< 約伯記 8 >

1 書亞人比勒達回答說:
Kisha Bildadi huyo Mshuhi akajibu na kusema,
2 這些話你要說到幾時? 口中的言語如狂風要到幾時呢?
“hata lini wewe utasema mambo haya? Kwa muda gani maneno ya kinywa chako yatakuwa kama upepo wenye nguvu?
3 上帝豈能偏離公平? 全能者豈能偏離公義?
Je Mungu hupotosha hukumu? Je Mwenyezi hupotosha haki?
4 或者你的兒女得罪了他; 他使他們受報應。
Watoto wako wametenda dhambi dhidi yake; tunalifahamu hili, kwa kuwa amewatia mkononi kwa makosa yao.
5 你若殷勤地尋求上帝, 向全能者懇求;
Lakini wewe unaonaje ukimtafuta Mungu kwa bidii na kufikisha haja yako kwa huyo Mwenyezi.
6 你若清潔正直, 他必定為你起來, 使你公義的居所興旺。
Ukiwa wewe ni msafi na mkamilifu, hakika angeamka mwenyewe kwa niaba yako na kukurudisha kwenye makazi ya haki yako.
7 你起初雖然微小, 終久必甚發達。
Japokuwa huo mwanzo wako ulikuwa ni mdogo, hata hivyo hali yako ya mwisho itaongezeka sana.
8 請你考問前代, 追念他們的列祖所查究的。
Tafadhari uwaulize vizazi vya zamani, na utie bidii katika hayo mababu zetu waliyojifunza.
9 我們不過從昨日才有,一無所知; 我們在世的日子好像影兒。
(Sisi ni wa jana tu na hatujui chochote kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli).
10 他們豈不指教你,告訴你, 從心裏發出言語來呢?
Je hawatakufunza wao na kukuambia? Je hawatatamka maneno yatokayo mioyoni mwao?
11 蒲草沒有泥豈能發長? 蘆荻沒有水豈能生發?
Je hayo mafunjo yaota pasipo matope? Je mafunjo yaota pasipo maji?
12 尚青的時候,還沒有割下, 比百樣的草先枯槁。
Wakati yakiwa bado ya kijani na hayajakatwa, hunyauka kabla ya mmea mwingine.
13 凡忘記上帝的人,景況也是這樣; 不虔敬人的指望要滅沒。
Hivyo pia njia ya wote wamsahauo Mungu, na matumaini ya asiyeamini Mungu yatatoweka.
14 他所仰賴的必折斷; 他所倚靠的是蜘蛛網。
Ujasiri wake utavunjika, na matumaini yake ni dhaifu kama utando wa buibui.
15 他要倚靠房屋,房屋卻站立不住; 他要抓住房屋,房屋卻不能存留。
Ataitegemea nyumba yake, lakini haitamsaidia; atashikamana nayo, lakini isidumu.
16 他在日光之下發青, 蔓子爬滿了園子;
Yeye huwa mti mbichi chini ya jua, na machipukizi yake huenea katika bustani yake yote.
17 他的根盤繞石堆, 扎入石地。
Mizizi yake hujifunga funga kwenye rundo la mawe; huangalia mahali pazuri katikati ya mawe;
18 他若從本地被拔出, 那地就不認識他,說: 我沒有見過你。
Lakini mtu huyu aking'olewa mahali pake, kisha mahali pale patamkana, na kusema, 'mimi sikukuona.'
19 看哪,這就是他道中之樂; 以後必另有人從地而生。
Tazama, hii ni “furaha” ya mtu mwenye tabia hiyo; mimea mingine itachipuka toka katika udongo ule ule mahali pake.
20 上帝必不丟棄完全人, 也不扶助邪惡人。
Tazama, Mungu hatamtupa mtu asiye na kosa; wala hatawathibitisha watendao uovu.
21 他還要以喜笑充滿你的口, 以歡呼充滿你的嘴。
Yeye atakijaza kinywa chako na kicheko, midomo yako na shangwe.
22 恨惡你的要披戴慚愧; 惡人的帳棚必歸於無有。
Wale ambao wanakuchukia wewe watavishwa aibu; nayo hema yake mwovu haitakuwepo tena.

< 約伯記 8 >