< מִשְׁלֵי 19 >
טוב-רש הולך בתמו-- מעקש שפתיו והוא כסיל | 1 |
Afadhali mtu maskini ambaye mwenendo wake hauna lawama, kuliko mpumbavu ambaye midomo yake imepotoka.
גם בלא-דעת נפש לא-טוב ואץ ברגלים חוטא | 2 |
Sio vizuri kuwa na juhudi bila maarifa, wala kufanya haraka na kuikosa njia.
אולת אדם תסלף דרכו ועל-יהוה יזעף לבו | 3 |
Upumbavu wa mtu mwenyewe huharibu maisha yake hata hivyo moyo wake humkasirikia Bwana.
הון--יסיף רעים רבים ודל מרעהו יפרד | 4 |
Mali huleta marafiki wengi, bali rafiki wa mtu maskini humwacha.
עד שקרים לא ינקה ויפיח כזבים לא ימלט | 5 |
Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa, naye amwagaye uongo hataachwa huru.
רבים יחלו פני-נדיב וכל-הרע לאיש מתן | 6 |
Wengi hujipendekeza kwa mtawala na kila mmoja ni rafiki wa mtu atoaye zawadi.
כל אחי-רש שנאהו-- אף כי מרעהו רחקו ממנו מרדף אמרים לא- (לו-) המה | 7 |
Mtu maskini huepukwa na ndugu zake wote: Je, marafiki zake watamkwepa kiasi gani! Ingawa huwafuata kwa kuwasihi, hawapatikani popote.
קנה-לב אהב נפשו שמר תבונה למצא-טוב | 8 |
Yeye apataye hekima huipenda nafsi yake mwenyewe, yeye ahifadhiye ufahamu hustawi.
עד שקרים לא ינקה ויפיח כזבים יאבד | 9 |
Shahidi wa uongo hataacha kuadhibiwa, naye amwagaye uongo ataangamia.
לא-נאוה לכסיל תענוג אף כי-לעבד משל בשרים | 10 |
Haistahili mpumbavu kuishi katika anasa, itakuwa vibaya kiasi gani kwa mtumwa kuwatawala wakuu.
שכל אדם האריך אפו ותפארתו עבר על-פשע | 11 |
Hekima ya mtu humpa uvumilivu, ni kwa utukufu wake kusamehe makosa.
נהם ככפיר זעף מלך וכטל על-עשב רצונו | 12 |
Ghadhabu ya mfalme ni kama mngurumo wa simba, bali wema wake ni kama umande juu ya nyasi.
הות לאביו בן כסיל ודלף טרד מדיני אשה | 13 |
Mwana mpumbavu ni maangamizi ya babaye, naye mke mgomvi ni kama kutonatona kusikoisha.
בית והון נחלת אבות ומיהוה אשה משכלת | 14 |
Nyumba na mali hurithiwa kutoka kwa wazazi, bali mke mwenye busara hutoka kwa Bwana.
עצלה תפיל תרדמה ונפש רמיה תרעב | 15 |
Uvivu huleta usingizi mzito, naye mtu mzembe huona njaa.
שמר מצוה שמר נפשו בוזה דרכיו יומת (ימות) | 16 |
Yeye ambaye hutii mafundisho huulinda uhai wake, bali yeye anayezidharau njia zake atakufa.
מלוה יהוה חונן דל וגמלו ישלם-לו | 17 |
Yeye amhurumiaye maskini humkopesha Bwana, naye atamtuza kwa aliyotenda.
יסר בנך כי-יש תקוה ואל-המיתו אל-תשא נפשך | 18 |
Mrudi mwanao, kwa maana katika hiyo kuna tumaini, usiwe mshirika katika mauti yake.
גרל- (גדל-) חמה נשא ענש כי אם-תציל ועוד תוסף | 19 |
Mtu mwenye kukasirika haraka ni lazima atapata adhabu yake, kama utamwokoa, itakubidi kufanya hivyo tena.
שמע עצה וקבל מוסר-- למען תחכם באחריתך | 20 |
Sikiliza mashauri na ukubali mafundisho, nawe mwishoni utakuwa na hekima.
רבות מחשבות בלב-איש ועצת יהוה היא תקום | 21 |
Kuna mipango mingi ndani ya moyo wa mtu, lakini kusudi la Bwana ndilo litakalosimama.
תאות אדם חסדו וטוב-רש מאיש כזב | 22 |
Lile mtu alionealo shauku ni upendo usio na mwisho, afadhali kuwa maskini kuliko kuwa mwongo.
יראת יהוה לחיים ושבע ילין בל-יפקד רע | 23 |
Kumcha Bwana huongoza kwenye uzima, kisha mtu hupumzika akiwa ameridhika, bila kuguswa na shida.
טמן עצל ידו בצלחת גם-אל-פיהו לא ישיבנה | 24 |
Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani, lakini hawezi hata kuupeleka kwenye kinywa chake!
לץ תכה ופתי יערם והוכיח לנבון יבין דעת | 25 |
Mpige mwenye mzaha, naye mjinga atajifunza busara, mkemee mwenye ufahamu naye atapata maarifa.
משדד-אב יבריח אם-- בן מביש ומחפיר | 26 |
Yeye amwibiaye baba yake na kumfukuza mama yake ni mwana aletaye aibu na fedheha.
חדל-בני לשמע מוסר לשגות מאמרי-דעת | 27 |
Mwanangu, ukiacha kusikiliza mafundisho, utatangatanga mbali na maneno ya maarifa.
עד בליעל יליץ משפט ופי רשעים יבלע-און | 28 |
Shahidi mla rushwa hudhihaki hukumu na kinywa cha mtu mwovu humeza ubaya kwa upesi.
נכונו ללצים שפטים ומהלמות לגו כסילים | 29 |
Adhabu zimeandaliwa kwa ajili ya wenye dhihaka na mapigo kwa ajili ya migongo ya wapumbavu.