< 民數記 29 >

1 「七月初一日,你們當有聖會;甚麼勞碌的工都不可做,是你們當守為吹角的日子。
Katika siku ya kwanza, ya mwezi wa saba, mtakuwa na kusanyiko takatifu la kumwabudu BWANA. Katika siku hiyo hamtafanya kazi zenu za kila siku. Itakuwa siku ya kupiga matarumbeta.
2 你們要將公牛犢一隻,公綿羊一隻,沒有殘疾、一歲的公羊羔七隻,作為馨香的燔祭獻給耶和華。
Mtatoa sadaka ya kuteketezwa ya kufanya harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa sadaka ya fahari mchanga, kondoo dume mmoja na wanakondoo dume saba wa mwaka mmoja, kila mmoja mkamilifu.
3 同獻的素祭用調油的細麵;為一隻公牛要獻伊法十分之三;為一隻公羊要獻伊法十分之二;
Pamoja na hao mtatoa sadaka ya unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu tatu za kumi za efa kwa ajili ya huyo fahari, sehemu mbili za kumi kwa ajili ya huyo kondoo mume,
4 為那七隻羊羔,每隻要獻伊法十分之一。
na sehemu ya kumi ya kila hao wanakondoo waume saba.
5 又獻一隻公山羊作贖罪祭,為你們贖罪。
Na mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.
6 這些是在月朔的燔祭和同獻的素祭,並常獻的燔祭與同獻的素祭,以及照例同獻的奠祭以外,都作為馨香的火祭獻給耶和華。」
Toeni hizo sadaka katika mwezi wa saba kama nyongeza ya sadaka mtakazotoa kila mwanzo wa kila mwezi: pamoja na sadaka maalumu za kuteketezwa na sadaka za unga. Hizi zitakuwa nyongeza za sadaka za kuteketezwa za kila siku, na sadaka zake za unga, na sadaka zake za vinywaji. Utakapokuwa ukiendelea na sadaka hizi, utakuwa ukitii kile kilichoamriwa kutoa harufu nzuri, sadaka iliyotengenezwa kwa moto kwa BWANA.
7 「七月初十日,你們當有聖會;要刻苦己心,甚麼工都不可做。
Siku ya kumi ya mwezi wa saba, mtakuwa na kusanyiko takatifu la kumwabudu BWANA. Mtajinyeneyekeza na hamtafanya kazi.
8 只要將公牛犢一隻,公綿羊一隻,一歲的公羊羔七隻,都要沒有殘疾的,作為馨香的燔祭獻給耶和華。
Mtatoa sadaka ya kuteketezwa ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa fahari mmoja mchanga ili kutoa harufu nzuri, kondoo mmoja mume, na wanakondoo saba waume wa mwaka mmoja. Wote wakamilifu.
9 同獻的素祭用調油的細麵:為一隻公牛要獻伊法十分之三;為一隻公羊要獻伊法十分之二;
Pamoja na sadaka hizo utatoa sadaka ya unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu tatu za kumi za efa kwa ajili ya fahari, sehemu mbili za kumi za kondoo dume mmoja,
10 為那七隻羊羔,每隻要獻伊法十分之一。
na sehemu ya kumi ya efa moja kwa kila mwanakondoo wale saba.
11 又獻一隻公山羊為贖罪祭。這是在贖罪祭和常獻的燔祭,與同獻的素祭並同獻的奠祭以外。」
Mtatatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya upatanisho. Hii itakuwa sadaka ya nyongeza ya upatanisho, ya sadaka ya kila siku ya kuteketezwa, pamoja na sadaka za unga, na sadaka zake za vinywaji.
12 「七月十五日,你們當有聖會;甚麼勞碌的工都不可做,要向耶和華守節七日。
Siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtakuwa na kusanyiko takatifu lakumwabudu BWANA. Siku hiyo hamtafanya kazi za kila siku, na mtazitunza hizo sikukuu kwa muda wa siku saba kwa ajili ya BWANA.
13 又要將公牛犢十三隻,公綿羊兩隻,一歲的公羊羔十四隻,都要沒有殘疾的,用火獻給耶和華為馨香的燔祭。
Mtatoa sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotengenezwa kwa moto ilikutoa harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa mafahari wachanga kumi na tatu, kondoo waume wawili, na wanakondoo waume kumi na nne wa mwaka mmoja. Wote wakamilifu.
14 同獻的素祭用調油的細麵;為那十三隻公牛,每隻要獻伊法十分之三;為那兩隻公羊,每隻要獻伊法十分之二;
Pamoja na hao mtatoa sadaka ya unga, unga mwembaba uliochanganywa na mafuta, sehemu tatu za kumi za efa kwa kila fahari katika hao kumi na tatu, sehemu mbili za kumi kwa kila hao kondoo dume wawili,
15 為那十四隻羊羔,每隻要獻伊法十分之一。
na sehemu ya kumi ya efa ya hao wanakondoo kumi na nne.
16 並獻一隻公山羊為贖罪祭,這是在常獻的燔祭和同獻的素祭並同獻的奠祭以外。
Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi katika nyongeza ya sadaka ya kuteketezwa, sadaka yake ya unga, pamoja na sadaka za vinywaji.
17 「第二日要獻公牛犢十二隻,公綿羊兩隻,沒有殘疾、一歲的公羊羔十四隻;
Siku ya pili ya kusanyiko, mtatoa mafahari kumi na mbili, kondoo dume wawili na wanakondoo dume kumi na mbili wa umri wa mwaka mmoja, wote wakamilifu.
18 並為公牛、公羊,和羊羔,按數照例,獻同獻的素祭和同獻的奠祭。
Pamoja nao mtatoa sadaka ya unga, na sadaka ya vinywaji kwa ajili ya wale mafahari, kondoo dume, na kwa ajili ya wale wanakondoo, mkitoa sadaka nyingi kama ilvyoamriwa.
19 又要獻一隻公山羊為贖罪祭。這是在常獻的燔祭和同獻的素祭並同獻的奠祭以外。
Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kuwa nyongeza ya sadaka za kila siku, sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji.
20 「第三日要獻公牛十一隻,公羊兩隻,沒有殘疾、一歲的公羊羔十四隻;
Siku ya tatu ya kusanyiko, mtatoa sadaka mafahari kumi na moja, kondoo dume wawili, na wanakondoo dume kumi na nne wa umri wa mwaka mmoja, wakamilifu.
21 並為公牛、公羊,和羊羔,按數照例,獻同獻的素祭和同獻的奠祭。
Pamoja na hizo sadaka mtatoa sadaka ya unga na sdaka ya vinywaji kwa wale mafahari, kwa wale kondoo dume, na kwa wale wanakondoo, utoe sadaka nyingi kama ilivyoamriwa.
22 又要獻一隻公山羊為贖罪祭。這是在常獻的燔祭和同獻的素祭並同獻的奠祭以外。
Mtatoa sadaka beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya zile sadaka za kila siku, na sadaka zake za unga, na sadaka zake za vinywaji.
23 「第四日要獻公牛十隻,公羊兩隻,沒有殘疾、一歲的公羊羔十四隻;
Siku ya nne ya kusanyiko, mtatoa mafahari kumi, kondoo dume wawili, na wanakondoo dume kumi na nne wa mwaka mmoja, wakamilifu.
24 並為公牛、公羊,和羊羔,按數照例,獻同獻的素祭和同獻的奠祭。
Pamoja na sadaka hizo mtatoa sadaka za unga na sdaka za vinywaji kwa wale mafahari, na kwa wale kondoo dume na kwa wale wanakodoo, mtatoa sadaka nyingi kama ilivyoamriwa.
25 又要獻一隻公山羊為贖罪祭。這是在常獻的燔祭和同獻的素祭並同獻的奠祭以外。
Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kuwa nyongeza ya sadaka za kuteketezwa za kila siku, sadaka zake za unga, na sadaka zake za vinywaji
26 「第五日要獻公牛九隻,公羊兩隻,沒有殘疾、一歲的公羊羔十四隻;
Siku ya tano ya kusanyiko, mtatoa mafahari tisa, kondoo dume wawili, na wanakondoo dume kumi na nne wa mwaka mmoja, wakamilifu.
27 並為公牛、公羊,和羊羔,按數照例,獻同獻的素祭和同獻的奠祭。
Pamoja na sadaka hizo mtatoa sadaka za unga na sadaka ya vinywaji kwa ajili ya wale mafahari, kondoo dume, na wale wanakondoo, mkitoa sdaka nyingi kama ilivyoamriwa.
28 又要獻一隻公山羊為贖罪祭。這是在常獻的燔祭和同獻的素祭並同獻的奠祭以外。
Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya sadaka za kuteketezwa za kila siku, na sadaka zake za unga, na sadaka za vinywaji.
29 「第六日要獻公牛八隻,公羊兩隻,沒有殘疾、一歲的公羊羔十四隻;
Siku ya sita ya kusanyiko, mtatoa mafahari wanane, kondoo dume wawili, na wanakondoo kumi na nne wa mwaka mmoja, wakamilifu.
30 並為公牛、公羊,和羊羔,按數照例,獻同獻的素祭和同獻的奠祭。
Pamoja na sadaka hizo mtatoa sadaka za unga nasadaka za vinywaji kwa wale mafahari, kondoo wa dume na wale wanakondoo, mkitoa sadaka nyingi kama ilivyoamriwa.
31 又要獻一隻公山羊為贖罪祭。這是在常獻的燔祭和同獻的素祭並同獻的奠祭以外。
Mtatoa beberu kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya sadaka za kila siku za kuteketezwa, sadaka zadaka zake za unga, na sadaka zake za vinywaji.
32 「第七日要獻公牛七隻,公羊兩隻,沒有殘疾、一歲的公羊羔十四隻;
Siku ya saba ya kusanyiko, mtatoa mafahari saba, kondoo dume saba, na wanakondoo dume kumi na nne wa mwaka mmoja, wakamilifu.
33 並為公牛、公羊,和羊羔,按數照例,獻同獻的素祭和同獻的奠祭。
Pamoja nao mtataengeneza sadaka ya unga na sadaka ya vinywaji kwa ajili ya wale mafahari, na kondoo dume, na kwa wale wanakondoo, mkitoa sadaka nyingi kama ilivyoamriwa.
34 又要獻一隻公山羊為贖罪祭。這是在常獻的燔祭和同獻的素祭並同獻的奠祭以外。
Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya vinywaji.
35 「第八日你們當有嚴肅會;甚麼勞碌的工都不可做;
Siku ya nane mtakuwa na kusanyiko lingine makini. Hamtafanya kazi zenu za kila siku.
36 只要將公牛一隻,公羊一隻,沒有殘疾、一歲的公羊羔七隻作火祭,獻給耶和華為馨香的燔祭;
Mtafanya sadaka za kuteketezwa, sadaka iliyotengenezwa kwa moto ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa fahari mmoja, kondoo mmoja dume, na wanakondoo saba dume wa umri wa mwaka mmoja, wakamilifu.
37 並為公牛、公羊,和羊羔,按數照例,獻同獻的素祭和同獻的奠祭。
Mtatoa sadaka zake za unga na sadaka zake za vinywaji kwa ajili ya yule fahari, kondoo dume, na kwa wale wanakondoo, mkifanya sadaka nyingi kadri ilivyoamriwa.
38 又要獻一隻公山羊為贖罪祭。這是在常獻的燔祭和同獻的素祭並同獻的奠祭以外。
Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya sadaka za kila siku, na sadaka zake za unga, na sadaka zake za vinywaji.
39 「這些祭要在你們的節期獻給耶和華,都在所許的願並甘心所獻的以外,作為你們的燔祭、素祭、奠祭,和平安祭。」
Hivi ndivyo utakavyotoa sadaka kwa BWANA katika sikukuu zenu za kila mwaka. Hivi vitakuwa nyongeza ya viapo vyenu na sadaka zenu za hiari. Mtavitoa hivi kama sadaka zenu za kuteketezwa, sadaka za unga, sadaka za vinywaji, na sadaka za amani.”
40 於是,摩西照耶和華所吩咐他的一切話告訴以色列人。
Musa aliwaambia wana wa Israeli kila kitu ambacho BWANA alikuwa amemwamuru kusema.

< 民數記 29 >