< 利未記 1 >
Mungu alimwita Musa na alisema naye kutoka kweye hema la kukutania, akasema,
2 「你曉諭以色列人說:你們中間若有人獻供物給耶和華,要從牛群羊群中獻牲畜為供物。
“Sema na wana wa Israeli na uwaambie, 'Mwanaume yeyote miongoni mwenu akileta sadaka kwa Bwana, aleta kama matoleo katika wanyama wako, iwapo mifugo au katika kundi.”
3 「他的供物若以牛為燔祭,就要在會幕門口獻一隻沒有殘疾的公牛,可以在耶和華面前蒙悅納。
Kama matoleo yake ni ya sadaka ya kutekezwa kutoka katika kundi, atatoa dume asiyekuwa na kasoro. Atamtoa katika mlango wa kuingilia katika hema ya kukutania, ili iwe imekubaliwa mbele za Bwana.
4 他要按手在燔祭牲的頭上,燔祭便蒙悅納,為他贖罪。
Ataweka mikono yake kichwani pa sadaka ya kuteketezwa, na ndipo itakuwa imekubaliwa badala yake kufanya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe.
5 他要在耶和華面前宰公牛;亞倫子孫作祭司的,要奉上血,把血灑在會幕門口、壇的周圍。
Ndipo atapaswa kuchinja ng'ombe mbele ya Bwana. Watoto wa Aroni, makuhani wataleta damu na kuinyunyizia katika madhabahu iliyo katika mlango wa kuingilia katika hema la kukutania.
Ndipo ataichuna sadaka ya kuteketezwa na kuikata vipande.
Kisha wana wa Haruni kuhani wataweka moto katika madhabahu na kuweka kuni ili kuchochea moto.
8 亞倫子孫作祭司的,要把肉塊和頭並脂油擺在壇上火的柴上。
Wana wa Haruni, makuhani wataweka vipande, kichwa na mafuta, watazipanga juu ya kuni zilizoko juu ya moto ulio madhabahuni.
9 但燔祭的臟腑與腿要用水洗。祭司就要把一切全燒在壇上,當作燔祭,獻與耶和華為馨香的火祭。
Lakini matumbo yake na miguu lazima ataiosha kwa maji. Kisha kuhani atateketeza kila kitu kilicho juu ya madhabahu kama sadaka ya kuteketeza. Italeta harufu nzuri sana kwangu; itakuwa sadaka iliyotolewa kwa moto kwa ajili yangu.
10 「人的供物若以綿羊或山羊為燔祭,就要獻上沒有殘疾的公羊。
Kama sadaka kwa ajili ya sadaka ya kuteketeza kutoka kundi, kondoo au mbuzi, lazima atoe dume asiye na kasoro.
11 要把羊宰於壇的北邊,在耶和華面前;亞倫子孫作祭司的,要把羊血灑在壇的周圍。
Lazima atamchinja juu ya madhabahu iliyo katika upande wa kaskazini mbele ya Bwana. Wana wa Haruni makuhani, watanyunyiza damu kila upande wa madhabahu.
12 要把燔祭牲切成塊子,連頭和脂油,祭司就要擺在壇上火的柴上;
Kisha ataikata katika vipande, pamoja na kichwa na mafuta yake, kuhani atavipanga juu ya kuni zilizo katika moto ulio madhabahuni,
13 但臟腑與腿要用水洗,祭司就要全然奉獻,燒在壇上。這是燔祭,是獻與耶和華為馨香的火祭。
lakini matumbo yake na miguu yake lazima ioshwe kwa maji. Kisha kuhani atatoa yote na kuiteketeza juu ya madhabahu. Ni sadaka ya kuteketezwa, italeta harufu nzuri kwa ajili ya Bwana; itakuwa sadaka ya Bwana iliyotolewa kwa moto.
14 「人奉給耶和華的供物,若以鳥為燔祭,就要獻斑鳩或是雛鴿為供物。
Kama sadaka yake kwa Bwana itakuwa ni sadaka ya kuteketezwa ni ndege, ndipo ataleta kama sadaka yake aidha ni huwa au kinda la njiwa.
15 祭司要把鳥拿到壇前,揪下頭來,把鳥燒在壇上;鳥的血要流在壇的旁邊;
Kuhani ataileta madhabahuni, atamnyonga kichwa chake, na kuiteketeza juu ya madhabahu. Kisha damu yake itachuruzishwa juu ya pande za madhabahu.
16 又要把鳥的嗉子和髒物除掉,丟在壇的東邊倒灰的地方。
Kisha atakiondoa kibofu chake pamoja na uchafu wake, na kukiweka upande wa mashariki mwa madhabahu, katika sehemu ya majivu.
17 要拿着鳥的兩個翅膀,把鳥撕開,只是不可撕斷;祭司要在壇上、在火的柴上焚燒。這是燔祭,是獻與耶和華為馨香的火祭。」
Kisha atapasua mabawa yake, lakini hatagawanya katika vipande viwili. Kisha Kuhani atamtekeza katika madhabahu, juu ya kuni amabazo ziko juu ya moto. Itakuwa sadaka ya kuteketezwa, na italeta harufu nzuri sana kwa Bwana; itakuwa sadaka ya Bwana iliyotolewa kwa moto.