< Ezekiel 17 >

1 And the word of Jehovah came to me, saying:
Neno la Bwana likanijia kusema:
2 Son of man, put forth a riddle, and speak a parable to the house of Israel;
“Mwanadamu, tega kitendawili, ukawaambie nyumba ya Israeli fumbo.
3 and say, Thus saith the Lord Jehovah: A great eagle, with great wings, with long feathers, full of plumage, which had divers colors, came to Lebanon, and took the highest branch of a cedar.
Waambie hivi, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Tai mkubwa mwenye mabawa yenye nguvu, yaliyojaa manyoya marefu ya rangi mbalimbali, alikuja Lebanoni. Akatua kwenye kilele cha mwerezi,
4 He cropped off the top of its young twigs, and carried it into a land of traffic; he set it in a city of merchants.
akakwanyua ncha yake na kuichukua mpaka nchi ya wafanyabiashara, akaipanda huko katika mji wa wachuuzi.
5 He took also one of the shoots of the land, and put it in a fruitful field; he placed it by great waters, and set it as a willow-tree.
“‘Akachukua baadhi ya mbegu za nchi yako na kuziweka katika udongo wenye rutuba. Akazipanda kama mti umeao kando ya maji mengi,
6 And it grew and became a spreading vine of low stature, whose branches turned towards him, and whose roots were under him. It became a vine, that brought forth branches, and shot forth boughs.
nazo zikaota na kuwa mzabibu mfupi, unaoeneza matawi yake. Matawi yake yakamwelekea huyo tai, mizizi yake ikabaki chini ya huo mzabibu. Kwa hiyo ukawa mzabibu na kutoa matawi na vitawi vyenye majani mengi.
7 There was also another great eagle, with great wings and many feathers; and, behold, this vine bent its roots toward him, and shot forth its branches toward him, that he might water it from the beds where it was planted.
“‘Lakini kulikuwa na tai mwingine mkubwa, mwenye mabawa yenye nguvu yaliyojaa manyoya. Tazama! Huu mzabibu ukatoa mizizi yake kumwelekea huyo tai kutoka mle kwenye shamba lile ulikopandwa na kutanda matawi yake kumwelekea kwa ajili ya kupata maji.
8 And yet it was planted in a good soil, by great waters, that it might bring forth branches, and that it might bear fruit, and be a goodly vine.
Ulikuwa umepandwa katika udongo mzuri wenye maji mengi ili uweze kutoa matawi, kuzaa matunda na uweze kuwa mzabibu mzuri sana.’
9 Say thou, Thus saith the Lord Jehovah: Shall it prosper? Shall not he pull up its roots, and cut off its fruit, that it wither? In all the leaves of its branching shall it wither; even without a mighty arm, or many people, shall he pluck it up by the roots.
“Waambie, ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Je, utastawi? Je, hautangʼolewa na kuondolewa matunda yake, ili uweze kunyauka? Majani yake mapya yanayochipua yote yatanyauka. Hautahitaji mkono wenye nguvu au watu wengi kuungʼoa na mizizi yake.
10 Yea, behold, it is planted; but shall it prosper? Shall it not utterly wither, when the east wind toucheth it? It shall wither in the beds where it grew.
Hata kama utapandwa pengine, Je, utastawi? Je, hautanyauka kabisa wakati upepo wa mashariki utakapoupiga, yaani, hautanyauka kabisa katika udongo mzuri ambamo ulikuwa umestawi vizuri?’”
11 Moreover, the word of Jehovah came to me, saying:
Ndipo neno la Bwana likanijia kusema:
12 Say now to the rebellious house, Know ye not what these things mean? Say, behold, the king of Babylon came to Jerusalem, and took her king and her princes, and led them with him to Babylon,
“Waambie nyumba hii ya kuasi, ‘Je, mnajua hii ina maana gani?’ Waambie: ‘Mfalme wa Babeli alikwenda Yerusalemu na kumchukua mfalme na watu maarufu, akarudi nao na kuwaleta mpaka Babeli.
13 and took one of the king's offspring, and made a covenant with him, and took an oath of him, and the mighty of the land he took away,
Ndipo akamchukua mmoja wa jamaa ya mfalme na kufanya mapatano naye, akamfanya aape. Akawachukua pia viongozi wa nchi,
14 that the kingdom might be brought low, so as not to lift itself up; that the covenant might be kept, and stand.
ili kuudhoofisha ufalme huo, usiweze kuinuka tena, ila uweze kuendelea tu chini ya mapatano yake.
15 But he rebelled against him, in sending his ambassadors into Egypt, that they might give him horses and much people. Shall he prosper? Shall he escape that doeth such things? Shall he break the covenant and be delivered?
Lakini mfalme aliasi dhidi yake kwa kutuma wajumbe wake kwenda Misri ili kupatiwa farasi na jeshi kubwa. Je, atashinda? Je, atafanikiwa? Je, mtu afanyaye mambo kama hayo ataokoka? Je, atavunja mapatano na bado aokoke?
16 As I live saith the Lord Jehovah, surely in the place where the king dwelleth that made him king, whose oath he despised, and whose covenant he broke, even with him in the midst of Babylon shall he die.
“‘Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, atafia huko Babeli, katika nchi ya mfalme aliyemketisha katika kiti cha enzi, ambaye alidharau kiapo chake na kuvunja mapatano yake.
17 Neither shall Pharaoh with his mighty army and great multitude accomplish anything for him in war, when they shall cast up mounds, and build forts to cut off many persons,
Farao na jeshi lake kubwa, na wingi wake wa watu hawataweza kusaidia chochote katika vita, wakati watakapozungukwa na jeshi ili kukatilia mbali maisha ya watu wengi.
18 he hath despised the oath, and broken the covenant; behold, he hath given the hand, and yet done all these things; he shall not escape!
Alidharau kiapo kwa kuvunja Agano. Kwa sababu aliahidi kwa mkono wake mwenyewe na bado akafanya mambo haya yote, hataokoka.
19 Therefore thus saith the Lord Jehovah: As I live, surely mine oath, which he hath despised, and my covenant, which he hath broken, will I recompense upon his own head.
“‘Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Hakika kama niishivyo, nitaleta juu ya kichwa chake kiapo changu, alichokidharau na Agano langu lile alilolivunja.
20 And I will spread my net upon him, and he shall be taken in my snare, and I will bring him to Babylon, and will contend with him there for his trespass which he hath committed against me.
Nitautandaza wavu wangu kwa ajili yake, naye atanaswa katika mtego wangu. Nitamleta mpaka Babeli na kutekeleza hukumu juu yake huko kwa kuwa hakuwa mwaminifu kwangu.
21 And all his fugitives with all his hosts shall fall by the sword, and they that remain shall be scattered to all the winds; and ye shall know that I, Jehovah, have spoken it.
Askari wake wote wanaotoroka wataanguka kwa upanga, nao watakaonusurika watatawanyika katika pande zote za dunia. Ndipo utakapojua kuwa Mimi Bwana nimesema.
22 Thus saith the Lord Jehovah: I also will take from the top of the high cedar, and will get it; and from the highest of its twigs will I crop a tender one, and plant it upon a high and lofty mountain.
“‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi mwenyewe nitachukua chipukizi kutoka kwenye kilele cha juu sana cha mwerezi na kukipanda, nitavunja kitawi kichanga kutoka matawi yake ya juu kabisa na kukipanda juu ya mlima mrefu ulioinuka sana.
23 Upon a high mountain of Israel will I plant it, and it shall bring forth boughs, and bear fruit, and be a goodly cedar; and under it shall dwell birds of every wing; in the shadow of its branches shall they dwell.
Katika vilele vya mlima mrefu wa Israeli nitakipanda, kitatoa matawi na kuzaa matunda na kuwa mwerezi mzuri sana. Ndege wa kila aina wataweka viota vyao ndani yake, nao watapata makazi katika kivuli cha matawi yake.
24 And all the trees of the field shall know that I, Jehovah, have brought down the high tree, and exalted the low tree; that I have dried up the green tree, and made the dry tree green. I, Jehovah, have spoken, and will do it.
Miti yote ya kondeni itajua kuwa Mimi Bwana ninaishusha miti mirefu na kuikuza miti mifupi kuwa miti mirefu. Mimi naikausha miti mibichi na kuifanya miti mikavu istawi. “‘Mimi Bwana nimesema, nami nitatenda.’”

< Ezekiel 17 >