< 士師記 9 >

1 耶路‧巴力的兒子亞比米勒到了示劍見他的眾母舅,對他們和他外祖全家的人說:
Abimeleki, mwana wa Yerubaali, akaenda kwa jamaa za mama yake huko Shekemu, akawaambia, na jamaa yote ya mama yake,
2 「請你們問示劍的眾人說,是耶路‧巴力的眾子七十人都管理你們好呢?還是一人管理你們好呢?你們又要記念我是你們的骨肉。」
Tafadhali sema haya, ili wakuu wote wa Shekemu wasikie, Ni kipi bora kwako Je, wana sabini wote wa Yerubali kutawala juu yenu, au kwamba moja tu atawale juu yenu? Kumbuka kwamba mimi ni mfupa na nyama yenu.
3 他的眾母舅便將這一切話為他說給示劍人聽,示劍人的心就歸向亞比米勒。他們說:「他原是我們的弟兄」;
Ndugu za mama yake waliongea kwa niaba yake kwa viongozi wa Shekemu, nao wakakubali kumfuata Abimeleki, wakasema, Yeye ndiye ndugu yetu.
4 就從巴力‧比利土的廟中取了七十舍客勒銀子給亞比米勒;亞比米勒用以雇了些匪徒跟隨他。
Wakampa vipande sabini vya fedha katika nyumba ya Baali Berith; Abimeleki akazitumia kwa kuajiri watu wasio na sheria na wasiokuwa wajinga, waliomfuata.
5 他往俄弗拉到他父親的家,將他弟兄、耶路‧巴力的眾子七十人都殺在一塊磐石上;只剩下耶路‧巴力的小兒子約坦,因為他躲藏了。
Abimeleki akaenda nyumbani kwa baba yake huko Ofra; na juu ya jiwe moja akawaua ndugu zake sabini, wana wa Yerubaali. Yotamu ndiye aliyebaki, mwana mdogo kabisa wa Yerubaali, kwa kuwa alijificha.
6 示劍人和米羅人都一同聚集,往示劍橡樹旁的柱子那裏,立亞比米勒為王。
Wakuu wote wa Shekemu na Beth Milo wakaungana, wakaenda kumfanya Abimeleki mfalme, karibu na mwaloni karibu na nguzo iliyoko Shekemu.
7 有人將這事告訴約坦,他就去站在基利心山頂上,向眾人大聲喊叫說:「示劍人哪,你們要聽我的話,上帝也就聽你們的話。
Yotamu alipoambiwa juu ya jambo hilo, akaenda, akasimama juu ya Mlima Gerizimu. Alipiga kelele akawaambia, 'Sikilizeni, enyi viongozi wa Shekemu, ili Mungu awasikilize.
8 有一時,樹木要膏一樹為王,管理他們,就去對橄欖樹說:『請你作我們的王。』
Siku moja miti ilikwenda kumtia mafuta mfalme juu yao. Wakauambia mzeituni, tawala juu yetu.
9 橄欖樹回答說:『我豈肯止住供奉神和尊重人的油,飄颻在眾樹之上呢?』
Lakini mti wa mizeituni ukawaambia, Je! Nitaacha mafuta yangu, ambayo hutumiwa kuheshimu miungu na wanadamu, ili nipate kurudi na kuvuka juu ya miti mingine?
10 樹木對無花果樹說:『請你來作我們的王。』
Miti hiyo ikamwambia mtini, 'Njoo utawale juu yetu.'
11 無花果樹回答說:『我豈肯止住所結甜美的果子,飄颻在眾樹之上呢?』
Lakini mtini ukawaambia, Je, nitaacha utamu wangu na matunda yangu mazuri, ili nipate kurudi na kuvuka juu ya miti mingine?
12 樹木對葡萄樹說:『請你來作我們的王。』
Miti hiyo ikamwambia mzabibu, 'Njoo utawale juu yetu.'
13 葡萄樹回答說:『我豈肯止住使神和人喜樂的新酒,飄颻在眾樹之上呢?』
Mzabibu ukawaambia, Je, nitaacha divai yangu mpya, ambayo hufurahisha miungu na wanadamu, na kurudi na kuvuka juu ya miti mingine?
14 眾樹對荊棘說:『請你來作我們的王。』
Kisha miti yote ikawaambia mchanga, 'Njoo utawale juu yetu.'
15 荊棘回答說:『你們若誠誠實實地膏我為王,就要投在我的蔭下;不然,願火從荊棘裏出來,燒滅黎巴嫩的香柏樹。』
Miti ya miiba ikaiambia miti, 'Ikiwa unataka kunipaka mafuta niwe mfalme juu yako, njoo na upate usalama chini ya kivuli changu. Ikiwa sivyo, basi moto lazima uondoke kwenye mchanga na uiteketeze mierezi ya Lebanoni. '
16 「現在你們立亞比米勒為王,若按誠實正直善待耶路‧巴力和他的全家,這就是酬他的勞。
Basi, ikiwa umefanya kweli na uaminifu, ulimfanya Abimeleki mfalme, na ikiwa umefanya vizuri juu ya Yerubaali na nyumba yake, na ikiwa umemuadhibu kama anavyostahili,
17 從前我父冒死為你們爭戰,救了你們脫離米甸人的手。
- na kufikiri kwamba baba yangu alipigana kwa ajili yenu, akahatarisha maisha yake, na akawaokoa kutoka kwenye mkono wa Midiani -
18 你們如今起來攻擊我的父家,將他眾子七十人殺在一塊磐石上,又立他婢女所生的兒子亞比米勒為示劍人的王;他原是你們的弟兄。
lakini leo umeamka juu ya nyumba ya baba yangu na kuwaua watoto wake, watu sabini, juu ya jiwe moja. Na umemfanya Abimeleki, mwana wa mtumishi wake, awe mfalme juu ya wakuu wa Shekemu, kwa sababu yeye ni ndugu yenu.
19 你們如今若按誠實正直待耶路‧巴力和他的家,就可因亞比米勒得歡樂,他也可因你們得歡樂;
Ikiwa mlifanya kwa uaminifu na uelekevu pamoja na Jerubalai na nyumba yake, basi mnapaswa kufurahi katika Abimeleki, naye apate kufurahi ndani yenu.
20 不然,願火從亞比米勒發出,燒滅示劍人和米羅眾人,又願火從示劍人和米羅人中出來,燒滅亞比米勒。」
Lakini ikiwa sio, moto utoke kwa Abimeleki, ukawaangamize watu wa Shekemu na Beth Milo. Basi moto utoke kwa watu wa Shekemu na Beth Milo, ili kumteketeza Abimeleki.
21 約坦因怕他弟兄亞比米勒,就逃跑,來到比珥,住在那裏。
Yothamu akakimbia, naye akaenda Beeri. Aliishi huko kwa sababu ilikuwa mbali na Abimeleki, kaka yake.
22 亞比米勒管理以色列人三年。
Abimeleki akatawala juu ya Israeli kwa miaka mitatu.
23 上帝使惡魔降在亞比米勒和示劍人中間,示劍人就以詭詐待亞比米勒。
Mungu alituma roho mbaya kati ya Abimeleki na viongozi wa Shekemu. Viongozi wa Shekemu walisaliti uaminifu waliokuwa nao kwa Abimeleki.
24 這是要叫耶路‧巴力七十個兒子所受的殘害歸與他們的哥哥亞比米勒,又叫那流他們血的罪歸與幫助他殺弟兄的示劍人。
Mungu alifanya hivyo ili uhalifu uliofanywa kwa wana sabini wa Yerubaali uweze kulipizwa kisasi, na Abimeleki ndugu yao atawajibishwa kwa kuwaua, na watu wa Shekemu watawajibishwa kwa sababu walimsaidia kuua ndugu zake.
25 示劍人在山頂上設埋伏,等候亞比米勒。凡從他們那裏經過的人,他們就搶奪。有人將這事告訴亞比米勒。
Basi wakuu wa Shekemu wakawaweka wanaume wamkisubiri juu ya vilima ili wamwangamize, nao wakawaibia wote waliokuwa wamepita katika barabara hiyo. Hii iliripotiwa kwa Abimeleki.
26 以別的兒子迦勒和他的弟兄來到示劍,示劍人都信靠他。
Gaali mwana wa Ebedi akenda pamoja na ndugu zake, wakavuka Shekemu. Viongozi wa Shekemu walimwamini.
27 示劍人出城到田間去,摘下葡萄,踹酒,設擺筵宴,進他們神的廟中吃喝,咒詛亞比米勒。
Wakaenda shambani wakakusanya zabibu kutoka kwa mizabibu, nao wakazikanyaga. Walifanya sherehe katika nyumba ya mungu wao, walikula na kunywa, kumlaani Abimeleki.
28 以別的兒子迦勒說:「亞比米勒是誰?示劍是誰?使我們服事他呢?他不是耶路‧巴力的兒子嗎?他的幫手不是西布勒嗎?你們可以服事示劍的父親哈抹的後裔。我們為何服事亞比米勒呢?
Gaali mwana wa Ebedi, akasema, Abimeleki ni nani, na Shekemu ni nani, hata tumtumikie? Je, si mwana wa Yerubaali? Na Zebuli si afisa wake? Watumikieni watu wa Hamori, baba yake Shekemu! Kwa nini tunapaswa kumtumikia?
29 惟願這民歸我的手下,我就除掉亞比米勒。」迦勒又對亞比米勒說:「增添你的軍兵出來吧。」
Laiti watu hawa wangekukuwa chini ya amri yangu! Kisha ningemuondoa Abimeleki. Ningemwambia Abimeleki, 'liondoe nje jeshi lako lote.'
30 邑宰西布勒聽見以別的兒子迦勒的話,就發怒,
Zebul, mkuu wa mji, aliposikia maneno ya Gaali, mwana wa Ebedi, hasira yake ikawaka.
31 悄悄地打發人去見亞比米勒,說:「以別的兒子迦勒和他的弟兄到了示劍,煽惑城中的民攻擊你。
Akatuma wajumbe kwa Abimeleki ili wapate kudanganya, akisema, Tazama, Gaali mwana wa Ebedi na ndugu zake wanafika Shekemu; nao wanauchochea mji dhidi yako.
32 現在你和跟隨你的人今夜起來,在田間埋伏。
Sasa, amka wakati wa usiku, wewe na askari pamoja nawe, na uandae uvamizi katika mashamba.
33 到早晨太陽一出,你就起來闖城。迦勒和跟隨他的人出來攻擊你的時候,你便向他們見機而做。」
Kisha asubuhi, jua litakapokwisha, inuka mapema na uangamize mji. Na yeye na watu waliokuwa pamoja naye watakapokuja juu yenu, fanyeni chochote mnachoweza.
34 於是,亞比米勒和跟隨他的眾人夜間起來,分作四隊,埋伏等候示劍人。
Basi Abimeleki akainuka usiku, yeye na watu wote waliokuwa pamoja naye, wakaandaa uvamizi dhidi ya Shekemu, wakagawanyika vitengo vinne.
35 以別的兒子迦勒出去,站在城門口。亞比米勒和跟隨他的人從埋伏之處起來。
Gaali mwana wa Ebedi akatoka, akasimama penye mlango wa mji. Abimeleki na watu waliokuwa pamoja naye wakatoka mahali pa kuficha.
36 迦勒看見那些人,就對西布勒說:「看哪,有人從山頂上下來了。」西布勒說:「你看見山的影子,以為是人。」
Gaali alipowaona hao watu, akamwambia Zebuli, “Tazama, watu wanatoka kwenye vilima!” Zebuli akamwambia, “Wewe unaona vivuli juu ya vilima kama vile watu”.
37 迦勒又說:「看哪,有人從高處下來,又有一隊從米惡尼尼橡樹的路上而來。」
Gaali akaongea tena na kusema, “Angalia, watu wanashuka katikati ya nchi, na kitengo kimoja kinakuja kwa njia ya mwaloni wa Maenenimu.”
38 西布勒對他說:「你曾說,亞比米勒是誰,叫我們服事他?你所誇的口在哪裏呢?這不是你所藐視的民嗎?你現在出去,與他們交戰吧!」
Ndipo Zebuli akamwambia, “Je, maneno yako ya kiburi yako wapi sasa, wewe uliyesema, 'Abimeleki ni nani, ili tumtumikie?' Je, hao sio watu ambao uliwadharau? Toka sasa na pigana nao.”
39 於是迦勒率領示劍人出去,與亞比米勒交戰。
Gaali akatoka na alikuwa akiwaongoza watu wa Shekemu, naye alipigana na Abimeleki.
40 亞比米勒追趕迦勒;迦勒在他面前逃跑,有許多受傷仆倒的,直到城門。
Abimeleki akamfukuza, na Gaali akakimbia mbele yake. Na wengi wakaanguka na majeraha ya mauti mbele ya mingilio ya lango la mji.
41 亞比米勒住在亞魯瑪。西布勒趕出迦勒和他弟兄,不准他們住在示劍。
Abimeleki alikaa Aruma. Zebul akawalazimisha Gaal na ndugu zake watoke Shekemu.
42 次日,民出到田間,有人告訴亞比米勒;
Siku ya pili watu wa Shekemu wakatoka shambani, na habari hii ikamfikia Abimeleki.
43 他就把他的人分作三隊,埋伏在田間,看見示劍人從城裏出來,就起來擊殺他們。
Aliwachukua watu wake, akawagawanywa katika vitengo vitatu, na wakaandaa uvamizi mashambani. Aliangalia na kuona watu wakitoka mjini. Akawakamata na kuwaua.
44 亞比米勒和跟隨他的一隊向前闖去,站在城門口;那兩隊直闖到田間,擊殺了眾人。
Abimeleki na vitengo vilivyokuwa pamoja naye vilishambulia na kuzuia maingilio ya lango la mji. Vitengo vingine viwili vilishambulia wote waliokuwa katika shamba na wakawaua.
45 亞比米勒整天攻打城,將城奪取,殺了其中的居民,將城拆毀,撒上了鹽。
Abimeleki alipigana na huo mji siku nzima. Aliteka mji huo, na kuwaua watu waliokuwa ndani yake. Akabomoa kuta za mji na kueneza chumvi juu yake.
46 示劍樓的人聽見了,就躲入巴力‧比利土廟的衛所。
Wakati wakuu wote wa mnara wa Shekemu waliposikia hayo, waliingia katika ngome ya nyumba ya El Berithi.
47 有人告訴亞比米勒說:「示劍樓的人都聚在一處。」
Abimeleki aliambiwa kuwa viongozi wote walikuwa wamekusanyika pamoja kwenye mnara wa Shekemu.
48 亞比米勒和跟隨他的人就都上撒們山。亞比米勒手拿斧子,砍下一根樹枝,扛在肩上,對跟隨他的人說:「你們看我所行的,也當趕緊照樣行。」
Abimeleki akaenda mpaka mlima wa Salmoni, yeye na watu wote waliokuwa pamoja naye. Abimeleki akachukua shoka na kukata matawi. Akaweka juu ya bega lake na kuwaagiza watu waliokuwa pamoja naye, 'Mlichoona nimekifanya fanyeni kama nilivyofanya.'
49 眾人就各砍一枝,跟隨亞比米勒,把樹枝堆在衛所的四圍,放火燒了衛所,以致示劍樓的人都死了,男女約有一千。
Basi kila mmoja akakata matawi, wakamfuata Abimeleki. Wakayafungia juu ya ukuta wa mnara, nao wakawasha moto, hata watu wote wa mnara wa Shekemu wakafa, wanaume na wanawake elfu.
50 亞比米勒到提備斯,向提備斯安營,就攻取了那城。
Abimeleki akaenda Tebezi, naye akapiga kambi dhidi ya Thebezi, akautwaa.
51 城中有一座堅固的樓;城裏的眾人,無論男女,都逃進樓去,關上門,上了樓頂。
Lakini kulikuwa na mnara wenye nguvu katika mji, wanaume na wanawake wote na viongozi wote wa mji walikimbilia na kujifungia wenyewe. Kisha wakaenda juu ya paa la mnara.
52 亞比米勒到了樓前攻打,挨近樓門,要用火焚燒。
Abimeleki alikwenda kwenye mnara na kupigana nao, naye akaenda karibu na mlango wa mnara ili kuuchoma.
53 有一個婦人把一塊上磨石拋在亞比米勒的頭上,打破了他的腦骨。
Lakini mwanamke akatupa jiwe la juu, juu ya kichwa cha Abimeleki likavunja fuvu lake.
54 他就急忙喊叫拿他兵器的少年人,對他說:「拔出你的刀來,殺了我吧!免得人議論我說,他為一個婦人所殺。」於是少年人把他刺透,他就死了。
Kisha akamwita yule kijana aliyekuwa anamchukulia silaha zake, akamwambia, “Chukua upanga wako ukaniue, kwa hiyo hakuna mtu atakayesema juu yangu, 'Mwanamke alimwua.'” Basi kijana wake akamchoma naye akafa.
55 以色列人見亞比米勒死了,便各回自己的地方去了。
Watu wa Israeli walipoona kwamba Abimeleki amekufa, wakaenda nyumbani.
56 這樣,上帝報應亞比米勒向他父親所行的惡,就是殺了弟兄七十個人的惡。
Basi Mungu akalipiza kisasi cha uovu wa Abimeleki alichomfanyia baba yake kwa kuua ndugu zake sabini.
57 示劍人的一切惡,上帝也都報應在他們頭上;耶路‧巴力的兒子約坦的咒詛歸到他們身上了。
Mungu akafanya uovu wote wa watu wa Shekemu ugeuke juu ya vichwa vyao wenyewe, na juu yao ilikuja laana ya Yothamu mwana wa Yerubaali.

< 士師記 9 >