Preface
Read
+
Publisher
Nainoia, Inc.
PO Box 462, Bellefonte, PA 16823
(814) 470-8028
Nainoia Inc, Publisher
LinkedIn/NAINOIA-INC
Third Party Publisher Resources
Request Custom Formatted Verses
Please contact us below
Submit your proposed corrections
I understand that the Aionian Bible republishes public domain and Creative Commons Bible texts and that volunteers may be needed to present the original text accurately. I also understand that apocryphal text is removed and most variant verse numbering is mapped to the English standard. I have entered my corrections under the verse(s) below. Proposed corrections to the Swahili Contemporary Version, Proverbs Chapter 1 https://www.AionianBible.org/Bibles/Swahili---Contemporary/Proverbs 1) Mithali za Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli: 2) Kwa kupata hekima na nidhamu; kwa kufahamu maneno ya busara; 3) kwa kujipatia nidhamu na busara, kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea; 4) huwapa busara wajinga, maarifa na akili kwa vijana; 5) wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao, wenye kupambanua na wapate mwongozo; 6) kwa kufahamu mithali na mifano, misemo na vitendawili vya wenye hekima. 7) Kumcha Bwana ndicho chanzo cha maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu. 8) Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako, wala usiyaache mafundisho ya mama yako. 9) Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako, na mkufu wa kuipamba shingo yako. 10) Mwanangu, kama wenye dhambi wakikushawishi, usikubaliane nao. 11) Kama wakisema, “Twende tufuatane; tukamvizie mtu na kumwaga damu, njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia; 12) tuwameze wakiwa hai kama kaburi, wakiwa wazima kama wale wanaotumbukia shimoni. (Sheol h7585) 13) Tutapata aina zote za vitu vya thamani na kujaza nyumba zetu kwa nyara. 14) Njoo ushirikiane nasi, vitu vyote tutakavyopata tutagawana.” 15) Mwanangu, usiandamane nao. Usiweke mguu wako katika njia zao, 16) kwa kuwa miguu yao hukimbilia kwenye dhambi, ni wepesi kumwaga damu. 17) Tazama ni jinsi gani ilivyo kazi bure kutandaza wavu wakati ndege wote wanakuona! 18) Watu hawa huvizia kumwaga damu yao wenyewe; hujivizia tu wenyewe! 19) Huu ndio mwisho wa wote ambao wanajipatia mali kwa hila; huuondoa uhai wa wale wenye mali. 20) Hekima huita kwa sauti kuu barabarani, hupaza sauti yake kwenye viwanja vikubwa; 21) kwenye makutano ya barabara za mji zenye makelele mengi hupaza sauti, kwenye malango ya mji hutoa hotuba yake: 22) “Enyi wajinga, mtangʼangʼania ujinga wenu hadi lini? Mpaka lini wenye mizaha watafurahia mizaha, na wapumbavu kuchukia maarifa? 23) Kama mngekuwa mmeitikia karipio langu, ningekuwa nimemimina roho yangu kwenu na kuwafahamisha maneno yangu. 24) Lakini kwa kuwa mlinikataa nilipowaita na hakuna yeyote aliyekubali niliponyoosha mkono wangu, 25) kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote na hamkukubali karipio langu, 26) mimi nami nitawacheka katika maafa yenu, nitawadhihaki wakati janga litawapata: 27) wakati janga litawapata kama tufani, wakati maafa yatawazoa kama upepo wa kisulisuli, wakati dhiki na taabu zitawalemea. 28) “Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu; watanitafuta lakini hawatanipata. 29) Kwa kuwa walichukia maarifa, wala hawakuchagua kumcha Bwana, 30) kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu, na kukataa maonyo yangu, 31) watakula matunda ya njia zao, na watashibishwa matunda ya hila zao. 32) Kwa kuwa ukaidi wa wajinga utawaua, nako kuridhika kwa wajinga kutawaangamiza. 33) Lakini yeyote anisikilizaye ataishi kwa usalama, atatulia, bila kuwa na hofu ya madhara.” Additional comments?
Refresh Captcha
The world's first Holy Bible un-translation!