Preface
Read
+
Publisher
Nainoia, Inc.
PO Box 462, Bellefonte, PA 16823
(814) 470-8028
Nainoia Inc, Publisher
LinkedIn/NAINOIA-INC
Third Party Publisher Resources
Request Custom Formatted Verses
Please contact us below
Submit your proposed corrections
I understand that the Aionian Bible republishes public domain and Creative Commons Bible texts and that volunteers may be needed to present the original text accurately. I also understand that apocryphal text is removed and most variant verse numbering is mapped to the English standard. I have entered my corrections under the verse(s) below. Proposed corrections to the New Swahili Bible, Exodus Chapter 38 https://www.AionianBible.org/Bibles/Swahili---New-Swahili-Bible/Exodus/38 1) Naye akafanya madhabahu ya toleo la kuteketezwa kwa mbao za mshita. Mikono mitano urefu wake, na mikono mitano upana wake, ilikuwa mraba, na mikono mitatu kimo chake. 2) Halafu akafanya pembe zake kwenye zile ncha zake nne. Pembe zake zilitoka kwake. Kisha akaifunika kwa shaba. 3) Baada ya hilo akavifanya vyombo vyote vya madhabahu, yale makopo na zile sepetu na yale mabakuli, zile nyuma na vile vyetezo. Vyombo vyake vyote alivifanya kwa shaba. 4) Tena akaifanyia madhabahu kiunzi cha fito, mtandao wa shaba, chini ya ukingo wake, chini kuelekea katikati yake. 5) Halafu akatengeneza pete nne kwenye ile miisho minne karibu na kile kiunzi cha shaba, ili kuitegemeza ile miti. 6) Bezaleli akafanya miti ya mshita na kuifunika kwa shaba. 7) Kisha akaitia ile miti kwenye zile pete zilizo pande za madhabahu ili kuibeba. Akaifanya kuwa sanduku la mbao lenye uwazi. 8) Kisha akafanya beseni ya shaba na kinara chake cha shaba. Kwa kutumia vioo vya watumishi wanawake ambao walifanya utumishi uliopangwa kwenye mwingilio wa hema la mkutano. 9) Naye akafanya ule ua. Upande unaokabili Negebu, kuelekea kusini, mapazia ya ua yalikuwa ya kitani bora kilichosokotwa, kwa mikono mia moja. 10) Nguzo zake ishirini na vikalio vyake ishirini vilikuwa vya shaba. Misumari ya nguzo na viungo vyake vilikuwa vya fedha 11) Pia, kwa ajili ya upande wa kaskazini kulikuwa na mikono mia. Nguzo zake ishirini na vikalio vyake ishirini vilikuwa vya shaba. Misumari ya nguzo na viungo vyake vilikuwa vya fedha. 12) Lakini kwa ajili ya upande wa magharibi mapazia yalikuwa mikono hamsini. Nguzo zake zilikuwa kumi na vikalio vyake kumi. Misumari ya nguzo na viungo vyake vilikuwa vya fedha. 13) Na kwa ajili ya upande wa mashariki kulikuwa na mikono hamsini. 14) Mapazia yalikuwa mikono kumi na mitano kwa upande mmoja. Nguzo zake zilikuwa tatu na vikalio vyake vitatu. 15) Na kwa ajili ya upande ule mwingine, huu na ule, wa lango la ua, mapazia yalikuwa mikono kumi na mitano. Nguzo zake zilikuwa tatu na vikalio vyake vitatu. 16) Mapazia yote ya ua kuzunguka pande zote yalikuwa ya kitani bora kilichosokotwa. 17) Navyo vikalio vya nguzo vilikuwa vya shaba. Vibanio vya vikalio na viungo vyake vilikuwa vya fedha navyo vilifunikwa kwa shaba sehemu ya juu, na kulikuwa na viungo vya shaba kwa ajili ya nguzo zote za ua. 18) Nacho kisitiri cha lango la ua kilikuwa na mikono ishirini urefu. Cha uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa, na urefu wake ulikuwa mikono ishirini, nacho kimo kotekote kilikuwa mikono mitano sawasawa na mapazia ya ua. 19) Na nguzo zake nne na vikalio vyake vinne vilikuwa vya shaba. Misumari yake ilikuwa ya fedha na utando wa vichwa vyake na viungo vyake ulikuwa wa fedha. 20) Na misumari yote ya hema kwa ajili ya maskani na kwa ajili ya ua kuzunguka pande zote ilikuwa ya shaba 21) Hivi ndivyo vitu vilivyohesabiwa vya maskani, maskani ya Ushuhuda, vilivyohesabiwa kwa amri ya Musa, kuwa utumishi wa Walawi chini ya uongozi wa Ithamari mwana wa Aruni kuhani. 22) Naye Bezaleli mwana wa Uri mwana wa Huru wa kabila la Yuda alifanya yote ambayo Yahweh alikuwa amemwamuru Musa. 23) Na pamoja naye alikuwa Oholiabu mwana wa Ahisamaki wa kabila la Dani, fundi na mtarizi na mfumaji wa uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora. 24) Dhahabu yote iliyotumiwa kwa ajili ya kazi katika kazi yote ya mahali patakatifu ikawa jumla ya dhahabu ya toleo la kutikisa, talanta ishirini na tisa na shekeli 730 kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. 25) Nayo fedha ya wale walioandikishwa kati ya kusanyiko ilikuwa talanta mia moja na shekeli 1, 775 kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, 26) ile nusu shekeli kwa ajili ya mtu mmoja ilikuwa nusu shekeli kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, Kwa kila mtu aliyekuwa akipita kuingia upande wa wale waliokuwa wameandikishwa kuanzia miaka ishirini na zaidi, jumla ya watu 603, 550. 27) Na talanta mia moja za fedha zilitumiwa kutengeneza vikalio vya mahali patakatifu na vikalio vya lile pazia. Vikalio mia moja vilitoshana na talanta mia moja, talanta moja kwa kikalio kimoja. 28) Na kutokana na zile shekeli 1, 775 alifanyiza vibanio vya nguzo na kuvifunika sehemu yake ya juu na kuviunganisha pamoja. 29) Nayo shaba ya toleo la kutikisa ilikuwa talanta sabini na shekeli 2, 400. 30) Naye akaitumia kufanya vile vikalio vya mwingilio wa hema la mkutano na ile madhabahu ya shaba na kile kiunzi chake cha shaba, na vyombo vyote vya madhabahu, 31) na vile vikalio vya ua kuzunguka pande zote, na vile vikalio vya lango la ua, na misumari yote ya maskani na misumari yote ya ua kuzunguka pande zote. Additional comments?
Refresh Captcha
The world's first Holy Bible un-translation!