< מִשְׁלֵי 24 >
אל-תקנא באנשי רעה ואל-תתאו להיות אתם | 1 |
Usiwe na husuda kwa wenye ubaya, wala usitamani kuambatana nao,
כי-שד יהגה לבם ועמל שפתיהם תדברנה | 2 |
kwa sababu mioyo yao inapanga njama za vurugu na midomo ya huongea juu ya madhara.
בחכמה יבנה בית ובתבונה יתכונן | 3 |
Kwa hekima nyumba hujengwa na kwa ufahamu huimarishwa.
ובדעת חדרים ימלאו-- כל-הון יקר ונעים | 4 |
Kwa maarifa vyumba hujazwa vitu vyote vya thamani na utajiri wa kupendeza.
גבר-חכם בעוז ואיש-דעת מאמץ-כח | 5 |
Shujaa wa hekima ni imara, na mtu wa maarifa huongeza nguvu zake;
כי בתחבלות תעשה-לך מלחמה ותשועה ברב יועץ | 6 |
maana kwa uongozi wa busara unaweza kufanya vita na kwa washauri wengi kuna ushindi.
ראמות לאויל חכמות בשער לא יפתח-פיהו | 7 |
Hekima ipo juu sana kwa mpumbavu; hafumbui kinywa chake kwenye mlango.
מחשב להרע-- לו בעל-מזמות יקראו | 8 |
Kuna yule mwenye kupanga kufanya mabaya- watu wanamwita bwana wa njama.
זמת אולת חטאת ותועבת לאדם לץ | 9 |
Mipango ya mpumbavu ni dhambi na watu humchukia mwenye dhihaka.
התרפית ביום צרה-- צר כחכה | 10 |
Kama utakuwa dhaifu na mwenye kuogopa siku ya taabu, basi nguvu zako ni haba.
הצל לקחים למות ומטים להרג אם-תחשוך | 11 |
Waokoe wanaochukuliwa kwenda kwenye mauti na uwashikilie wale wanaopepesuka kwenda kwa mchinjaji.
כי-תאמר-- הן לא-ידענו-זה הלא-תכן לבות הוא-יבין ונצר נפשך הוא ידע והשיב לאדם כפעלו | 12 |
Kama utasema, “Tazama, hatujui chochote juu ya hili,” je yule anayepima mioyo hajui unachosema? Na yule anayelinda maisha yako, je hajui? Je Mungu hatampa kila mmoja kile anachostahili?
אכל-בני דבש כי-טוב ונפת מתוק על-חכך | 13 |
Mwanangu, kula asali kwa kuwa ni nzuri, kwa sababu matone ya sega la asali ni matamu unapoonja.
כן דעה חכמה--לנפשך אם-מצאת ויש אחרית ותקותך לא תכרת | 14 |
Hekima ndiyo ilivyo katika nafsi yako - kama utaitafuta, tumaini lako halitabatilika na kutakuwa na tumaini.
אל-תארב רשע לנוה צדיק אל-תשדד רבצו | 15 |
Usisubiri kwa kuvizia kama waovu ambao hushambulia nyumba ya mwenye haki. Usiiharibu nyumba yake!
כי שבע יפול צדיק וקם ורשעים יכשלו ברעה | 16 |
Maana mwenye haki huanguka mara saba na kuinuka tena, lakini waovu huangushwa kwa maafa.
בנפל אויביך (אויבך) אל-תשמח ובכשלו אל-יגל לבך | 17 |
Usisherekee wakati adui yako anapoanguka na wala moyo wako usifurahi anapojikwaa,
פן-יראה יהוה ורע בעיניו והשיב מעליו אפו | 18 |
au Yehova ataona na kutoridhika na kuondoa ghadhabu juu yake.
אל-תתחר במרעים אל-תקנא ברשעים | 19 |
Usifadhaike kwa sababu ya watenda mabaya, na wala usiwahusudu watu waovu,
כי לא-תהיה אחרית לרע נר רשעים ידעך | 20 |
maana mtu mbaya hana matumaini na taa ya watu waovu itazimika.
ירא-את-יהוה בני ומלך עם-שונים אל-תתערב | 21 |
Mwanangu; mche Yehova, na umwogope mfalme, usishirikiane na watu wenye kuasi dhidi yao,
כי-פתאם יקום אידם ופיד שניהם מי יודע | 22 |
maana kwa ghafula msiba wao utakuja na ni nani ajuaye ukubwa wa uharibifu utakao kuja kutoka kwa hao wote?
גם-אלה לחכמים הכר-פנים במשפט בל-טוב | 23 |
Haya ni maneno ya wenye busara pia. Upendeleo katika kuhukumu kesi kwa sheria si vizuri.
אמר לרשע--צדיק אתה יקבהו עמים יזעמוהו לאמים | 24 |
Anayemwambia mwenye hatia, “Wewe upo sawa,” atalaaniwa na watu na mataifa yatamchukia.
ולמוכיחים ינעם ועליהם תבוא ברכת-טוב | 25 |
Bali wenye kuwakemea waovu watakuwa na furaha na zawadi za wema zitakuja kwao.
שפתים ישק משיב דברים נכחים | 26 |
Anayetoa jibu la kweli hutoa busu kwenye midomo.
הכן בחוץ מלאכתך--ועתדה בשדה לך אחר ובנית ביתך | 27 |
Andaa kazi yako ya nje, na tayarisha kila kitu kwa ajili yako mwenyewe shambani; baada ya hapo, jenga nyumba yako.
אל-תהי עד-חנם ברעך והפתית בשפתיך | 28 |
Usitoe ushahidi dhidi ya jirani yako bila sababu na usidanganye kwa midomo yako.
אל-תאמר--כאשר עשה-לי כן אעשה-לו אשיב לאיש כפעלו | 29 |
Usiseme, “Mimi nitamtendea kile alichonitendea; nitalipiza kwa kile alichofanya.”
על-שדה איש-עצל עברתי ועל-כרם אדם חסר-לב | 30 |
Nilikwenda jirani na shamba la mtu mvivu, nikapita kwenye shamba la mzabibu la mtu asiye na akili.
והנה עלה כלו קמשנים--כסו פניו חרלים וגדר אבניו נהרסה | 31 |
Miiba imeota kila sehemu, ardhi ilikuwa imefunikwa kwa upupu, na ukuta wake wa mawe ulikuwa umebomoka.
ואחזה אנכי אשית לבי ראיתי לקחתי מוסר | 32 |
Kisha nikaliona na kufikiria juu yake; nikatazama na kupokea mafundisho.
מעט שנות מעט תנומות מעט חבק ידים לשכב | 33 |
Kulala kidogo, kusinzia kidogo, kupumzika kwa kukunja mikono kidogo-
ובא-מתהלך רישך ומחסריך כאיש מגן | 34 |
na umasikini huja kwa kutembea juu yako, na mahitaji yako kama askari mwenye silaha.