< תהילים 30 >

מזמור שיר-חנכת הבית לדוד ב ארוממך יהוה כי דליתני ולא-שמחת איבי לי 1
Nitakutukuza wewe, Yahwe, kwa kuwa umeniinua na haujawaruhusu maadui zangu juu yangu.
יהוה אלהי-- שועתי אליך ותרפאני 2
Yahwe Mungu wangu, nilikulilia wewe kwa ajili ya msaada, nawe ukaniponya.
יהוה--העלית מן-שאול נפשי חייתני מיורדי- (מירדי-) בור (Sheol h7585) 3
Yahwe, wewe umeitoa roho yangu kuzimuni; nawe umeniweka hai mbali na kaburi. (Sheol h7585)
זמרו ליהוה חסידיו והודו לזכר קדשו 4
Mwimbieni sifa Yahwe, ninyi waaminifu wake! Mshukuruni Bwana mkumbukapo utakatifu wake.
כי רגע באפו-- חיים ברצונו בערב ילין בכי ולבקר רנה 5
Kwa kuwa hasira yake ni ya muda tu; bali neema yake yadumu milele. Kilio huja usiku, bali furaha huja asubuhi.
ואני אמרתי בשלוי-- בל-אמוט לעולם 6
Kwa ujasiri nilisema, “Sitatikiswa kamwe.”
יהוה-- ברצונך העמדתה להררי-עז הסתרת פניך הייתי נבהל 7
Yahwe, kwa neema yako uliniweka mimi kama mlima imara; lakini ulipouficha uso wako, nilisumbuka.
אליך יהוה אקרא ואל-אדני אתחנן 8
Nilikulilia wewe, Yahwe, na kuomba msaada kwa Bwana wangu!
מה-בצע בדמי ברדתי אל-שחת היודך עפר היגיד אמתך 9
Kuna faida gani katika kifo changu, kama nitaenda kaburini? Je, mavumbi yatakusifu wewe? Yatatangaza uaminifu wako?
שמע-יהוה וחנני יהוה היה-עזר לי 10
Sikia, Yahwe, na unihurumie! Yahwe, uwe msaidizi wangu.
הפכת מספדי למחול לי פתחת שקי ותאזרני שמחה 11
Wewe umegeuza kuomboleza kwangu kuwa kucheza; wewe umeyaondoa mavazi yangu ya magunia na kunivisha furaha.
למען יזמרך כבוד-- ולא ידם יהוה אלהי לעולם אודך 12
Hivyo sasa utukufu wangu utakuimbia sifa wewe na hautanyamaza; Yahwe Mungu wangu, nitakushukuru wewe milele!

< תהילים 30 >