
Bila kuni moto huzimika; pasipo uchongezi ugomvi humalizika.
פחם לגחלים ועצים לאש ואיש מדונים לחרחר ריב׃ 21
Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, na kama kuni kwenye moto, ndivyo alivyo mtu mgomvi kwa kuchochea ugomvi.
דברי נרגן כמתלהמים והם ירדו חדרי בטן׃ 22
Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu; huingia sehemu za ndani sana za mtu.
כסף סיגים מצפה על חרש שפתים דלקים ולב רע׃ 23
Kama rangi ingʼaayo iliyopakwa kwenye vyombo vya udongo ndivyo ilivyo midomo laini pamoja na moyo mbaya.
בשפתו ינכר שונא ובקרבו ישית מרמה׃ 24
Mtu mwenye nia ya kudhuru wengine hujificha kwa maneno ya midomo yake, lakini moyoni mwake huficha udanganyifu.
כי יחנן קולו אל תאמן בו כי שבע תועבות בלבו׃ 25
Ingawa maneno yake huvutia, usimwamini, kwa maana machukizo saba hujaza moyo wake.
תכסה שנאה במשאון תגלה רעתו בקהל׃ 26
Nia yake ya kudhuru wengine inaweza kufichwa na udanganyifu, lakini uovu wake utafichuliwa kwenye kusanyiko.
כרה שחת בה יפל וגלל אבן אליו תשוב׃ 27
Kama mtu akichimba shimo, atatumbukia ndani yake, kama mtu akivingirisha jiwe, litamrudia.
לשון שקר ישנא דכיו ופה חלק יעשה מדחה׃ 28
Ulimi wa uongo, huwachukia wale unaowaumiza, nacho kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.

< מִשְׁלֵי 26 >