Aionian Verses
And all his sons and all his daughters rose up to comfort him; but he refused to be comforted; and he said, For I will go down into the grave unto my son mourning. Thus his father wept for him. (Sheol )
Wanawe wote na binti zake wakaja kumfariji, lakini hakukubali kufarijiwa. Akasema, “Hapana, nitamwombolezea mwanangu mpaka nimfikie kaburini.” Kwa hiyo baba yake akaendelea kumlilia. (Sheol )
And he said, My son shall not go down with you; for his brother is dead, and he is left alone: if mischief befall him by the way in the which all of you go, then shall all of you bring down my gray hairs with sorrow to the grave. (Sheol )
Lakini Yakobo akasema, “Mwanangu hatashuka huko pamoja nanyi; ndugu yake amekufa naye ndiye peke yake aliyebaki. Ikiwa atapatwa na madhara katika safari mnayoiendea, mtashusha kichwa changu chenye mvi kaburini kwa masikitiko.” (Sheol )
And if all of you take this also from me, and mischief befall him, all of you shall bring down my gray hairs with sorrow to the grave. (Sheol )
Ikiwa mtaniondolea huyu tena na akapatwa na madhara, mtashusha kichwa changu chenye mvi kaburini nikiwa mwenye huzuni.’ (Sheol )
It shall come to pass, when he sees that the lad is not with us, that he will die: and your servants shall bring down the gray hairs of your servant our father with sorrow to the grave. (Sheol )
akiona kijana hayupo nasi, atakufa. Watumishi wako watashusha kichwa chenye mvi cha baba yetu kaburini kwa huzuni. (Sheol )
But if the LORD make a new thing, and the earth open her mouth, and swallow them up, with all that appertain unto them, and they go down quick into the pit; then all of you shall understand that these men have provoked the LORD. (Sheol )
Lakini ikiwa Bwana ataleta jambo jipya kabisa, ardhi ikifunua kinywa chake na kuwameza wao, pamoja na kila kitu kilicho mali yao, nao washuke chini kaburini wakiwa hai, ndipo mtafahamu kuwa watu hawa wamemdharau Bwana.” (Sheol )
They, and all that appertained to them, went down alive into the pit, and the earth closed upon them: and they perished from among the congregation. (Sheol )
Wakashuka chini kaburini wakiwa hai, pamoja na kila kitu walichokuwa nacho; nchi ikajifunika juu yao, nao wakaangamia wakatoweka kutoka kusanyiko. (Sheol )
For a fire is kindled in mine anger, and shall burn unto the low hell, and shall consume the earth with her increase, and set on fire the foundations of the mountains. (Sheol )
Kwa maana moto umewashwa kwa hasira yangu, ule uwakao hadi kwenye vina vya mauti. Utateketeza dunia pamoja na mazao yake, na kuwasha moto katika misingi ya milima. (Sheol )
The LORD kills, and makes alive: he brings down to the grave, and brings up. (Sheol )
“Bwana huua na huleta uhai, hushusha chini mpaka kaburini na hufufua. (Sheol )
The sorrows of hell compassed me about; the snares of death prevented me; (Sheol )
Kamba za kuzimu zilinizunguka, mitego ya mauti ilinikabili. (Sheol )
Do therefore according to your wisdom, and let not his hoar head go down to the grave in peace. (Sheol )
Shughulika naye kwa kadiri ya hekima yako, lakini usiache kichwa chake chenye mvi kishukie kaburi kwa amani. (Sheol )
Now therefore hold him not guiltless: for you are a wise man, and know what you ought to do unto him; but his hoar head bring you down to the grave with blood. (Sheol )
Lakini sasa, usidhani kwamba hana hatia. Wewe ni mtu wa hekima, utajua la kumtendea. Zishushe mvi zake kaburini kwa damu.” (Sheol )
As the cloud is consumed and vanishes away: so he that goes down to the grave shall come up no more. (Sheol )
Kama vile wingu liondokavyo na kutoweka, vivyo hivyo yeye ashukaye kaburini harudi tena. (Sheol )
It is as high as heaven; what can you do? deeper than hell; what can you know? (Sheol )
Ni juu mno kuliko mbingu: waweza kufanya nini? Kina chake ni kirefu kuliko kuzimu: wewe waweza kujua nini? (Sheol )
O that you would hide me in the grave, that you would keep me secret, until your wrath be past, that you would appoint me a set time, and remember me! (Sheol )
“Laiti kama ungenificha kaburini, na kunisitiri hadi hasira yako ipite! Laiti ungeniwekea wakati, na kisha ukanikumbuka! (Sheol )
If I wait, the grave is mine house: I have made my bed in the darkness. (Sheol )
Kama nyumba pekee ninayoitarajia ni kaburi, kama nikikitandika kitanda changu gizani, (Sheol )
They shall go down to the bars of the pit, when our rest together is in the dust. (Sheol )
Je, litashuka chini hadi kwenye malango ya mauti? Je, tutashuka pamoja mavumbini?” (Sheol )
They spend their days in wealth, and in a moment go down to the grave. (Sheol )
Huitumia miaka yao katika mafanikio nao hushuka kaburini kwa amani. (Sheol )
Drought and heat consume the snow waters: so does the grave those which have sinned. (Sheol )
Kama vile joto na hari vinyakuavyo theluji iliyoyeyuka, ndivyo kuzimu kuwanyakuavyo waliotenda dhambi. (Sheol )
Hell is naked before him, and destruction has no covering. (Sheol )
Mauti iko wazi mbele za Mungu; Uharibifu haukufunikwa. (Sheol )
For in death there is no remembrance of you: in the grave who shall give you thanks? (Sheol )
Hakuna mtu anayekukumbuka akiwa amekufa. Ni nani awezaye kukusifu akiwa kuzimu? (Sheol )
The wicked shall be turned into hell, and all the nations that forget God. (Sheol )
Waovu wataishia kuzimu, naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu. (Sheol )
For you will not leave my soul in hell; neither will you suffer your Holy One to see corruption. (Sheol )
kwa maana hutaniacha kaburini, wala hutamwacha Mtakatifu Wako kuona uharibifu. (Sheol )
The sorrows of hell compassed me about: the snares of death prevented me. (Sheol )
Kamba za kuzimu zilinizunguka, mitego ya mauti ilinikabili. (Sheol )
O LORD, you have brought up my soul from the grave: you have kept me alive, that I should not go down to the pit. (Sheol )
Ee Bwana, umenitoa Kuzimu, umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti. (Sheol )
Let me not be ashamed, O LORD; for I have called upon you: let the wicked be ashamed, and let them be silent in the grave. (Sheol )
Usiniache niaibike, Ee Bwana, kwa maana nimekulilia wewe, bali waovu waaibishwe na kunyamazishwa Kuzimu. (Sheol )
Like sheep they are laid in the grave; death shall feed on them; and the upright shall have dominion over them in the morning; and their beauty shall consume in the grave from their dwelling. (Sheol )
Kama kondoo, wamewekewa kwenda kaburini, nacho kifo kitawala. Wanyofu watawatawala asubuhi, maumbile yao yataozea kaburini, mbali na majumba yao makubwa ya fahari. (Sheol )
But God will redeem my soul from the power of the grave: for he shall receive me. (Selah) (Sheol )
Lakini Mungu atakomboa uhai wangu na kaburi, hakika atanichukua kwake. (Sheol )
Let death seize upon them, and let them go down quick into hell: for wickedness is in their dwellings, and among them. (Sheol )
Kifo na kiwajie adui zangu ghafula, na washuke kuzimu wangali hai, kwa maana uovu upo ndani yao. (Sheol )
For great is your mercy toward me: and you have delivered my soul from the low hell. (Sheol )
Kwa maana upendo wako ni mkuu kwangu; umeniokoa kutoka kwenye vilindi vya kaburi. (Sheol )
For my soul is full of troubles: and my life draws nigh unto the grave. (Sheol )
Kwa maana nafsi yangu imejaa taabu, na maisha yangu yanakaribia kaburi. (Sheol )
What man is he that lives, and shall not see death? shall he deliver his soul from the hand of the grave? (Selah) (Sheol )
Ni mtu gani awezaye kuishi na asione kifo, au kujiokoa mwenyewe kutoka nguvu za kaburi? (Sheol )
The sorrows of death compassed me, and the pains of hell got hold upon me: I found trouble and sorrow. (Sheol )
Kamba za mauti zilinizunguka, maumivu makuu ya kuzimu yalinipata, nikalemewa na taabu na huzuni. (Sheol )
If I ascend up into heaven, you are there: if I make my bed in hell, behold, you are there. (Sheol )
Kama nikienda juu mbinguni, wewe uko huko; nikifanya vilindi kuwa kitanda changu, wewe uko huko. (Sheol )
Our bones are scattered at the grave's mouth, as when one cuts and cleaves wood upon the earth. (Sheol )
Watasema, “Kama mtu anavyolima na kuvunja ardhi, ndivyo mifupa yetu imetawanywa kwenye mlango wa kaburi.” (Sheol )
Let us swallow them up alive as the grave; and whole, as those that go down into the pit: (Sheol )
tuwameze wakiwa hai kama kaburi, wakiwa wazima kama wale wanaotumbukia shimoni. (Sheol )
Her feet go down to death; her steps take hold on hell. (Sheol )
Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo; hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini. (Sheol )
Her house is the way to hell, going down to the chambers of death. (Sheol )
Nyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini, ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti. (Sheol )
But he knows not that the dead are there; and that her guest are in the depths of hell. (Sheol )
Lakini hawajui hata kidogo kuwa wafu wako humo, kwamba wageni wake huyo mwanamke wako katika vilindi vya kuzimu. (Sheol )
Hell and destruction are before the LORD: how much more then the hearts of the children of men? (Sheol )
Mauti na Uharibifu viko wazi mbele za Bwana: je, si zaidi sana mioyo ya wanadamu! (Sheol )
The way of life is above to the wise, that he may depart from hell beneath. (Sheol )
Mapito ya uzima huelekea juu kwa ajili ya wenye hekima kumwepusha asiende chini kaburini. (Sheol )
You shall beat him with the rod, and shall deliver his soul from hell. (Sheol )
Mwadhibu kwa fimbo na kuiokoa nafsi yake kutoka mautini. (Sheol )
Hell and destruction are never full; so the eyes of man are never satisfied. (Sheol )
Kuzimu na Uharibifu havishibi kadhalika macho ya mwanadamu. (Sheol )
The grave; and the barren womb; the earth that is not filled with water; and the fire that says not, It is enough. (Sheol )
Ni kaburi, tumbo lisilozaa, nchi isiyoshiba maji kamwe, na moto, usiosema kamwe, ‘Yatosha!’ (Sheol )
Whatsoever your hand finds to do, do it with your might; for there is no work, nor device, nor knowledge, nor wisdom, in the grave, where you go. (Sheol )
Lolote mkono wako upatalo kufanya, fanya kwa nguvu zako zote, kwa kuwa huko kuzimu, unakokwenda, hakuna kufanya kazi wala mipango wala maarifa wala hekima. (Sheol )
Set me as a seal upon your heart, as a seal upon your arm: for love is strong as death; jealousy is cruel as the grave: the coals thereof are coals of fire, which has a most vehement flame. (Sheol )
Nitie kama muhuri moyoni mwako, kama muhuri kwenye mkono wako; kwa maana upendo una nguvu kama mauti, wivu wake ni mkatili kama kuzimu. Unachoma kama mwali wa moto, kama mwali mkubwa wa moto wa Bwana hasa. (Sheol )
Therefore hell has enlarged herself, and opened her mouth without measure: and their glory, and their multitude, and their pomp, and he that rejoices, shall descend into it. (Sheol )
Kwa hiyo kaburi limeongeza hamu yake na kupanua mdomo wake bila kikomo, ndani mwake watashuka wakuu wao na wingi wa watu, pamoja na wagomvi wao, na wafanyao sherehe wote. (Sheol )
Ask you a sign of the LORD your God; ask it either in the depth, or in the height above. (Sheol )
“Mwombe Bwana Mungu wako ishara, iwe kwenye vina virefu sana, au kwenye vimo virefu sana.” (Sheol )
Hell from beneath is moved for you to meet you at your coming: it stirs up the dead for you, even all the chief ones of the earth; it has raised up from their thrones all the kings of the nations. (Sheol )
Kuzimu kote kumetaharuki kukulaki unapokuja, kunaamsha roho za waliokufa ili kukupokea, wote waliokuwa viongozi katika ulimwengu, kunawafanya wainuke kwenye viti vyao vya kifalme: wale wote waliokuwa wafalme juu ya mataifa. (Sheol )
Your pomp is brought down to the grave, and the noise of your viols: the worm is spread under you, and the worms cover you. (Sheol )
Majivuno yako yote yameshushwa mpaka kuzimu, pamoja na kelele ya vinubi vyako, mafunza yametanda chini yako, na minyoo imekufunika. (Sheol )
Yet you shall be brought down to hell, to the sides of the pit. (Sheol )
Lakini umeshushwa chini hadi kuzimu, hadi kwenye vina vya shimo. (Sheol )
Because all of you have said, We have made a covenant with death, and with hell are we at agreement; when the overflowing scourge shall pass through, it shall not come unto us: for we have made lies our refuge, and under falsehood have we hid ourselves: (Sheol )
Ninyi mnajisifu, “Tumefanya agano na mauti, tumefanya mapatano na kuzimu. Wakati pigo lifurikalo litakapopita, haliwezi kutugusa sisi, kwa kuwa tumefanya uongo kuwa kimbilio letu na miungu ya uongo kuwa mahali petu pa kujificha.” (Sheol )
And your covenant with death shall be disannulled, and your agreement with hell shall not stand; when the overflowing scourge shall pass through, then all of you shall be trodden down by it. (Sheol )
Agano lenu na kifo litabatilishwa, patano lenu na kuzimu halitasimama. Wakati pigo lifurikalo litakapowakumba, litawaangusha chini. (Sheol )
I said in the cutting off of my days, I shall go to the gates of the grave: I am deprived of the residue of my years. (Sheol )
Nilisema, “Katika ustawi wa maisha yangu, je, ni lazima nipite katika malango ya mauti, na kupokonywa miaka yangu iliyobaki?” (Sheol )
For the grave cannot praise you, death can not celebrate you: they that go down into the pit cannot hope for your truth. (Sheol )
Kwa maana kaburi haliwezi kukusifu, mauti haiwezi kuimba sifa zako; wale washukao chini shimoni hawawezi kuutarajia uaminifu wako. (Sheol )
And you went to the king with ointment, and did increase your perfumes, and did send your messengers far off, and did debase yourself even unto hell. (Sheol )
Ulikwenda kwa Moleki ukiwa na mafuta ya zeituni, na ukaongeza manukato yako. Ukawatuma wajumbe wako mbali sana, ukashuka kwenye kaburi lenyewe! (Sheol )
Thus says the Lord GOD; In the day when he went down to the grave I caused a mourning: I covered the deep for him, and I restrained the floods thereof, and the great waters were stayed: and I caused Lebanon to mourn for him, and all the trees of the field fainted for him. (Sheol )
“‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika siku ile mwerezi uliposhushwa chini kaburini nilizifunika chemchemi zenye maji mengi kwa maombolezo: Nilivizuia vijito vyake na wingi wa maji yake nikauzuia. Kwa sababu yake niliivika Lebanoni huzuni, nayo miti yote ya shambani ikanyauka. (Sheol )
I made the nations to shake at the sound of his fall, when I cast him down to hell with them that descend into the pit: and all the trees of Eden, the choice and best of Lebanon, all that drink water, shall be comforted in the nether parts of the earth. (Sheol )
Niliyafanya mataifa yatetemeke kwa kishindo cha kuanguka kwake wakati nilipoushusha chini kaburini pamoja na wale washukao shimoni. Ndipo miti yote ya Edeni, miti iliyo bora kuliko yote na iliyo mizuri sana ya Lebanoni, miti yote ile iliyokunywa maji vizuri, ilifarijika hapa duniani. (Sheol )
They also went down into hell with him unto them that be slain with the sword; and they that were his arm, that dwelt under his shadow in the midst of the heathen. (Sheol )
Wale walioishi katika kivuli chake, wale walioungana naye miongoni mwa mataifa, nao pia walikuwa wamezikwa pamoja naye, wakiungana na wale waliouawa kwa upanga. (Sheol )
The strong among the mighty shall speak to him out of the midst of hell with them that help him: they are gone down, they lie uncircumcised, slain by the sword. (Sheol )
Kutoka kuzimu viongozi hodari watanena kuhusu Misri pamoja na wale walioungana nao, ‘Wameshuka chini, nao wamelala kimya pamoja na hao wasiotahiriwa, pamoja na wale waliouawa kwa upanga.’ (Sheol )
And they shall not lie with the mighty that are fallen of the uncircumcised, which are gone down to hell with their weapons of war: and they have laid their swords under their heads, but their iniquities shall be upon their bones, though they were the terror of the mighty in the land of the living. (Sheol )
Je, hawakulala na mashujaa wengine wasiotahiriwa waliouawa, ambao wameshuka kaburini wakiwa na silaha zao za vita, ambao panga zao ziliwekwa chini ya vichwa vyao na uovu wao juu ya mifupa yao? Adhabu kwa ajili ya dhambi zao ilikuwa juu ya mifupa yao, ingawa vitisho vya mashujaa hawa vilikuwa vimeenea hadi kwenye nchi ya walio hai. (Sheol )
I will ransom them from the power of the grave; I will redeem them from death: O death, I will be your plagues; O grave, I will be your destruction: repentance shall be hid from mine eyes. (Sheol )
“Nitawakomboa watu hawa kutoka nguvu za kaburi, nitawakomboa kutoka mautini. Yako wapi, ee mauti, mateso yako? Uko wapi, ee kuzimu, uharibifu wako? “Sitakuwa na huruma, (Sheol )
Though they dig into hell, thence shall mine hand take them; though they climb up to heaven, thence will I bring them down: (Sheol )
Wajapojichimbia chini mpaka kwenye vina vya kuzimu, kutoka huko mkono wangu utawatoa. Wajapopanda juu hadi kwenye mbingu, kutoka huko nitawashusha. (Sheol )
And said, I cried by reason of mine affliction unto the LORD, and he heard me; out of the belly of hell cried I, and you heard my voice. (Sheol )
Akasema: “Katika shida yangu nalimwita Bwana, naye akanijibu. Kutoka kina cha kaburi niliomba msaada, nawe ukasikiliza kilio changu. (Sheol )
Yea also, because he trangresses by wine, he is a proud man, neither keeps at home, who enlarges his desire as hell, and is as death, and cannot be satisfied, but gathers unto him all nations, and heaps unto him all people: (Sheol )
hakika mvinyo humsaliti; ni mwenye kiburi na hana amani. Kwa sababu ni mlafi kama kuzimu na kama kifo kamwe hatosheki; anajikusanyia mataifa yote na kuchukua watu wote mateka. (Sheol )
But I say unto you, That whosoever is angry with his brother without a cause shall be in danger of the judgment: and whosoever shall say to his brother, Raca, shall be in danger of the council: but whosoever shall say, You fool, shall be in danger of hell fire. (Geenna )
Lakini mimi nawaambia kwamba, yeyote atakayemkasirikia ndugu yake, atapaswa hukumu. Tena, yeyote atakayemwambia ndugu yake, ‘Raka,’atapaswa kujibu kwa Baraza la Wayahudi. Lakini yeyote atakayesema ‘Wewe mpumbavu!’ atapaswa hukumu ya moto wa jehanamu. (Geenna )
And if your right eye offend you, pluck it out, and cast it from you: for it is profitable for you that one of your members should perish, and not that your whole body should be cast into hell. (Geenna )
Jicho lako la kuume likikusababisha kutenda dhambi, lingʼoe ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima ukatupwa jehanamu. (Geenna )
And if your right hand offend you, cut it off, and cast it from you: for it is profitable for you that one of your members should perish, and not that your whole body should be cast into hell. (Geenna )
Kama mkono wako wa kuume ukikusababisha kutenda dhambi, ukate, uutupe mbali. Ni afadhali kwako kupoteza kiungo kimoja cha mwili wako kuliko mwili wako mzima utupwe jehanamu. (Geenna )
And fear not them which kill the body, but are not able to kill the soul: but rather fear him which is able to destroy both soul and body in hell. (Geenna )
Msiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho. Afadhali mwogopeni yeye awezaye kuiangamiza roho na mwili katika jehanamu. (Geenna )
And you, Capernaum, which are exalted unto heaven, shall be brought down to hell: for if the mighty works, which have been done in you, had been done in Sodom, it would have remained until this day. (Hadēs )
Nawe Kapernaumu, je, utainuliwa hadi mbinguni? La hasha, utashushwa mpaka kuzimu. Miujiza iliyofanyika kwako ingefanyika huko Sodoma, mji huo ungalikuwepo hadi leo. (Hadēs )
And whosoever speaks a word (logos) against the Son of man, it shall be forgiven him: but whosoever speaks against the Holy Spirit, (pneuma) it shall not be forgiven him, neither in this world, neither in the world to come. (aiōn )
Mtu yeyote atakayesema neno dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa, lakini yeyote anenaye neno dhidi ya Roho Mtakatifu hatasamehewa, iwe katika ulimwengu huu au katika ulimwengu ujao. (aiōn )
He also that received seed among the thorns is he that hears the word; (logos) and the care of this world, and the deceitfulness of riches, choke the word, (logos) and he becomes unfruitful. (aiōn )
Ile mbegu iliyopandwa katika miiba ni yule mtu alisikiaye neno, lakini masumbufu ya maisha haya na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno na kulifanya lisizae matunda. (aiōn )
The enemy that sowed them is the devil; the harvest is the end of the world; and the reapers are the angels. (aiōn )
Yule adui aliyepanda magugu ni ibilisi. Mavuno ni mwisho wa dunia, nao wavunaji ni malaika. (aiōn )
As therefore the tares are gathered and burned in the fire; so shall it be in the end of this world. (aiōn )
“Kama vile magugu yangʼolewavyo na kuchomwa motoni, ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia. (aiōn )
So shall it be at the end of the world: the angels shall come forth, and sever the wicked from among the just, (aiōn )
Hivi ndivyo itakavyokuwa wakati wa mwisho wa dunia. Malaika watakuja na kuwatenganisha watu waovu na watu wenye haki. (aiōn )
And I say also unto you, That you are Peter, and upon this rock I will build my church; and the gates of hell shall not prevail against it. (Hadēs )
Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya Kuzimu hayataweza kulishinda. (Hadēs )
Wherefore if your hand or your foot offend you, cut them off, and cast them from you: it is better for you to enter into life halt or physically disabled, rather than having two hands or two feet to be cast into everlasting fire. (aiōnios )
Ikiwa mkono wako au mguu wako unakusababisha utende dhambi, ukate na uutupe mbali. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa huna mkono mmoja au mguu mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele. (aiōnios )
And if your eye offend you, pluck it out, and cast it from you: it is better for you to enter into life with one eye, rather than having two eyes to be cast into hell fire. (Geenna )
Nalo jicho lako likikusababisha kutenda dhambi, lingʼoe, ulitupe mbali. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili lakini ukatupwa katika moto wa jehanamu. (Geenna )
And, behold, one came and said unto him, Good Master, what good thing shall I do, that I may have eternal life? (aiōnios )
Mtu mmoja akamjia Yesu na kumuuliza, “Mwalimu mwema, nifanye jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?” (aiōnios )
And every one that has forsaken houses, or brethren, or sisters, or father, or mother, or wife, or children, or lands, for my name's sake, shall receive an hundredfold, and shall inherit everlasting life. (aiōnios )
Kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu zake wa kiume au wa kike, baba au mama, watoto au mashamba kwa ajili yangu, atapokea mara mia zaidi ya hayo, na ataurithi uzima wa milele. (aiōnios )
And when he saw a fig tree in the way, he came to it, and found nothing thereon, but leaves only, and said unto it, Let no fruit grow on you henceforward for ever. And presently the fig tree withered away. (aiōn )
Akauona mtini kando ya barabara, naye akaukaribia, lakini hakupata tunda lolote ila majani. Ndipo akauambia, “Wewe usizae matunda tena kamwe!” Papo hapo ule mtini ukanyauka. (aiōn )
Woe unto you, scribes and Pharisees, hypocrites! for all of you compass sea and land to make one proselyte, and when he is made, all of you make him twofold more the child of hell than yourselves. (Geenna )
“Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo, enyi wanafiki! Ninyi mnasafiri baharini na nchi kavu ili kumfanya mtu mmoja mwongofu, lakini baada ya kumpata, mnamfanya mwana wa jehanamu mara mbili kuliko ninyi! (Geenna )
All of you serpents, all of you generation of vipers, how can all of you escape the damnation of hell? (Geenna )
“Ninyi nyoka, ninyi uzao wa nyoka wenye sumu! Mtaiepukaje hukumu ya jehanamu? (Geenna )
And as he sat upon the mount of Olives, the disciples came unto him privately, saying, Tell us, when shall these things be? and what shall be the sign of your coming, and of the end of the world? (aiōn )
Yesu alipokuwa ameketi kwenye Mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake wakamjia faraghani, wakamuuliza, “Tuambie, mambo haya yatatukia lini, nayo dalili ya kuja kwako na ya mwisho wa dunia ni gani?” (aiōn )
Then shall he say also unto them on the left hand, Depart from me, all of you cursed, into everlasting fire, prepared for the devil and his angels: (aiōnios )
“Kisha atawaambia wale walio upande wake wa kushoto, ‘Ondokeni kwangu, ninyi mliolaaniwa, nendeni kwenye moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya ibilisi na malaika zake. (aiōnios )
And these shall go away into everlasting punishment: but the righteous into life eternal. (aiōnios )
“Ndipo hawa watakapoingia kwenye adhabu ya milele, lakini wale wenye haki wataingia katika uzima wa milele.” (aiōnios )
Teaching them to observe all things whatsoever I have commanded you: and, lo, I am with you always, even unto the end of the world. Amen. (aiōn )
nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika mimi niko pamoja nanyi siku zote, hadi mwisho wa nyakati.” (aiōn )
But he that shall blaspheme against the Holy Spirit (pneuma) has never forgiveness, but is in danger of eternal damnation. (aiōn , aiōnios )
Lakini yeyote anayemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe, atakuwa na hatia ya dhambi ya milele.” (aiōn , aiōnios )
And the cares of this world, and the deceitfulness of riches, and the lusts of other things entering in, choke the word, (logos) and it becomes unfruitful. (aiōn )
lakini masumbufu ya maisha haya, na udanganyifu wa mali na tamaa ya mambo mengine huja na kulisonga lile neno na kulifanya lisizae. (aiōn )
And if your hand offend you, cut it off: it is better for you to enter into life physically disabled, than having two hands to go into hell, into the fire that never shall be quenched: (Geenna )
Kama mkono wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa na mkono mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili lakini ukaingia jehanamu, mahali ambako moto hauzimiki. [ (Geenna )
And if your foot offend you, cut it off: it is better for you to enter halt into life, than having two feet to be cast into hell, into the fire that never shall be quenched: (Geenna )
Kama mguu wako ukikusababisha kutenda dhambi, ukate. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa kiwete, kuliko kuwa na miguu miwili lakini ukaingia jehanamu. [ (Geenna )
And if your eye offend you, pluck it out: it is better for you to enter into the kingdom of God with one eye, than having two eyes to be cast into hell fire: (Geenna )
Nalo jicho lako likikusababisha kutenda dhambi, lingʼoe. Ni afadhali kwako kuingia katika Ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili lakini ukatupwa jehanamu, (Geenna )
And when he was gone forth into the way, there came one running, and kneeled to him, and asked him, Good Master, what shall I do that I may inherit eternal life? (aiōnios )
Yesu alipokuwa anaondoka, mtu mmoja akamkimbilia, akapiga magoti mbele yake, akamuuliza, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?” (aiōnios )
But he shall receive an hundredfold now in this time, houses, and brethren, and sisters, and mothers, and children, and lands, with persecutions; and in the world to come eternal life. (aiōn , aiōnios )
ambaye hatalipwa mara mia katika ulimwengu huu: nyumba, ndugu wa kiume na wa kike, mama na baba na watoto, mashamba pamoja na mateso, kisha uzima wa milele katika ulimwengu ujao. (aiōn , aiōnios )
And Jesus answered and said unto it, No man eat fruit of you hereafter for ever. And his disciples heard it. (aiōn )
Akauambia ule mti, “Tangu leo mtu yeyote asile kamwe matunda kutoka kwako.” Wanafunzi wake walimsikia akisema hayo. (aiōn )
And he shall reign over the house of Jacob for ever; and of his kingdom there shall be no end. (aiōn )
Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” (aiōn )
As he spoke to our fathers, to Abraham, and to his seed for ever. (aiōn )
Abrahamu na uzao wake milele, kama alivyowaahidi baba zetu.” (aiōn )
As he spoke by the mouth of his holy prophets, which have been since the world began: (aiōn )
kama alivyonena kwa vinywa vya manabii wake watakatifu tangu zamani, (aiōn )
And they besought him that he would not command them to go out into the deep. (Abyssos )
Wale pepo wachafu wakamsihi sana asiwaamuru kwenda katika Shimo. (Abyssos )
And you, Capernaum, which are exalted to heaven, shall be thrust down to hell. (Hadēs )
Nawe, Kapernaumu, je, utainuliwa hadi mbinguni? La hasha, utashushwa mpaka kuzimu.” (Hadēs )
And, behold, a certain lawyer stood up, and tempted him, saying, Master, what shall I do to inherit eternal life? (aiōnios )
Wakati huo mtaalamu mmoja wa sheria alisimama ili kumjaribu Yesu, akamuuliza, “Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?” (aiōnios )
But I will forewarn you whom all of you shall fear: Fear him, which after he has killed has power to cast into hell; yea, I say unto you, Fear him. (Geenna )
Lakini nitawaambia nani wa kumwogopa: Mwogopeni yule ambaye baada ya kuua mwili, ana mamlaka ya kuwatupa motoni. Naam, nawaambia, mwogopeni huyo! (Geenna )
And the lord commended the unjust steward, because he had done wisely: for the children of this world are in their generation wiser than the children of light. (aiōn )
“Yule bwana akamsifu yule msimamizi dhalimu kwa jinsi alivyotumia ujanja. Kwa maana watu wa dunia hii wana ujanja zaidi wanapojishughulisha na mambo ya dunia kuliko watu wa nuru. (aiōn )
And I say unto you, Make to yourselves friends of the mammon of unrighteousness; that, when all of you fail, they may receive you into everlasting habitations. (aiōnios )
Nawaambia, tumieni mali ya kidunia kujipatia marafiki, ili itakapokwisha, mkaribishwe katika makao ya milele. (aiōnios )
And in hell he lift up his eyes, being in torments, and sees Abraham far off, and Lazarus in his bosom. (Hadēs )
Kule kuzimu alipokuwa akiteseka, alitazama juu, akamwona Abrahamu kwa mbali, naye Lazaro alikuwa karibu yake. (Hadēs )
And a certain ruler asked him, saying, Good Master, what shall I do to inherit eternal life? (aiōnios )
Mtawala mmoja akamuuliza Yesu, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?” (aiōnios )
Who shall not receive manifold more in this present time, and in the world to come life everlasting. (aiōn , aiōnios )
ambaye hatapewa mara nyingi zaidi ya hivyo katika maisha haya, na hatimaye kupata uzima wa milele ujao.” (aiōn , aiōnios )
And Jesus answering said unto them, The children of this world marry, and are given in marriage: (aiōn )
Yesu akawajibu, “Katika maisha haya watu huoa na kuolewa. (aiōn )
But they which shall be accounted worthy to obtain that world, and the resurrection from the dead, neither marry, nor are given in marriage: (aiōn )
Lakini wale ambao wamehesabiwa kwamba wanastahili kupata nafasi katika ulimwengu ule na katika ufufuo wa wafu, hawaoi wala hawaolewi. (aiōn )
That whosoever believes in him should not perish, but have eternal life. (aiōnios )
Ili kila mtu amwaminiye awe na uzima wa milele. (aiōnios )
For God so loved the world, that he gave his only begotten Son, that whosoever believes in him should not perish, but have everlasting life. (aiōnios )
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. (aiōnios )
He that believes on the Son has everlasting life: and he that believes not the Son shall not see life; but the wrath of God abides on him. (aiōnios )
Yeyote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele, lakini yeye asiyemwamini Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake.” (aiōnios )
But whosoever drinks of the water that I shall give him shall never thirst; but the water that I shall give him shall be in him a well of water springing up into everlasting life. (aiōn , aiōnios )
Lakini yeyote anywaye maji nitakayompa hataona kiu kamwe. Maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika uzima wa milele.” (aiōn , aiōnios )
And he that reaps receives wages, and gathers fruit unto life eternal: that both he that sows and he that reaps may rejoice together. (aiōnios )
Mvunaji tayari anapokea mshahara wake, naye anakusanya mazao kwa ajili ya uzima wa milele. Ili yeye apandaye na yeye avunaye wafurahi pamoja. (aiōnios )
Verily, verily, I say unto you, He that hears my word, (logos) and believes on him that sent me, has everlasting life, and shall not come into condemnation; but is passed from death unto life. (aiōnios )
“Amin, amin nawaambia, yeyote anayesikia maneno yangu na kumwamini yeye aliyenituma, anao uzima wa milele, naye hatahukumiwa, bali amepita kutoka mautini, na kuingia uzimani. (aiōnios )
Search the scriptures; for in them all of you think all of you have eternal life: and they are they which testify of me. (aiōnios )
Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele, maandiko haya ndiyo yanayonishuhudia Mimi. (aiōnios )
Labour not for the food which perishes, but for that food which endures unto everlasting life, which the Son of man shall give unto you: for him has God the Father sealed. (aiōnios )
Msishughulikie chakula kiharibikacho, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele, ambacho Mwana wa Adamu atawapa. Yeye ndiye ambaye Mungu Baba amemtia muhuri.” (aiōnios )
And this is the will of him that sent me, that every one which sees the Son, and believes on him, may have everlasting life: and I will raise him up at the last day. (aiōnios )
Kwa maana mapenzi ya Baba yangu ni kwamba kila mmoja amtazamaye, Mwana na kumwamini awe na uzima wa milele, nami nitawafufua siku ya mwisho.” (aiōnios )
Verily, verily, I say unto you, He that believes on me has everlasting life. (aiōnios )
Amin, amin nawaambia, yeye anayeamini anao uzima wa milele. (aiōnios )
I am the living bread which came down from heaven: if any man eat of this bread, he shall live for ever: and the bread that I will give is my flesh, which I will give for the life of the world. (aiōn )
Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu yeyote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.” (aiōn )
Whoso eats my flesh, and drinks my blood, has eternal life; and I will raise him up at the last day. (aiōnios )
Mtu yeyote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. (aiōnios )
This is that bread which came down from heaven: not as your fathers did eat manna, and are dead: he that eats of this bread shall live for ever. (aiōn )
Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, si kama ule mkate baba zenu waliokula nao wakafa. Lakini yeye aulaye mkate huu ataishi milele.” (aiōn )
Then Simon Peter answered him, Lord, to whom shall we go? you have the words (rhema) of eternal life. (aiōnios )
Simoni Petro akamjibu, “Bwana, tuondoke twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. (aiōnios )
And the servant abides not in the house for ever: but the Son abides ever. (aiōn )
Mtumwa hakai nyumbani anakotumika siku zote, lakini mwana hukaa nyumbani daima. (aiōn )
Verily, verily, I say unto you, If a man keep my saying, (logos) he shall never see death. (aiōn )
Amin, amin nawaambia, mtu yeyote akilitii neno langu hataona mauti milele.” (aiōn )
Then said the Jews unto him, Now we know that you have a devil. Abraham is dead, and the prophets; and you say, If a man keep my saying, (logos) he shall never taste of death. (aiōn )
Ndipo Wayahudi wakamwambia, “Sasa tumejua kwamba una pepo mchafu. Ikiwa Abrahamu alikufa na vivyo hivyo manabii, nawe unasema ‘Mtu akitii neno langu hatakufa milele.’ (aiōn )
Since the world began was it not heard that any man opened the eyes of one that was born blind. (aiōn )
Tangu zamani hatujasikia kwamba mtu amemponya yeyote aliyezaliwa kipofu. (aiōn )
And I give unto them eternal life; and they shall never perish, neither shall any man pluck them out of my hand. (aiōn , aiōnios )
nami ninawapa uzima wa milele, hawataangamia kamwe wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka mikono yangu. (aiōn , aiōnios )
And whosoever lives and believes in me shall never die. Believe you this? (aiōn )
na yeyote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je, unasadiki haya?” (aiōn )
He that loves his life shall lose it; and he that hates his life in this world shall keep it unto life eternal. (aiōnios )
Mtu yeyote anayependa maisha yake atayapoteza, naye ayachukiaye maisha yake katika ulimwengu huu atayaokoa hata kwa uzima wa milele. (aiōnios )
The people answered him, We have heard out of the law that Christ abides for ever: and how say you, The Son of man must be lifted up? who is this Son of man? (aiōn )
Ule umati wa watu ukapiga kelele ukasema, “Tumesikia kutoka Sheria kwamba ‘Kristo adumu milele,’ wewe wawezaje kusema, ‘Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu’? Huyu ‘Mwana wa Adamu’ ni nani?” (aiōn )
And I know that his commandment is life everlasting: whatsoever I speak therefore, even as the Father said unto me, so I speak. (aiōnios )
Nami ninajua amri zake huongoza hadi kwenye uzima wa milele. Hivyo lolote nisemalo, ndilo lile Baba aliloniambia niseme.” (aiōnios )
Peter says unto him, You shall never wash my feet. Jesus answered him, If I wash you not, you have no part with me. (aiōn )
Petro akamwambia, “La, wewe hutaninawisha miguu kamwe.” Yesu akamjibu, “Kama nisipokunawisha, wewe huna sehemu nami.” (aiōn )
And I will pray the Father, and he shall give you another Comforter, that he may abide with you for ever; (aiōn )
Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele. (aiōn )
As you have given him power over all flesh, that he should give eternal life to as many as you have given him. (aiōnios )
Kwa kuwa umempa mamlaka juu ya wote wenye mwili ili awape uzima wa milele wale uliompa. (aiōnios )
And this is life eternal, that they might know you the only true God, and Jesus Christ, whom you have sent. (aiōnios )
Nao uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma. (aiōnios )
Because you will not leave my soul in hell, neither will you suffer your Holy One to see corruption. (Hadēs )
Kwa maana hutaniacha kaburini, wala hutamwacha Aliye Mtakatifu wako kuona uharibifu. (Hadēs )
He seeing this before spoke of the resurrection of Christ, that his soul was not left in hell, neither his flesh did see corruption. (Hadēs )
Daudi, akiona mambo yaliyoko mbele, akanena juu ya kufufuka kwa Kristo, kwamba hakuachwa kaburini, wala mwili wake haukuona uharibifu. (Hadēs )
Whom the heaven must receive until the times of restitution of all things, which God has spoken by the mouth of all his holy prophets since the world began. (aiōn )
Ilimpasa mbingu zimpokee mpaka wakati wa kufanywa upya kila kitu, kama Mungu alivyoahidi zamani kupitia kwa vinywa vya manabii wake watakatifu. (aiōn )
Then Paul and Barnabas waxed bold, and said, It was necessary that the word (logos) of God should first have been spoken to you: but seeing all of you put it from you, and judge yourselves unworthy of everlasting life, lo, we turn to the Gentiles. (aiōnios )
Ndipo Paulo na Barnaba wakawajibu kwa ujasiri, wakisema, “Ilitupasa kunena nanyi neno la Mungu kwanza. Lakini kwa kuwa mmelikataa, mkajihukumu wenyewe kuwa hamstahili uzima wa milele, sasa tunawageukia watu wa Mataifa. (aiōnios )
And when the Gentiles heard this, they were glad, and glorified the word (logos) of the Lord: and as many as were ordained to eternal life believed. (aiōnios )
Watu wa Mataifa waliposikia haya wakafurahi na kulitukuza neno la Bwana; nao wote waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini. (aiōnios )
Known unto God are all his works from the beginning of the world. (aiōn )
ambayo yamejulikana tangu zamani. (aiōn )
For the invisible things of him from the creation of the world are clearly seen, being understood by the things that are made, even his eternal power and Godhead; so that they are without excuse: (aïdios )
Kwa maana tangu kuumbwa kwa ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani, uweza wake wa milele na asili yake ya Uungu, imeonekana waziwazi, ikitambuliwa kutokana na yale aliyoyafanya ili wanadamu wasiwe na udhuru. (aïdios )
Who changed the truth of God into a lie, and worshipped and served the creature more than the Creator, who is blessed for ever. Amen. (aiōn )
Kwa sababu waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakaabudu na kutumikia kiumbe badala ya Muumba, ahimidiwaye milele! Amen. (aiōn )
To them who by patient continuance in well doing seek for glory and honour and immortality, eternal life: (aiōnios )
Wale ambao kwa kuvumilia katika kutenda mema hutafuta utukufu, heshima na maisha yasiyoharibika, Mungu atawapa uzima wa milele. (aiōnios )
That as sin has reigned unto death, even so might grace reign through righteousness unto eternal life by Jesus Christ our Lord. (aiōnios )
ili kwamba kama vile dhambi ilivyotawala kwa njia ya mauti, vivyo hivyo neema iweze kutawala kwa njia ya kuhesabiwa haki hata kuleta uzima wa milele katika Yesu Kristo Bwana wetu. (aiōnios )
But now being made free from sin, and become servants to God, all of you have your fruit unto holiness, and the end everlasting life. (aiōnios )
Lakini sasa kwa kuwa mmewekwa huru mbali na dhambi na mmekuwa watumwa wa Mungu, faida mnayopata ni utakatifu, ambao mwisho wake ni uzima wa milele. (aiōnios )
For the wages of sin is death; but the gift of God is eternal life through Jesus Christ our Lord. (aiōnios )
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. (aiōnios )
Whose are the fathers, and of whom as concerning the flesh Christ came, who is over all, God blessed for ever. Amen. (aiōn )
Wao ni wa uzao wa mababa wakuu wa kwanza, ambao kutoka kwao Kristo alikuja kwa jinsi ya mwili kama mwanadamu, yeye ambaye ni Mungu aliye juu ya vyote, mwenye kuhimidiwa milele! Amen. (aiōn )
Or, Who shall descend into the deep? (that is, to bring up Christ again from the dead.) (Abyssos )
“au ‘Ni nani atashuka kwenda kuzimu?’” (yaani ili kumleta Kristo kutoka kwa wafu.) (Abyssos )
For God has concluded them all in unbelief, that he might have mercy upon all. (eleēsē )
Kwa maana Mungu amewafunga wanadamu wote kwenye kuasi ili apate kuwarehemu wote. (eleēsē )
For of him, and through him, and to him, are all things: to whom be glory for ever. Amen. (aiōn )
Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake, viko kwake na kwa ajili yake. Utukufu ni wake milele! Amen. (aiōn )
And be not conformed to this world: but be all of you transformed by the renewing of your mind, that all of you may prove what is that good, and acceptable, and perfect, will of God. (aiōn )
Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kuonja na kuhakikisha ni nini mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na ukamilifu. (aiōn )
Now to him that is of power to establish you according to my gospel, and the preaching of Jesus Christ, according to the revelation of the mystery, which was kept secret since the world began, (aiōnios )
Sasa atukuzwe yeye awezaye kuwafanya ninyi imara kwa Injili yangu na kuhubiriwa kwa Yesu Kristo, kutokana na kufunuliwa siri zilizofichika tangu zamani za kale. (aiōnios )
But now is made manifest, and by the scriptures of the prophets, according to the commandment of the everlasting God, made known to all nations for the obedience of faith: (aiōnios )
Lakini sasa siri hiyo imefunuliwa na kujulikana kupitia maandiko ya kinabii kutokana na amri ya Mungu wa milele, ili mataifa yote yaweze kumwamini na kumtii (aiōnios )
To God only wise, be glory through Jesus Christ for ever. Amen. (aiōn )
Mungu aliye pekee, mwenye hekima, ambaye kwa njia ya Yesu Kristo utukufu ni wake milele na milele! Amen. (aiōn )
Where is the wise? where is the scribe? where is the disputer of this world? has not God made foolish the wisdom of this world? (aiōn )
Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi msomi? Yuko wapi mwanafalsafa wa nyakati hizi? Je, Mungu hakufanya hekima ya ulimwengu huu kuwa upumbavu? (aiōn )
Nevertheless we speak wisdom among them that are perfect: yet not the wisdom of this world, nor of the princes of this world, that come to nothing: (aiōn )
Lakini miongoni mwa watu waliokomaa twanena hekima, wala si hekima ya ulimwengu huu au ya watawala wa dunia hii wanaobatilika. (aiōn )
But we speak the wisdom of God in a mystery, even the hidden wisdom, which God ordained before the world unto our glory: (aiōn )
Sisi tunanena hekima ya Mungu ambayo ni siri, tena iliyofichika, ambayo Mungu aliikusudia kabla ya ulimwengu kuwepo, kwa ajili ya utukufu wetu. (aiōn )
Which none of the princes of this world knew: for had they known it, they would not have crucified the Lord of glory. (aiōn )
Hakuna hata mtawala mmoja wa nyakati hizi aliyeelewa jambo hili. Kwa maana kama wangelielewa, wasingemsulubisha Bwana wa utukufu. (aiōn )
Let no man deceive himself. If any man among you seems to be wise in this world, let him become a fool, that he may be wise. (aiōn )
Msijidanganye. Kama mtu yeyote miongoni mwenu akidhani kuwa ana hekima kwa viwango vya dunia hii, inampasa awe mjinga ili apate kuwa na hekima. (aiōn )
Wherefore, if food make my brother to offend, I will eat no flesh while the world stands, lest I make my brother to offend. (aiōn )
Kwa hiyo, kama kile ninachokula kitamfanya ndugu yangu aanguke katika dhambi, sitakula nyama kamwe, nisije nikamfanya ndugu yangu aanguke. (aiōn )
Now all these things happened unto them for ensamples: and they are written for our admonition, upon whom the ends of the world are come. (aiōn )
Mambo haya yote yaliwapata wao ili yawe mifano kwa wengine, nayo yaliandikwa ili yatuonye sisi ambao mwisho wa nyakati umetufikia. (aiōn )
O death, where is your sting? O grave, where is your victory? (Hadēs )
“Kuko wapi, ee mauti, kushinda kwako? Uko wapi, ee mauti, uchungu wako?” (Hadēs )
In whom the god of this world has blinded the minds of them which believe not, lest the light of the glorious gospel of Christ, who is the image of God, should shine unto them. (aiōn )
Kwa habari yao, mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Kristo, aliye sura ya Mungu. (aiōn )
For our light affliction, which is but for a moment, works for us a far more exceeding and eternal weight of glory; (aiōnios )
Kwa maana dhiki yetu nyepesi iliyo ya kitambo inatutayarisha kwa ajili ya utukufu wa milele unaozidi kuwa mwingi kupita kiasi, (aiōnios )
While we look not at the things which are seen, but at the things which are not seen: for the things which are seen are temporal; but the things which are not seen are eternal. (aiōnios )
kwa sababu hatuangalii yale yanayoweza kuonekana bali yale yasiyoweza kuonekana. Kwa maana yale yanayoweza kuonekana ni ya kitambo tu, bali yale yasiyoweza kuonekana ni ya milele. (aiōnios )
For we know that if our earthly house of this tabernacle were dissolved, we have a building of God, an house not made with hands, eternal in the heavens. (aiōnios )
Kwa maana twajua kama hema yetu ya dunia tunayoishi ikiharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu, nyumba iliyo ya milele kule mbinguni, isiyojengwa kwa mikono ya wanadamu. (aiōnios )
(As it is written, He has dispersed abroad; he has given to the poor: his righteousness remains for ever. (aiōn )
Kama ilivyoandikwa: “Ametawanya vipawa vyake kwa ukarimu akawapa maskini; haki yake hudumu milele.” (aiōn )
The God and Father of our Lord Jesus Christ, which is blessed for evermore, knows that I lie not. (aiōn )
Mungu na Baba wa Bwana Yesu, yeye ambaye anahimidiwa milele, anajua ya kuwa mimi sisemi uongo. (aiōn )
Who gave himself for our sins, that he might deliver us from this present evil world, according to the will of God and our Father: (aiōn )
aliyejitoa kwa ajili ya dhambi zetu ili apate kutuokoa katika ulimwengu huu wa sasa ulio mbaya, sawasawa na mapenzi yake yeye aliye Mungu na Baba yetu. (aiōn )
To whom be glory for ever and ever. Amen. (aiōn )
Utukufu una yeye milele na milele. Amen. (aiōn )
For he that sows to his flesh shall of the flesh reap corruption; but he that sows to the Spirit (pneuma) shall of the Spirit (pneuma) reap life everlasting. (aiōnios )
Apandaye kwa mwili, katika mwili wake atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye katika Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. (aiōnios )
Far above all principality, and power, and might, and dominion, and every name that is named, not only in this world, but also in that which is to come: (aiōn )
juu sana kuliko falme zote na mamlaka, enzi na milki, na juu ya kila jina litajwalo, si katika ulimwengu huu tu, bali katika ule ujao pia. (aiōn )
Wherein in time past all of you walked according to the course of this world, according to the prince of the power of the air, the spirit (pneuma) that now works in the children of disobedience: (aiōn )
ambazo mlizitenda mlipofuatisha namna ya ulimwengu huu na za yule mtawala wa ufalme wa anga, yule roho atendaye kazi sasa ndani ya wale wasiotii. (aiōn )
That in the ages to come he might show the exceeding riches of his grace in his kindness toward us through Christ Jesus. (aiōn )
ili katika ule ulimwengu ujao apate kuonyesha wingi wa neema yake isiyopimika, iliyodhihirishwa kwetu kwa wema wake ndani ya Kristo Yesu. (aiōn )
And to make all men see what is the fellowship of the mystery, which from the beginning of the world has been hid in God, who created all things by Jesus Christ: (aiōn )
na kuweka wazi kwa kila mtu siri hii iliyokuwa imefichwa tangu zamani katika Mungu, aliyeumba vitu vyote. (aiōn )
According to the eternal purpose which he purposed in Christ Jesus our Lord: (aiōn )
sawasawa na kusudi lake la milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. (aiōn )
Unto him be glory in the church by Christ Jesus throughout all ages, world without end. Amen. (aiōn )
yeye atukuzwe katika kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote, milele na milele. Amen. (aiōn )
For we wrestle not against flesh and blood, but against principalities, against powers, against the rulers of the darkness of this world, against spiritual wickedness in high places. (aiōn )
Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. (aiōn )
Now unto God and our Father be glory for ever and ever. Amen. (aiōn )
Mungu wetu aliye Baba yetu apewe utukufu milele na milele. Amen. (aiōn )
Even the mystery which has been hid from ages and from generations, but now is made manifest to his saints: (aiōn )
Hii ni siri iliyokuwa imefichika tangu zamani na kwa vizazi vingi, lakini sasa imefunuliwa kwa watakatifu. (aiōn )
Who shall be punished with everlasting destruction from the presence of the Lord, and from the glory of his power; (aiōnios )
Wataadhibiwa kwa uangamivu wa milele na kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa uweza wake, (aiōnios )
Now our Lord Jesus Christ himself, and God, even our Father, which has loved us, and has given us everlasting consolation and good hope through grace, (aiōnios )
Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe na Mungu Baba yetu, aliyetupenda na kwa neema yake akatupatia faraja ya milele na tumaini jema, (aiōnios )
Nevertheless for this cause I obtained mercy, that in me first Jesus Christ might show forth all longsuffering, for a pattern to them which should hereafter believe on him to life everlasting. (aiōnios )
Lakini kwa sababu hiyo nilipata rehema, ili katika mimi, niliyekuwa mwenye dhambi kuliko wote, Kristo Yesu apate kuonyesha uvumilivu wake usio na kikomo, ili niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini na wapate uzima wa milele. (aiōnios )
Now unto the King eternal, immortal, invisible, the only wise God, be honour and glory for ever and ever. Amen. (aiōn )
Basi Mfalme wa milele, asiye na mwisho, asiyeonekana, aliye Mungu pekee, apewe heshima na utukufu milele na milele. Amen. (aiōn )
Fight the good fight of faith, lay hold on eternal life, unto which you are also called, and have professed a good profession before many witnesses. (aiōnios )
Pigana vile vita vizuri vya imani. Shika uzima wa milele ambao ndio ulioitiwa ulipokiri ule ukiri mzuri mbele ya mashahidi wengi. (aiōnios )
Who only has immortality, dwelling in the light which no man can approach unto; whom no man has seen, nor can see: to whom be honour and power everlasting. Amen. (aiōnios )
yeye peke yake ambaye hapatikani na mauti, na anakaa katika nuru isiyoweza kukaribiwa, ambaye hakuna mwanadamu aliyemwona wala awezaye kumwona. Heshima na uweza una yeye milele. Amen. (aiōnios )
Charge them that are rich in this world, that they be not high-minded, nor trust in uncertain riches, but in the living God, who gives us richly all things to enjoy; (aiōn )
Waagize wale ambao ni matajiri wa ulimwengu huu waache kujivuna, wala wasiweke tumaini lao katika mali ambayo si ya hakika, bali waweke tumaini lao katika Mungu ambaye hutupatia vitu vyote kwa wingi ili tuvifurahie. (aiōn )
Who has saved us, and called us with an holy calling, not according to our works, but according to his own purpose and grace, which was given us in Christ Jesus before the world began, (aiōnios )
ambaye alituokoa na kutuita katika mwito mtakatifu: si kwa kadiri ya matendo yetu mema bali kwa sababu ya kusudi lake mwenyewe na neema yake. Neema hii tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele. (aiōnios )
Therefore I endure all things for the elect's sakes, that they may also obtain the salvation which is in Christ Jesus with eternal glory. (aiōnios )
Kwa hiyo ninavumilia mambo yote kwa ajili ya wateule wa Mungu, kusudi wao nao wapate wokovu ulio katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele. (aiōnios )
For Demas has forsaken me, having loved this present world, and is departed unto Thessalonica; Crescens to Galatia, Titus unto Dalmatia. (aiōn )
kwa sababu Dema, kwa kuupenda ulimwengu, ameniacha na amekwenda Thesalonike. Kreske amekwenda Galatia na Tito amekwenda Dalmatia. (aiōn )
And the Lord shall deliver me from every evil work, and will preserve me unto his heavenly kingdom: to whom be glory for ever and ever. Amen. (aiōn )
Bwana ataniokoa katika kila shambulio baya na kunileta salama katika Ufalme wake wa mbinguni. Atukuzwe yeye milele na milele. Amen. (aiōn )
In hope of eternal life, which God, that cannot lie, promised before the world began; (aiōnios )
imani na ujuzi ulioko katika tumaini la uzima wa milele, ambao Mungu, asiyesema uongo, aliahidi hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, (aiōnios )
Teaching us that, denying ungodliness and worldly lusts, we should live soberly, righteously, and godly, in this present world; (aiōn )
Nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, ili tupate kuishi maisha ya kiasi, ya haki na ya utaua katika ulimwengu huu wa sasa, (aiōn )
That being justified by his grace, we should be made heirs according to the hope of eternal life. (aiōnios )
ili kwamba, tukiisha kuhesabiwa haki kwa neema yake, tupate kuwa warithi tukiwa na tumaini la uzima wa milele. (aiōnios )
For perhaps he therefore departed for a season, that you should receive him for ever; (aiōnios )
Huenda sababu ya yeye kutengwa nawe kwa kitambo kidogo ni ili uwe naye daima. (aiōnios )
Has in these last days spoken unto us by his Son, whom he has appointed heir of all things, by whom also he made the worlds; (aiōn )
lakini katika siku hizi za mwisho anasema nasi kwa njia ya Mwanawe, ambaye amemweka kuwa mrithi wa vitu vyote, na ambaye kupitia kwake aliuumba ulimwengu. (aiōn )
But unto the Son he says, Your throne, O God, is for ever and ever: a sceptre of righteousness is the sceptre of your kingdom. (aiōn )
Lakini kwa habari za Mwana asema, “Kiti chako cha enzi, Ee Mungu, kitadumu milele na milele, nayo haki itakuwa fimbo ya utawala ya ufalme wako. (aiōn )
As he says also in another place, You are a priest for ever after the order of Melchisedec. (aiōn )
Pia mahali pengine asema, “Wewe ni kuhani milele, kwa mfano wa Melkizedeki.” (aiōn )
And being made perfect, he became the author of eternal salvation unto all them that obey him; (aiōnios )
na akiisha kukamilishwa, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii. (aiōnios )
Of the doctrine of baptisms, and of laying on of hands, and of resurrection of the dead, and of eternal judgment. (aiōnios )
mafundisho kuhusu aina za ubatizo, kuwekea watu mikono, ufufuo wa wafu, na hukumu ya milele. (aiōnios )
And have tasted the good word (rhema) of God, and the powers of the world to come, (aiōn )
ambao wameonja uzuri wa Neno la Mungu na nguvu za wakati ujao, (aiōn )
Where the forerunner is for us entered, even Jesus, made an high priest for ever after the order of Melchisedec. (aiōn )
mahali ambapo Yesu mtangulizi wetu aliingia kwa niaba yetu. Yeye amekuwa Kuhani Mkuu milele, kwa mfano wa Melkizedeki. (aiōn )
For he testifies, You are a priest for ever after the order of Melchisedec. (aiōn )
Kwa maana imeshuhudiwa kwamba: “Wewe ni kuhani milele, kwa mfano wa Melkizedeki.” (aiōn )
(For those priests were made without an oath; but this with an oath by him that said unto him, The Lord swore and will not repent, You are a priest for ever after the order of Melchisedec: ) (aiōn )
lakini Yesu alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alimwambia: “Bwana ameapa naye hatabadilisha mawazo yake: ‘Wewe ni kuhani milele.’” (aiōn )
But this man, because he continues ever, has an unchangeable priesthood. (aiōn )
Lakini kwa sababu Yesu anaishi milele, anao ukuhani wa kudumu. (aiōn )
For the law makes men high priests which have infirmity; but the word (logos) of the oath, which was since the law, makes the Son, who is consecrated for evermore. (aiōn )
Kwa kuwa sheria huwaweka makuhani wakuu watu ambao ni dhaifu; lakini lile neno la kiapo, lililokuja baada ya sheria, lilimweka Mwana, ambaye amefanywa kuwa mkamilifu milele. (aiōn )
Neither by the blood of goats and calves, but by his own blood he entered in once into the holy place, having obtained eternal redemption for us. (aiōnios )
Hakuingia kwa njia ya damu ya mbuzi na ya ndama; lakini aliingia Patakatifu pa Patakatifu mara moja tu kwa damu yake mwenyewe, akiisha kupata ukombozi wa milele. (aiōnios )
How much more shall the blood of Christ, who through the eternal Spirit (pneuma) offered himself without spot to God, purge your conscience from dead works to serve the living God? (aiōnios )
Basi ni zaidi aje damu ya Kristo, ambaye kwa Roho wa milele alijitoa nafsi yake kwa Mungu kuwa sadaka isiyo na waa, itatusafisha dhamiri zetu kutokana na matendo yaletayo mauti, ili tupate kumtumikia Mungu aliye hai! (aiōnios )
And for this cause he is the mediator of the new testament, that by means of death, for the redemption of the transgressions that were under the first testament, they which are called might receive the promise of eternal inheritance. (aiōnios )
Kwa sababu hii Kristo ni mpatanishi wa agano jipya, ili kwamba wale walioitwa waweze kupokea ile ahadi ya urithi wa milele: kwa vile yeye alikufa awe ukombozi wao kutoka kwa dhambi walizozitenda chini ya agano la kwanza. (aiōnios )
For then must he often have suffered since the foundation of the world: but now once in the end of the world has he appeared to put away sin by the sacrifice of himself. (aiōn )
Ingekuwa hivyo, ingempasa Kristo kuteswa mara nyingi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Lakini sasa ametokea mara moja tu katika mwisho wa nyakati aiondoe dhambi kwa kujitoa mwenyewe kuwa dhabihu. (aiōn )
Through faith we understand that the worlds were framed by the word (rhema) of God, so that things which are seen were not made of things which do appear. (aiōn )
Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, vitu vyote vinavyoonekana havikuumbwa kutoka kwa vitu vinavyoonekana. (aiōn )
Jesus Christ the same yesterday, and to day, and for ever. (aiōn )
Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo na hata milele. (aiōn )
Now the God of peace, that brought again from the dead our Lord Jesus, that great shepherd of the sheep, through the blood of the everlasting covenant, (aiōnios )
Basi Mungu wa amani, ambaye kwa damu ya Agano la milele alimleta tena kutoka kwa wafu Bwana wetu Yesu, yule Mchungaji Mkuu wa kondoo, (aiōnios )
Make you perfect in every good work to do his will, working in you that which is well-pleasing in his sight, through Jesus Christ; to whom be glory for ever and ever. Amen. (aiōn )
awafanye ninyi wakamilifu mkiwa mmekamilishwa katika kila jambo jema ili mpate kutenda mapenzi yake, naye atende ndani yetu kile kinachompendeza machoni Pake, kwa njia ya Yesu Kristo, ambaye utukufu una yeye milele na milele. Amen. (aiōn )
And the tongue is a fire, a world of iniquity: so is the tongue among our members, that it defiles the whole body, and sets on fire the course of nature; and it is set on fire of hell. (Geenna )
Ulimi pia ni moto, ndio ulimwengu wa uovu kati ya viungo vya mwili. Ulimi huutia mwili wote wa mtu unajisi na kuuwasha moto mfumo mzima wa maisha yake, nao wenyewe huchomwa moto wa jehanamu. (Geenna )
Being born again, not of corruptible seed, but of incorruptible, by the word (logos) of God, which lives and abides for ever. (aiōn )
Kwa maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu ile iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika, kupitia kwa neno la Mungu lililo hai na linalodumu milele. (aiōn )
But the word (rhema) of the Lord endures for ever. And this is the word (rhema) which by the gospel is preached unto you. (aiōn )
lakini neno la Bwana ladumu milele.” Hili ndilo neno lililohubiriwa kwenu. (aiōn )
If any man speak, let him speak as the oracles of God; if any man minister, let him do it as of the ability which God gives: that God in all things may be glorified through Jesus Christ, to whom be praise and dominion for ever and ever. Amen. (aiōn )
Yeyote asemaye hana budi kusema kama mtu asemaye maneno ya Mungu mwenyewe. Yeyote ahudumuye hana budi kuhudumu kwa nguvu zile anazopewa na Mungu, ili Mungu apate kutukuzwa katika mambo yote kwa njia ya Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye milele na milele. Amen. (aiōn )
But the God of all grace, who has called us unto his eternal glory by Christ Jesus, after that all of you have suffered a while, make you perfect, establish, strengthen, settle you. (aiōnios )
Nanyi mkiisha kuteswa kwa kitambo kidogo, Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele ndani ya Kristo, yeye mwenyewe atawarejesha na kuwatia nguvu, akiwaimarisha na kuwathibitisha. (aiōnios )
To him be glory and dominion for ever and ever. Amen. (aiōn )
Uweza una yeye milele na milele. Amen. (aiōn )
For so an entrance shall be ministered unto you abundantly into the everlasting kingdom of our Lord and Saviour Jesus Christ. (aiōnios )
na mtajaliwa kwa ukarimu mwingi kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. (aiōnios )
For if God spared not the angels that sinned, but cast them down to hell, and delivered them into chains of darkness, to be reserved unto judgment; (Tartaroō )
Kwa maana, kama Mungu hakuwasamehe malaika walipotenda dhambi, bali aliwatupa kuzimu katika vifungo vya giza wakae humo mpaka ije hukumu; (Tartaroō )
But grow in grace, and in the knowledge of our Lord and Saviour Jesus Christ. To him be glory both now and for ever. Amen. (aiōn )
Bali kueni katika neema na katika kumjua Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na milele! Amen. (aiōn )
(For the life was manifested, and we have seen it, and bear witness, and show unto you that eternal life, which was with the Father, and was manifested unto us; ) (aiōnios )
Uzima huo ulidhihirishwa; nasi tumeuona na kuushuhudia, nasi twawatangazia uzima wa milele, ambao ulikuwa pamoja na Baba, nao ukadhihirishwa kwetu. (aiōnios )
And the world passes away, and the lust thereof: but he that does the will of God abides for ever. (aiōn )
Nao ulimwengu unapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu milele. (aiōn )
And this is the promise that he has promised us, even eternal life. (aiōnios )
Hii ndiyo ahadi yake kwetu, yaani, uzima wa milele. (aiōnios )
Whosoever hates his brother is a murderer: and all of you know that no murderer has eternal life abiding in him. (aiōnios )
Yeyote amchukiaye ndugu yake ni muuaji, nanyi mwajua ya kwamba muuaji hana uzima wa milele ndani yake. (aiōnios )
And this is the record, that God has given to us eternal life, and this life is in his Son. (aiōnios )
Huu ndio ushuhuda: kwamba Mungu ametupa uzima wa milele, nao huo uzima umo katika Mwanawe. (aiōnios )
These things have I written unto you that believe on the name of the Son of God; that all of you may know that all of you have eternal life, and that all of you may believe on the name of the Son of God. (aiōnios )
Nawaandikia mambo haya ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu ili mpate kujua ya kuwa mnao uzima wa milele. (aiōnios )
And we know that the Son of God has come, and has given us an understanding, that we may know him that is true, and we are in him that is true, even in his Son Jesus Christ. This is the true God, and eternal life. (aiōnios )
Nasi pia twajua ya kwamba Mwana wa Mungu amekuja, naye ametupa sisi ufahamu ili tupate kumjua yeye aliye Kweli. Nasi tumo ndani yake yeye aliye Kweli, yaani, ndani ya Yesu Kristo Mwanawe. Yeye ndiye Mungu wa kweli na uzima wa milele. (aiōnios )
For the truth's sake, which dwells in us, and shall be with us for ever. (aiōn )
kwa sababu ya ile kweli ikaayo ndani yetu na ambayo itaendelea kukaa nasi milele: (aiōn )
And the angels which kept not their first estate, but left their own habitation, he has reserved in everlasting chains under darkness unto the judgment of the great day. (aïdios )
Nao malaika ambao hawakulinda nafasi zao, lakini wakayaacha makao yao, hawa amewaweka katika giza, wakiwa wamefungwa kwa minyororo ya milele kwa ajili ya hukumu Siku ile kuu. (aïdios )
Even as Sodom and Gomorrha, and the cities about them in like manner, giving themselves over to fornication, and going after strange flesh, are set forth for an example, suffering the vengeance of eternal fire. (aiōnios )
Vivyo hivyo, Sodoma na Gomora na pia ile miji iliyokuwa kandokando, ambayo kwa jinsi moja na hao, walijifurahisha kwa uasherati na kufuata tamaa za mwili zisizo za asili, waliwekwa wawe mfano kwa kuadhibiwa katika moto wa milele. (aiōnios )
Raging waves of the sea, foaming out their own shame; wandering stars, to whom is reserved the blackness of darkness for ever. (aiōn )
Wao ni mawimbi makali ya bahari, yakitoa povu la aibu yao wenyewe, ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba waliowekewa milele. (aiōn )
Keep yourselves in the love (agape) of God, looking for the mercy of our Lord Jesus Christ unto eternal life. (aiōnios )
Jilindeni katika upendo wa Mungu mkitazamia kwa furaha rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo ili awalete katika uzima wa milele. (aiōnios )
To the only wise God our Saviour, be glory and majesty, dominion and power, both now and ever. Amen. (aiōn )
kwake yeye Mungu pekee Mwokozi wetu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu, utukufu, ukuu, uweza na mamlaka ni vyake tangu milele, sasa na hata milele! Amen. (aiōn )
And has made us kings and priests unto God and his Father; to him be glory and dominion for ever and ever. Amen. (aiōn )
akatufanya sisi kuwa ufalme na makuhani, tumtumikie Mungu wake ambaye ni Baba yake. Utukufu na uwezo ni vyake milele na milele! Amen. (aiōn )
I am he that lives, and was dead; and, behold, I am alive for evermore, Amen; and have the keys of hell and of death. (aiōn , Hadēs )
Mimi ni Yeye Aliye Hai, niliyekuwa nimekufa, na tazama, ni hai milele na milele! Nami ninazo funguo za mauti na kuzimu. (aiōn , Hadēs )
And when those beasts give glory and honour and thanks to him that sat on the throne, who lives for ever and ever, (aiōn )
Kila mara viumbe hao wanne wenye uhai wanapomtukuza, kumheshimu na kumshukuru yeye aketiye kwenye kile kiti cha enzi, tena aishiye milele na milele, (aiōn )
The four and twenty elders fall down before him that sat on the throne, and worship him that lives for ever and ever, and cast their crowns before the throne, saying, (aiōn )
wale wazee ishirini na wanne huanguka mbele zake aketiye kwenye kiti cha enzi na kumwabudu yeye aliye hai milele na milele. Huziweka taji zao mbele ya kiti cha enzi, wakisema: (aiōn )
And every creature which is in heaven, and on the earth, and under the earth, and such as are in the sea, and all that are in them, heard I saying, Blessing, and honour, and glory, and power, be unto him that sits upon the throne, and unto the Lamb for ever and ever. (aiōn )
Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, chini ya nchi na baharini na vyote vilivyomo ndani yake vikiimba: “Sifa na heshima na utukufu na uweza ni vyake yeye aketiye juu ya hicho kiti cha enzi na kwa Mwana-Kondoo, milele na milele!” (aiōn )
And I looked, and behold a pale horse: and his name that sat on him was Death, and Hell followed with him. And power was given unto them over the fourth part of the earth, to kill with sword, and with hunger, and with death, and with the beasts of the earth. (Hadēs )
Nikatazama, na hapo mbele yangu alikuwepo farasi mwenye rangi ya kijivujivu! Yeye aliyempanda aliitwa Mauti, naye Kuzimu alikuwa akimfuata nyuma yake kwa karibu. Wakapewa mamlaka juu ya robo ya dunia, kuua kwa upanga, njaa, tauni na kwa wanyama wakali wa dunia. (Hadēs )
Saying, Amen: Blessing, and glory, and wisdom, and thanksgiving, and honour, and power, and might, be unto our God for ever and ever. Amen. (aiōn )
wakisema: “Amen! Sifa na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu viwe kwa Mungu wetu milele na milele. Amen!” (aiōn )
And the fifth angel sounded, and I saw a star fall from heaven unto the earth: and to him was given the key of the bottomless pit. (Abyssos )
Malaika wa tano akaipiga tarumbeta yake, nami nikaona nyota iliyokuwa imeanguka toka angani hadi ardhini. Nyota hiyo ilipewa ufunguo wa lile Shimo. (Abyssos )
And he opened the bottomless pit; and there arose a smoke out of the pit, as the smoke of a great furnace; and the sun and the air were darkened by reason of the smoke of the pit. (Abyssos )
Alipolifungua hilo Shimo, moshi ukapanda kutoka humo kama moshi wa tanuru kubwa sana. Jua na anga vikatiwa giza na ule moshi uliotoka katika hilo Shimo. (Abyssos )
And they had a king over them, which is the angel of the bottomless pit, whose name in the Hebrew tongue is Abaddon, but in the Greek tongue has his name Apollyon. (Abyssos )
Walikuwa na mfalme wao, ambaye ni malaika wa lile Shimo, ambaye jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kiyunani ni Apolioni. (Abyssos )
And swore by him that lives for ever and ever, who created heaven, and the things that therein are, and the earth, and the things that therein are, and the sea, and the things which are therein, that there should be time no longer: (aiōn )
Naye akaapa kwa Yule aishiye milele na milele, aliyeumba mbingu na vyote vilivyomo, dunia na vyote viijazavyo, pamoja na bahari na vyote vilivyomo ndani yake, akasema, “Hakuna kungoja tena! (aiōn )
And when they shall have finished their testimony, the beast that ascends out of the bottomless pit shall make war against them, and shall overcome them, and kill them. (Abyssos )
Basi watakapokuwa wamemaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika lile Shimo atapigana nao vita, atawashinda na kuwaua. (Abyssos )
And the seventh angel sounded; and there were great voices in heaven, saying, The kingdoms of this world are become the kingdoms of our Lord, and of his Christ; and he shall reign for ever and ever. (aiōn )
Yule malaika wa saba akaipiga tarumbeta yake, pakawa na sauti kubwa mbinguni iliyosema: “Ufalme wa ulimwengu umekuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atatawala milele na milele.” (aiōn )
And I saw another angel fly in the midst of heaven, having the everlasting gospel to preach unto them that dwell on the earth, and to every nation, and kindred, and tongue, and people, (aiōnios )
Kisha nikamwona malaika mwingine akiruka juu angani, naye alikuwa na Injili ya milele ya kuwatangazia wale waishio duniani, yaani, kwa kila taifa, kabila, lugha na jamaa. (aiōnios )
And the smoke of their torment ascends up for ever and ever: and they have no rest day nor night, who worship the beast and his image, and whosoever receives the mark of his name. (aiōn )
Nao moshi wa mateso yao hupanda juu milele na milele. Hakuna mapumziko, mchana wala usiku, kwa wale wamwabuduo huyo mnyama na sanamu yake, au kwa yeyote anayepokea chapa ya jina lake.” (aiōn )
And one of the four beasts gave unto the seven angels seven golden vials full of the wrath of God, who lives for ever and ever. (aiōn )
Ndipo mmoja wa wale viumbe wanne wenye uhai akawapa wale malaika saba mabakuli saba ya dhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu, yeye aishiye milele na milele. (aiōn )
The beast that you saw was, and is not; and shall ascend out of the bottomless pit, and go into perdition: and they that dwell on the earth shall wonder, whose names were not written in the book of life from the foundation of the world, when they behold the beast that was, and is not, and yet is. (Abyssos )
Huyo mnyama ambaye ulimwona, wakati fulani alikuwepo, lakini sasa hayupo, naye atapanda kutoka lile Shimo na kwenda kwenye maangamizo yake. Watu waishio duniani ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima tangu kuumbwa kwa ulimwengu watastaajabu kumwona huyo mnyama, kwa maana alikuwepo wakati fulani, na sasa hayupo, lakini atakuwepo. (Abyssos )
And again they said, Alleluia And her smoke rose up for ever and ever. (aiōn )
Wakasema tena kwa nguvu: “Haleluya! Moshi wake huyo kahaba unapanda juu milele na milele.” (aiōn )
And the beast was taken, and with him the false prophet that wrought miracles before him, with which he deceived them that had received the mark of the beast, and them that worshipped his image. These both were cast alive into a lake of fire burning with brimstone. (Limnē Pyr )
Lakini yule mnyama akakamatwa pamoja na huyo nabii wa uongo ambaye alikuwa amefanya ishara kwa niaba ya huyo mnyama, ambaye kwa ishara hizi aliwadanganya wale waliopokea chapa ya huyo mnyama na kuiabudu sanamu yake. Hawa wawili wakatupwa wakiwa hai ndani ya ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti. (Limnē Pyr )
And I saw an angel come down from heaven, having the key of the bottomless pit and a great chain in his hand. (Abyssos )
Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, akiwa ameshika ufunguo wa lile Shimo na mnyororo mkubwa mkononi mwake. (Abyssos )
And cast him into the bottomless pit, and shut him up, and set a seal upon him, that he should deceive the nations no more, till the thousand years should be fulfilled: and after that he must be loosed a little season. (Abyssos )
Akamtupa katika lile Shimo, akamfunga humo na kulitia lakiri, ili kumzuia asiendelee kudanganya mataifa mpaka hiyo miaka 1,000 itimie. Baada ya hayo lazima afunguliwe kwa muda mfupi. (Abyssos )
And the devil that deceived them was cast into the lake of fire and brimstone, where the beast and the false prophet are, and shall be tormented day and night for ever and ever. (aiōn , Limnē Pyr )
Naye ibilisi aliyewadanganya akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti walikokuwa wametupwa yule mnyama na yule nabii wa uongo. Watateswa humo usiku na mchana, milele na milele. (aiōn , Limnē Pyr )
And the sea gave up the dead which were in it; and death and hell delivered up the dead which were in them: and they were judged every man according to their works. (Hadēs )
Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake, nayo mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Kila mtu akahukumiwa kulingana na yale aliyoyatenda. (Hadēs )
And death and hell were cast into the lake of fire. This is the second death. (Hadēs , Limnē Pyr )
Kisha mauti na Kuzimu zikatupwa katika ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. (Hadēs , Limnē Pyr )
And whosoever was not found written in the book of life was cast into the lake of fire. (Limnē Pyr )
Iwapo mtu jina lake halikuonekana katika kile kitabu cha uzima, alitupwa ndani ya lile ziwa la moto. (Limnē Pyr )
But the fearful, and unbelieving, and the abominable, and murderers, and whoremongers, and sorcerers, and idolaters, and all liars, shall have their part in the lake which burns with fire and brimstone: which is the second death. (Limnē Pyr )
Lakini waoga, wasioamini, wachafu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, pamoja na waongo wote, mahali pao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.” (Limnē Pyr )
And there shall be no night there; and they need no candle, neither light of the sun; for the Lord God gives them light: and they shall reign for ever and ever. (aiōn )
Usiku hautakuwako tena, wala hawatahitaji mwanga wa taa au wa jua, kwa maana Bwana Mungu atakuwa nuru yao, nao watatawala milele na milele. (aiōn )
These are wells without water, clouds that are carried with a tempest; to whom the mist of darkness is reserved for ever. ()